Urusi kaonesha mfano mbaya, Venezuela naye anafuata: Dunia inaanza kuharibika

Urusi kaonesha mfano mbaya, Venezuela naye anafuata: Dunia inaanza kuharibika

Rwanda na Burundi zilikuwa ni sehemu za Tanzania ya leo wakati tukiitwa Deutsch-Ostafrika; je na sisi pia tuzirudishe kwa nguvu eti kwa sababu za kihistoria?

View attachment 2842608
Rwanda na Burundi zilikuwa sehemu ya Tanzania mwaka gani ?

Maana Tanzania haija wahi kuwa Koloni,bali muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.
 
Huo mfano mbaya kwanini iwe Urusi na Venezuela,na sio Uingereza, Ufaransa, Israel, Marekani,ambao wote wapo kwenye ardhi za nchi nyingine kinyume cha sheria?
Mtazamo mfupi huo uliojaa mawazo ya ugombea uhuru wa miaka sitini; Uingereza, Ufaransa na Israel wamevamia nchi gani. Mgawanyo wa ardhi baina ya Israel na Palestina ulifanywa na Umoja wa mataifa mwaka 1947 kufuatia mapendekezo ya United Nations Special Commission on Palestine. Waarabu wengine hawataki kuwapo kwa Tiafa la Israel, na ndiyo maana ya mgogoro huo. Wangetambua tu mipaka hiyo iliyowekwa na umoja wa mataifa kama Tanganyika ilivyotambua mipaka baina yake na nchi za Rwanda na Burundi ambayo iliweka na umoja wa mataifa baada ya vita ya kwanza, kusingekuwapo mgogoro.
 
Ila Uingereza kuvikalia visiwa vya Falk Island ni sawa?

Ufaransa mpaka Leo kuishikilia Mayotte ni sawa?

Marekani na Hawaii, unataka kusema nini?

Israel na maeneo ya Wapalestina?

China na Tibet, Xinjiang, Macau?

Angola na Jimbo la Kabinda?

Wewe kwa maono yako mafupi unazani yameanza kutokea Jana?

Dunia haipo fair na mwenye nguvu ndio mtawala.
Mifano yako mingi ni propaganda tu za wapigania uhuru. Dunia tunayoshi leo siyo ile ya zamani, huwezi kusema kuwa kwa vile mambo fulani yalifanyika mwaka 1884 basi nawe uyafanye leo. Kama mwaka 1884 walikuwa wanaandika barua kwa mikono leo tunaandika kwa computer.

Hawaii ni jimbo halali la Marekani kama ilivyo Texas na Alaska; inawakilishwwa na Congressman mmoja na Maseneta wawili kwenye bunge la marekani, na pia hupiga kura kumchagua rais wa Marekani.

Israel na Palestina waliganywa aradhi na Umaja wa Mataifa, hakukuwa na Taifa la Israel lililovamia Taifa jingine la Palestina kwani wakati huo eneo hilo lilikuwa ni koloni la Uingereza. Ni mwaka huo 1948 ndipo mataifa ya Isarel na Paletsina yalipoundwa.

Mayote lilikuwa koloni la Ufaransa tangua miaka 1884 na wala wananchi wenyewe hawajawahi kudai uhuru; hawakuvamiwa leo.

Visiwa vya Falklands vilikuwa tupu kabisa wakati Uingereza inavichukua mwaka 1765. Argentina ilividai kwa vile tu vikoi jirani yake lakini visiwa hivyo havikuwa kukaliwa na watu wa aina yoyote ispokuwa waingereza tundio walianzisha maskani pale. Ujirani hauhalalishi kujichukulia.

Angola pamoja na jimbo lake la Cabinda lilikuwa koloni la wareno kwa kufuata mipaka ya mwaka 1884; walipopata Uhuru walipata kama nchi moja.

China na Tibet ni tatizo kama hilo la Urusi; Tibet lilikuwa Taifa lenye serikali yake China ikaivamaia, na mpaka leo hawelewani pale Tibet.
 
Ila Uingereza kuvikalia visiwa vya Falk Island ni sawa?

Ufaransa mpaka Leo kuishikilia Mayotte ni sawa?

Marekani na Hawaii, unataka kusema nini?

Israel na maeneo ya Wapalestina?

China na Tibet, Xinjiang, Macau?

Angola na Jimbo la Kabinda?

Wewe kwa maono yako mafupi unazani yameanza kutokea Jana?

Dunia haipo fair na mwenye nguvu ndio mtawala.
No.
Kuheshimu mipaka ni jambo la muhimu sana kwa karne hii na zama hizi za sasa. Aidha, Sheria za kimataifa kuhusu mipaka ya kimataifa inafaa sana kuheshimiwa ili kulinda amani na pia kulinda usalama na maisha ya watu. Ubabe wa kuvamia nchi za watu wengine au kujimegea ardhi kwa nguvu kutoka kwa mataifa ya jirani siyo kitu kizuri hata kidogo kwa dunia ya sasa iliyostaarabika.
 
Urusi imeonyesha mfano kuwa taifa moja linaweza kumega ardhi ya Taifa jingine na kuifanya yake, Venezuela naye sasa anafuata, anataka kumega nusu ya Guiyana ajichukulie. Hii lawlessness itaishia wapi, Je Tanzania nasi tujitwalie Burundi na Rwanda zote kwa vile wakati wa Mjerumani tulikuwa nchi moja?
sio urusi kaanza izi mambo,omba mafaili mahakamani uone kesi za ardhi!!
 
Mtazamo mfupi huo uliojaa mawazo ya ugombea uhuru wa miaka sitini; Uingereza, Ufaransa na Israel wamevamia nchi gani. Mgawanyo wa ardhi baina ya Israel na Palestina ulifanywa na Umoja wa mataifa mwaka 1947 kufuatia mapendekezo ya United Nations Special Commission on Palestine. Waarabu wengine hawataki kuwapo kwa Tiafa la Israel, na ndiyo maana ya mgogoro huo. Wangetambua tu mipaka hiyo iliyowekwa na umoja wa mataifa kama Tanganyika ilivyotambua mipaka baina yake na nchi za Rwanda na Burundi ambayo iliweka na umoja wa mataifa baada ya vita ya kwanza, kusingekuwapo mgogoro.
Ww ni mpuambavu kwahiyo uharamu huwa unapimwa kutokana na muda ulio tendeka?
Hivi kuna mfano mbaya kama huu anao uonesha Israel sasa hivi wa kupuuza Sheria za kimataifa ambaye yeye mwenyewe alizisaini kuziheshimu?,kuuwa watoto na wanawake, kushambulia shule , kushambulia Hospital, kushambulia kambi za wakimbizi,kuuwa waandishi wa habari,kuuwa wafanyakazi wa UN, kuwavua watu nguo huku ukiwarecod ,kutumia njaa,kiu na magonjwa kama silaha ya kivita, kuwafunga watoto wa miaka mpaka 10 magerezani, kupiga watu risasi kiholela huko west bank,kuwanyanganya watu ardhi zao.

Hivi taifa lenye nguvu zaidi ya mara 10 ya Israel ambao ni china siku likiivamia Taiwan unadhani litahofia nn kuhusu sheria za vita hali ya kuwa sasa hivi wanaona Israel ikizikiuka bila kuwajibishwa?
Hivi Urusi akiamua kutumia nguvu za maangamizi nchini Ukraine dunia itakuwa na nn cha kuiambia?
Au Uturuki ikiamuwa kuwavamia wapiganaji wa kikrudi walioko Syria na kufanya maangamizi makubwa kama ya Israel inayo yafanya dunia itakuwa na ujasiri gani wa kuiwajibisha hali ya kuwa kwa Israel ilitazamwa tu?

Hiyo ndo maana ya mifano mibaya sana maana kwa sasa utayafanya mataifa yaanze kupuuza sheria za kimataifa.
 
Wewe ni stupid na foolish kabisa kwa kuandika upumbavu huu hadharani
 
Urusi imeonyesha mfano kuwa taifa moja linaweza kumega ardhi ya Taifa jingine na kuifanya yake, Venezuela naye sasa anafuata, anataka kumega nusu ya Guiyana ajichukulie. Hii lawlessness itaishia wapi, Je Tanzania nasi tujitwalie Burundi na Rwanda zote kwa vile wakati wa Mjerumani tulikuwa nchi moja?
Hakuanza Urusi alianza baba lao US na wapambe wake. Wamefanya hivyo nchi nyingi tu wakiondoa tawala zilizopo na kuzikalia nchi kimabavu. Sijui ni kitu gani huwa kinawafanya muone US anachofanya ni sawa ila wengine si sawa.
 
Hakuanza Urusi alianza baba lao US na wapbe wake. Wamefanya hivyo nchi nyingi tu wakiondoa tawala zilizopo na kuzikalia nchi kimabavu. Sijui ni kitu gani huwa kinawafanya muone US anachofanya ni sawa ila wengine si sawa.
Tangu UN ianze, Marekani haijawahi kukamata ardhi ya nchi ambayo mipaka yake inatambuliwa na UN ikaibadilisha kwa nguvu ili ardhi ile iwe mali ya US. Uanzishwaji wa UN ilikuwa ni kufanya dunia iwe sehemu ya haki na kuachana na mfumo wa ukoloni wa Berlin Conference
 
Kitu cha kwanza ambacho US ilikifanya baada ya kufanikiwa kuteka baghdad na kuangusha utawala wa sadam ililuwa kushusha bendera ya Iraq na kupandisha bendera ya US huku wakiangusha sanam la Sadam.
Umajua kushusha bendera ya nchi na kupandisha ya nchi nyingine ina maana gani?
Tukio lilikiwa live na walipojishtukia wakakata matangazo.
 
Issue kubwa ni hii tabia mbaya kuvamia majirani na kujimegea ardhi zao. Urusi ni nchi yenye ardhi kubwa sana kuliko nchi nyingine yoyote duniani, lakini bado wana tamaa ya kujimegea ardhi kutoka nchi ndogo kama Ukraine. Dunia tunaelekea pabaya!
Inasikitisha sana, na kuna vichwa panzi wanashangilia huo uharamia wa uporaji.
 
kwa urusi inataka kurudisha nchi zake zote zilizokuwa jamhuri, USSR, labda kama atataka kumega zile nchi ambozo hazikuwa shirikisho lake.
USSR iliundwa na nchi huru na ikafika mahali hizo nchi zikaona umoja huo na Ukomunisti ni umaskini na udikteta tu zikaamua kujiondoa, Urusi haiwezi kuwalazimisha tena kurudia muunganiko mfu.
 
Uvamizi huwa unafanywa kwaajili ya kupora rasilimali za nchi husika.

WATANZANIA TUNA RASILIMALI ZA KUTOSHA, TUIOMBE SERIKALI ITUMIE RASILIMALI ZETU VIZURI NA SIO KUVAMIA NCHI NYENGINE.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
Usa alianza zamani sana

England walipora kisiwa kule Argentina
 
Back
Top Bottom