Urusi imesitisha huduma za kusambaza gesi katika nchi za Bulgaria na Poland, hali ambayo inaonesha mwelekeo wa uhusiano wa Urusi na mataifa ya Ulaya unazidi kudhorota.
Inadaiwa kuwa agizo hilo limetolewa na Rais wa Urusi, Vladimir Putin.
Nchi hizo ni za kwanza Barani Ulaya kusitishiwa usambazaji kutoka Urusi tangu taifa hilo lililoanza kuivamia Ukraine, Februari 24, 2022.
Vita ya Urusi na Ukraine imesababisha vifo zaidi ya 1,000, pia uhusiano unazidi kuwa mbaya kati ya Urusi na wanachama wa NATO.
Source: Daily Mail