Urusi imepuuza tangazo la Trump la kupeleka manowari karibu na Urusi

Urusi imepuuza tangazo la Trump la kupeleka manowari karibu na Urusi

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
838
Je, hii inaweza kuwa mara ya kwanza katika historia kurushiana maneno kwenye mitandao ya kijamii kusababisha ongezeko la matumizi ya nyuklia?

Rais Donald Trump, aliyekerwa na kauli za Rais wa zamani wa Urusi Dmitry Medvedev, anasema ameamuru manowari mbili za nyuklia kusogea karibu na Urusi.

Kwa hivyo, Moscow itajibuje? Je! tuko kwenye njia ya mzozo wa nyuklia kati ya Marekani na Urusi?
Vyombo vya habari vya Urusi vimepuuza tangazo la Trump.

Akizungumza na gazeti la Moskovsky Komsomolets, mchambuzi wa masuala ya kijeshi alihitimisha kuwa Trump alizungumza "akiwa na hasira". Luteni jenerali mstaafu aliiambia Kommersant kwamba mazungumzo ya rais wa Marekani kuhusu manowari yalikuwa "makelele yasiyo na maana". "Nina hakika Trump hakutoa maagizo yoyote [kuhusu manowari]," mtaalam wa usalama wa Urusi alisema.

Kommersant pia anataja kwamba mnamo 2017, Trump alisema kwamba alituma manowari mbili za nyuklia kwenye peninsula ya Korea kama onyo kwa Korea Kaskazini.

Hata hivyo muda si mrefu, Trump alifanya mkutano na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un. Kwa hivyo, cha ajabu, je, kupelekwa kwa manowari ya hivi punde zaidi ya Donald Trump kunaweza kuwa utangulizi wa mkutano wa kilele wa Marekani na Urusi?
 
Trump wala Putin hakuna mwenye jeuri ya kutumia silaha za nyuklia! Unapozungumza Bomu LA nyuklia LA kisasa, unazungumzia Bomu lenye uwezo wa kuangamiza dunia wala si nchi moja!! Hiyo in CHAIN REACTION! Once started it will continue up to when ALL ATOMS contained in that particular bomb have disintegrated!! Hebu fikirià tani moja tu ya ENRICHED URANIUM!! INA matrilioni ya atoms yasiyohesabika!! Mpaka yote hayo yaishe!! Achana na mabomu yaliyopiga Hiroshima hayo kwa sasa ni kama mwanasesere!!
 
Back
Top Bottom