Urusi imeonesha Afrika ndiyo msingi wa dunia kwa sasa

Urusi imeonesha Afrika ndiyo msingi wa dunia kwa sasa

Joined
May 27, 2022
Posts
11
Reaction score
58
RUSSIA IMEONESHA AFRICA NDIYO MSINGI WA DUNIA KWA SASA

Mafahali wawili wanaposhindana wanyonge hupita salama

ndugu zangu utaona Rais Putin kwa sasa ameikumbatia sana Africa kama moja ya msingi mkuu wa uchumi wa Russia hii ni kudhihirisha kuwa Africa ni dude kubwa lililolala lililotumi na wazungu na Russia analijua hilo ndo maana ameamua kuja mzima mzima (Mungu ambariki) kwani yeye historia inaonesha ni rafiki mwaminifu na siyo mbinafsi kama manyangau ya magharibi na Uchina.

kiukwel unapoongelea ukombozi wa uhuru wa Bara la Africa huwez kuitenga Russia and all of this alifanya buree bila kutanguliza maslai yake ya kiuchumi mbele, kama kuna kaka nje ya Africa ambaye twapaswa kumwangalia na kumshika kwa ajili ya utumwa wa fikra ambao Hawa Manyangau wanataka kutuingiza basi huyo kaka lazma awe Russia ya Putin.

Sasa ni wakati wa Africa kutambua nafasi yake katika Dunia, ni wakati wa viongozi wengi wa Africa kuwaza kumiliki silaha nyingi za Nuclear na uwezo wa kijeshi kwani bila majeshi imara ni ngumu kumiliki uchumi katikati ya unyonywaji wa manyangau, na najua hili la kumiliki silaha za maangamizi litatokea muda siyo mrefuu miongoni mwa nchi za Africa hasa kwa kuwa Rais putin ameamua kuachia mbawa zake juu ya Africa na kuwakinga Mashoga kwa makucha yake.
 
Nyie hamjui Russia vizuri ni watu wanaojali maslahi yao tuu hamna kingine hana msaada wowote walikuwepo hapo kanda ya ziwa kama trainers wa kijeshi waliishia wapi? Kwanini waliondoka?
Unaonekana Bado kinda alafu kibaya zaidi umenyimwa hata kusoma historia ya afrika

Sent from my RMX2189 using JamiiForums mobile app
 
Putin hana pa kushika...mchina haeleweki, mkorea anajipanga mwenyewe, muhindi naye ki asili hataki vita vita.

Kete iliyobakia ni Africa..anajipenyeza penyeza walau aungwe mkono.

Ila hajui kwamba Africa ina mikataba mirefu ya ushirikiano wa kimaendeleo ya watu wa magharibi pamoja na US.

Kazi anayo.
 
Ila urusi ni tajiri Sana Yani pamoja na kuendesha vita, kuwekewa vikwazo Bado katusamehe madeni dah.!
Mkuu mwabie tajiri Putin atujengee matundu ya vyoo shule za msingi zote, madarasa na mabweni katika shule zote za kata afu atufutie madeni yetu yote ndo aje tumfuate
 
Putin hana pa kushika...mchina haeleweki, mkorea anajipanga mwenyewe, muhindi naye ki asili hataki vita vita.

Kete iliyobakia ni Africa..anajipenyeza penyeza walau aungwe mkono.

Ila hajui kwamba Africa ina mikataba mirefu ya ushirikiano wa kimaendeleo ya watu wa magharibi pamoja na US.

Kazi anayo.
Laaaaaa!!!!
 
Haya yatawezekana tukiacha kuchagua viongozi walafi na was*ng* was*ng* kama hawa tulio nao kwasasa ambao wanaendekeza mambo ya kitoto katika serikali.

Vyama vya siasa vyenye wizi mwingi kazi kutuchagulia viongozi ambao umri umeenda wanakuja na akili za mwaka 60 hapa wakati huu.

Tazama kama Nigeria, mtu wanapitisha zee lina miaka 70+ ili awafanyie nini sasa?!

Wakati kuna vijana damu changa na wana spirit nzuri tu ya uongozi na mageuzi.

Hebu tubadilike ni muda wetu sasa wa sisi kuwa na meza ya maamuzi kwenye ramani ya dunia sio kila siku kuamriwa na kutii maagizo ya kifalafala tu.
 
Putin ameifanyia nini Africa??
Africa imefaidikaje na uhusiano wa Russia au kukumbatiwa na Putin kama ulivyosema?
Siasa nyingi za uhuru Russia alitoa sapoti maana ndie hasimu nambari moja wa mataifa ya magharibi rejea history mataifa mengi ya africa kuwa na sera za ujamaa. Tazama hata china na kwingineko.

Russia hajawahi kuchukuwa watumwa wala kuwa na koloni afrika.

Unaona JWTZ na uwezo wao wa kijeshi, 100% ni mafunzo kutoka kwa trainers wa urusi.

Unapozungumzia uhuru ile miaka ya 1960's yaani miaka ya sitini russia alifanya ushirika mkubwa sana nyuma ya pazia kuzisaidia inchi na mataifa mbali mbali kusimama na kujitegemea.

Ukitazama mataifa ya magharibi yaani US na wenzake, wamekuwa na history ya kulinyonya, kulifilisi, kulilaghai kwa siasa uchwara, kulihujumu na kulipoteza bara la afrika na wengineo ili wao wafaidike sisi tukianguka.

Mataifa ya magharibi yametoa mikopo kwa wingi sana kwa mataifa changa ikiwamo afrika na kushawishi mabadiliko ya mifumo ya uendeshaji wa inchi na serikali ambayo haitakuwa na faida kwa siku za baadae na hivyo kuziacha hizi inchi zikiwa tegemezi wa misaada ya mikopo na kutoweza kumudu gharama za uendeshaji wa serikali.

US hapendi mataifa mengine kujitegemea na ndio maana popote anapoona kuna taifa linaanza maamkizi ya kunyanyuka yeye huja na fitina na kuharibu haraka sana ili mipango ifeli tazama Libya, iraq, Syria na kwengineko.

Kwasasa US anapiga sana vita China kuendelea maana hataki kuona taifa lingine likipaa na kuwa imara at the same time hapendi kuona mataifa mengine yakishirikiana kujikwamua kiuchumi kwenda juu.
 
Haya yatawezekana tukiacha kuchagua viongozi walafi na was*ng* was*ng* kama hawa tulio nao kwasasa ambao wanaendekeza mambo ya kitoto katika serikali...
Damu changa,,,,nisaidie watatu tu ni akina nani ao?

Isije kuwa Babu tale,wema sepetu,Steve Nyerere,[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Andika mifano husika badala ya kuandika mambo jumla jumla tu, hayo yote uliyosema naweza kusema hivyo kwa Marekani pia.
Siasa nyingi za uhuru Russia alitoa sapoti maana ndie hasimu nambari moja wa mataifa ya magharibi rejea history mataifa mengi ya africa kuwa na sera za ujamaa. Tazama hata china na kwingineko...
 
Back
Top Bottom