Urusi: Mahakama yapiga marufuku Facebook na Instagram

Urusi: Mahakama yapiga marufuku Facebook na Instagram

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mahakama mjini Moscow imepiga marufuku shughuli za Instagram na Facebook zinazoonesha "msimamo mkali" nchini Urusi, ripoti zinasema.

"Tunalikubali ombi la upande wa mashtaka la kupiga marufuku shughuli za [Instagram na kampuni mama ya Facebook] ya Meta," Jaji Olga Solopova alisema, kwa mujibu wa shirika la habari la serikali ya Urusi Tass.

Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Urusi imesema kuwa kumekuwa na machapisho makali kwenye mitandao ya kijamii, ikitoa wito wa vurugu dhidi ya raia wa Urusi, ikiwa ni pamoja na wanajeshi wa nchi hiyo walioko nchini Ukraine.

Mapema mwezi huu, waendesha mashtaka walitoa wito wa kufanyika uchunguzi wa jinai dhidi ya Meta.

Upatikanaji wa Facebook na Instagram tayari ulikuwa umezuiliwa nchini humo juu ya kile Moscow ilichokielezea kama kutumika kusambaza "habari za uongo" kuhusu uvamizi wake nchini Ukraine.

Meta imesema itawaruhusu watumiaji wa mitandao yake kupinga uvamizi wa Rais wa Urusi Vladimir Putin na wanajeshi wa Urusi.

Jaji alisema uamuzi wa mahakama hayuhusiani na huduma za mtandao wa WhatsApp, ambayo pia unamilikiwa na Meta.

BBC
 
putin anajua fika sasa a naingia kwenye first wave ya myumbo wa uchumi na ili kuzuia habari za makali ya vikwazo inabidi azuie social media zote.
tulioko nje ya urusi tutakuwa tunatumiwa picha za majenerali wachache wakinywa whisk ili kuaminisha dunia kuwa vikwazo havina Athali.
 
Vikwazo havina athari ukweli usemwe
 
PANDORA/AVATAR
Vikwazo havina athari ukweli usemwe

2929-2.jpg
 
Back
Top Bottom