"Uroto wa kuku ulivyotaka kunitoa meno

"Uroto wa kuku ulivyotaka kunitoa meno

Zero IQ

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
13,959
Reaction score
24,935
Leo nakumbuka ile way back nikiwa chalii yaani bado mdogo wakati huo nikiwa napata kila kitu kutoka kwa wazazi kuanzia kula, mavazi mpaka lala yangu ilikuwa juu yao mi nikiwa kama boss mtoto nisiejua chochote zaidi ni kutumia tu,

Sasa kuna siku bi mdashi alipika kuku haikuwa siku ya sherehe kama ilivyozoeleka kwa wakati ule kwamba kula kuku mpaka sherehe au mgeni toka mjini aje kuwatembelea,

Kama kawaida hiyo siku ilianza vyema tu kwa mama kachukua mpunga na kuanikia, ilivyofika jioni jioni nikaanua ule mpunga nikasogeza kino na kutwanga ili tupate mchele wa kupika siku hiyo(wakati huo hakukuwa na mashine za kukoboa),

Basi ilivyofikia muda wa kupika mama akaingia jikoni akakamata na kuku mmoja kibandani kwa sababu ya kitoweo,

ilivyofika muda wa kula mtoto wa kiume kwa kazi niliyofanya ya kutwanga mpunga nikapewa paja la kuku kubwa kubwa hivi sasa baada ya kumaliza zile nyama nikawa nanga'ngana na ile supu supu ya ndani ya mfupa waswahili wanaita UBOHO,

Nilikatazwa mara ya kwanza na mzee nikawa nanga'ngana, mara ya pili ya tatu ilivyofika si mfupa ukaitika kupasuka meno yaligongana nikajing'ata ulimi nusu nusu nitoe na meno,

Ule UBOHO wa kuku sikuufaidi tena zaidi ya kuugulia maumivu.

Key.
UBOHO=Bone Marrow=Uroto
 
Back
Top Bottom