Urithi

Richbest

Senior Member
Joined
May 23, 2011
Posts
101
Reaction score
24
Habari wapendwa! Nimekua nikisumbuliwa sana na usingizi badae nimekuja kugundua inawezekana nikawa nimerithi kutoka kwa mama maana nimegundua ana usingizi sana akitulia tu kidogo analala sasa mimi ni mwanafunzi na hii kitu inanitesa sana.Je inawezekana kitu kama hicho na nawezaje kulishinda kulitibu.Asanten sana na jion njema:yawn::yawn:
 
Pole sana richebest hilo siyo tatizo la kurithi l ni lakuambukizwa . Pale mbungho (tse tse fly) anafanana na inzi ila yeye mkubwa ,akimung'ata mtu mwenye parasite aina ya trypanosoma brucei rhodensience akija kukung'ata wewe tayari nawewe atakuambukiza hilo tatizo, Kama mama yako atakuwa na huo ugonjwa wa sleeping sicknes atakuwa amekuambukiza kupitia huyo mbungh'o(tse tse fly) . Kwa upande mwingine inaweza kuwa chakula unachokula jaribu kuangali chakula kama jamii ya ndizi huwa zina chemical aina ya serotonin ambayo inafanya una sinzia sana lakini siyo tatizo wala si ugonjwa ni hali ya kawaida, ila ndizi ina faida nyingi za kiafya. Pia madawa ya hospitali huchangia hilo tatizo.ebu tueleze vizuri huwa unalala masaa mangapi
 
Tatizo limekuanza lini? Unasinzia masaa mangapi katika masaa 24? Ulishawahia tumia madawa ya usingizi madawa ya kuzuia wasiwasi, au yale yakupunguza mawazo?, . Kwa wingi unakula chakula cha aina gani?
 
Tatiza limeanza kama miaka 6 iliyopita ila naona kama linaongezeka mwanzon ilikuwa ni kidogo kawaida naweza nikasinzia kwa muda wa saa moja au chin ya hapo huwa napanda kitandan saa nne na nusu halafu maajabu naweza nikakosa usingizi hadi saa ssita ndio nikalala na ninaamka saa kumi na mbili na nusu nikiingia darasan saa 2 ikifika na nusu au saa tatu nasinziaa sijawahi kutumia dawa ya usingizi wala ya wasiwasi wala ya kupunguza wasiwasi chakula changu kikuu ni wali nyama maharage ndizi sio sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…