Urusi kaonesha mfano mbaya, Venezuela naye anafuata: Dunia inaanza kuharibika

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Urusi imeonyesha mfano kuwa taifa moja linaweza kumega ardhi ya Taifa jingine na kuifanya yake, Venezuela naye sasa anafuata, anataka kumega nusu ya Guiyana ajichukulie. Hii lawlessness itaishia wapi, Je Tanzania nasi tujitwalie Burundi na Rwanda zote kwa vile wakati wa Mjerumani tulikuwa nchi moja?
 
Je Tanzania nasi tujitwalie Burundi na Rwanda zote kwa vile wakati wa Mjerumani tulikuwa nchi moja?
Uvamizi huwa unafanywa kwaajili ya kupora rasilimali za nchi husika.

WATANZANIA TUNA RASILIMALI ZA KUTOSHA, TUIOMBE SERIKALI ITUMIE RASILIMALI ZETU VIZURI NA SIO KUVAMIA NCHI NYENGINE.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Ila Uingereza kuvikalia visiwa vya Falk Island ni sawa?

Ufaransa mpaka Leo kuishikilia Mayotte ni sawa?

Marekani na Hawaii, unataka kusema nini?

Israel na maeneo ya Wapalestina?

China na Tibet, Xinjiang, Macau?

Angola na Jimbo la Kabinda?

Wewe kwa maono yako mafupi unazani yameanza kutokea Jana?

Dunia haipo fair na mwenye nguvu ndio mtawala.
 
pk mwenyewe anatamani walau aichukue karagwe na ngara na huko goma mashariki mwa kongo tz itawezaje kuitwa rwanda na burundi? Kwanza tz haina tamaa ya kujiongezea maeneo kwenye nchi za watu ila wakileta uchokozi wanavamiwa tu na kuzimega hizo nchi.
 
pk mwenyewe anatamani walau aichukue karagwe na ngara na huko goma mashariki mwa kongo tz itawezaje kuitwa rwanda na burundi? Kwanza tz haina tamaa ya kujiongezea maeneo kwenye nchi za watu ila wakileta uchokozi wanavamiwa tu na kuzimega hizo nchi.
Issue kubwa ni hii tabia mbaya kuvamia majirani na kujimegea ardhi zao. Urusi ni nchi yenye ardhi kubwa sana kuliko nchi nyingine yoyote duniani, lakini bado wana tamaa ya kujimegea ardhi kutoka nchi ndogo kama Ukraine. Dunia tunaelekea pabaya!
 
Issue kubwa ni hii tabia mbaya kuvamia majirani na kujimegea ardhi zao. Urusi ni nchi yenye ardhi kubwa sana kuliko nchi nyingine yoyote duniani, lakini bado wana tamaa ya kujimegea ardhi kutoka nchi nndogo kama Ukraine. Dunaina tunaelekea pabaya!
kwa urusi inataka kurudisha nchi zake zote zilizokuwa jamhuri, USSR, labda kama atataka kumega zile nchi ambozo hazikuwa shirikisho lake.
 
Vipi mazayuni?
 
Haya ndio majibu ya thread, mjadala umeisha.
 
Greenland na Canada
 
Ufaransa gani anayeishikilia Mayotte? Mayotte walipiga kura ya kujiondoa Commoro, wakajiondoa Afrika na kujiunga Ufaransa.
Misrae na Palestina mbona hamuongelei maeneo ambayo Israel alimpatia Palestina?
Ile Gaza ilikua ya Misri, Israel akaiteka kutoka Misri. Baadaye waliposaini makubaliano ya amani, kati ya Israel na Misri, Israel akaamua kumrudishia Misri maeneo ya Mlima Sinai (ingawa siyo ya Misri yoteyote) na Gaza akawapatia Wapalestina
 
Burundi ni ya kujichotea tu kwanza warundi wenyewe wanapenda kuwa watanzania na watapata ulinzi madhubuti na chokochoko za Rwanda.
Halafu tunaibadilisha jini unakuwa Tanganyika Bashite anakuwa mkuu wa mkoa.Ndayishimiye anakuwa waziri wa maendeleo ya jamii jinsia, wanawake na watoto.
 
Huo mfano mbaya kwanini iwe Urusi na Venezuela,na sio Uingereza, Ufaransa, Israel, Marekani,ambao wote wapo kwenye ardhi za nchi nyingine kinyume cha sheria?
 
Good 👍 uko vizuri mkuu
 
Tanganyika zanzibar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…