Umekosea spelling hapo kwenye figures au macho yangu?
Hii inanikumbusha mwaka 2010 nilipochaguliwa na TCU nikasomee Medicine (Udaktari) chuo cha IMTU -International Medical & Technological University kipo kule Mbezi Beach. Nikajua ndoto zangu zimetimia.
Nafika naambiwa tuition fees ni USD 4,500 hafu kwa muda huo exchange rate ikiwa 1USD=1,500Tsh. Kwahiyo ada tu kama Mill. 6.75Tsh kwa mwaka. Hafu yale mazagazaga ya direct cost jumla kama Mill. 1.2Tsh hivi.
Nikajipa moyo mbona HESLB wananipa mkopo 100%.
Kuja ulizia zaidi bodi, nikaambiwa 100% yao ina limitation. Maximum ni Mill. 2.6Tsh, endapo tuition fees ya mtu ikizidi hiyo itabidi yeye mwanafunzi aongezee.
Sikua na jinsi zaidi ya kwenda TCU kupiga magoti wanibadirishie course. Na hii ndio inanifanya niangaike hadi sasa, maana walinipangia course ambayo ata katika list ya course ninavyo apply haikuwepo.
Hii nchi ukiwa na ndoto, endelea kulala tu. Kamwe haziji kutimia.
Sasa mtoto wa mkulima kweli hapa si tunadanganyana?
Ila trust me, watu Watanzania kibao wanasoma hapo.
Hivi vyuo vya Tanzania wanaojifanya wanalipisha ada kwa USD wahuni sana. Kwa uchumi huu, ada kila mwaka utaona inaongezeka maana thamani ya pesa yetu inazidi kushuka kila jua likitua.