Urusi imekuwa nchi ya kwanza kutambua serikali ya Taliban ya Afghanistan

Urusi imekuwa nchi ya kwanza kutambua serikali ya Taliban ya Afghanistan

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
838
Urusi imekuwa nchi ya kwanza kuutambua rasmi utawala wa Taliban, huku Waziri wa Mambo ya Nje wa Afghanistan Amir Khan Muttaqi akiuita uamuzi wa "ujasiri".

Alikutana na balozi wa Urusi nchini Afghanistan, Dmitry Zhirnov, mjini Kabul siku ya Alhamisi, ambapo Bw Zhirnov aliwasilisha rasmi uamuzi wa serikali yake wa kuitambua Imarati ya Kiislamu ya Afghanistan.

Muttaqi alisema ni "awamu mpya ya mahusiano chanya, kuheshimiana, na ushirikiano wenye tija", na kwamba mabadiliko yatatumika kama "mfano" kwa nchi zingine.Taliban wametaka kutambuliwa kimataifa tangu waliporejea madarakani Agosti 2021, licha ya ripoti za kuongezeka kwa ukiukwaji wa haki za binadamu.

"Tunaamini kwamba kitendo cha kutambuliwa rasmi kwa serikali ya Imarati ya Kiislamu ya Afghanistan kitatoa msukumo katika maendeleo ya ushirikiano wenye tija baina ya nchi zetu," wizara ya mambo ya nje ya Urusi ilisema katika taarifa yake.

Ilisema Urusi iliona uwezekano wa ushirikiano wa "kibiashara na kiuchumi" katika "nishati, usafiri, kilimo na miundombinu", na kwamba itaendelea kusaidia Kabul kupambana dhidi ya vitisho vya ugaidi na biashara ya madawa ya kulevya.

Urusi ilikuwa moja ya nchi chache sana ambazo hazikufunga ubalozi wao nchini Afghanistan mnamo 2021, na ilisema kwenye mtandao wa Telegraph kwamba "kupanua mazungumzo na Kabul" ni muhimu katika suala la usalama wa kikanda na maendeleo ya kiuchumi.

Nchi hiyo pia ilikuwa ya kwanza kusaini mkataba wa kimataifa wa kiuchumi na Taliban mwaka 2022, ambapo walikubali kusambaza mafuta, gesi na ngano kwa Afghanistan.
 
Back
Top Bottom