Urusi: Makuruta wapya kusajiliwa kuongeza nguvu jeshini

Adolph Jr

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2016
Posts
5,950
Reaction score
9,511
Urusi yatoa wito makuruta(Recruits) wapya kusajiliwa kuongeza nguvu katika jeshi

Makumi ya maelfu ya wanajeshi wa Urusi wameuawa au kujeruhiwa tangu kuanza kwa vita, wanasema maafisa wa Magharibi

Mji wa Volosovo, karibu na St Petersburg, unashamiri.

Sio uchumi ni vipaza sauti.

Kama miji mingi nchini Urusi, Volosovo imeviweka kwenye nguzo ndefu ambazo ziko kwenye barabara kuu.

Kitamaduni hutumika kwa kucheza muziki wa kizalendo wakati wa sikukuu za kitaifa.

Ingawa, sasa hivi vinatumika kwa kusudi tofauti.

‘’Vikosi viwili vya kujitolea vinaundwa. Tunawaalika wanaume kutoka umri wa miaka 18 hadi 60 kujiunga,’’ wasemaji walipaza sauti.

Ni ujumbe unaorudiwa juu na chini katika nchi hii kubwa.

Katika mitandao ya kijamii, kwenye TV na kwenye mabango, wanaume wanahimizwa kutia saini mikataba ya muda mfupi na wanajeshi ili kupigana nchini Ukraine.

Kwa kukabiliwa na hasara kubwa katika vita vya Ukraine, mamlaka imezindua shughuli ya kuajiri makurutu wapya katika jeshi la Urusi.

Ninamsimamisha mtu mmoja barabarani huko Volosovo na kumuuliza kama anaunga mkono mwito wa watu wanaojitolea kujiunga na jeshi.

‘’Ndiyo! Ningekuwa mdogo ningeenda, lakini sasa ni mzee sana,’’ ananiambia huku akikunja ngumi.

‘’Tunapaswa kuwapiga kwa mabomu!’’

Lakini watu wengi katika mji wanaonekana kuwa na shauku kidogo.

[Vita] ni chungu sana hata kuzungumzia,’’ mwanamke mmoja analalamika.

‘’Kuwaua ndugu zako ni makosa.’’

Ninamuuliza angesema nini ikiwa mmoja wa jamaa yake angetaka kujiunga.

‘’Kwa nini uende? Miili yao pekee ndiyo itarudishwa nyumbani.’’

Na miili mingi iko.

Video za vijana kujisajili kama makurutu wapya zinawahimiza kujiunga na jeshi la Urusi

Urusi haitoi idadi, lakini maafisa wa Magharibi wanasema kati ya wanajeshi 70,000 na 80,000 wa Urusi wameuawa au kujeruhiwa tangu ilipoanzisha uvamizi wake nchini Ukraine miezi sita iliyopita.

Ili kuvutia waajiriwa wapya, mamlaka inawapa waliojitolea kiasi kikubwa cha fedha, mashamba na hata malipo kwa watoto wao katika shule za Kirusi.

Wanaosajili wamekuwa wakitembelea magereza ya Urusi ili kuwasajili wafungwa, wakiwaahidi uhuru na pesa.

Mwandishi wa habari za uchunguzi Roman Dobrokhotov anasema harakati za kusajili makurutu ni ishara ya kukata tamaa kwa upande wa mamlaka: ‘’Hii sio aina ya askari wanaohitajika kwa vita vya ushindi. Kremlin bado ina matumaini kwamba wingi unaweza kushinda ubora. Kwamba wanaweza kupata mamia ya maelfu ya watu waliokata tamaa na madeni yao na kuwatumbukiza tu katika eneo la migogoro.’’

Licha ya kiasi kikubwa cha fedha kinachotolewa kwa wanaojisajili - hadi £4,700 ($5,700) kwa mwezi katika baadhi ya matukio - Roman anasema ukweli ni tofauti.

‘’Kwa kweli watu hawaoni pesa hizi,’’ anasema.

Sasa wanarudi [kutoka Ukraine] na kutuambia waandishi wa habari jinsi walivyodanganywa. Hili pia linaathiri hali, ukosefu huu wa imani kwa serikali yetu, kwa hivyo sidhani kama mkakati huu utafanikiwa.’’

Lakini wengine wanafurahi kujiunga.

Mwana wa Nina Chubarina Yevgeny aliondoka kijijini kwao katika mkoa wa kaskazini wa Karelia kujiunga na kikosi cha kujitolea.

Nina anasema mwanawe, ambaye hakuwa na uzoefu wa kijeshi, alipewa bunduki na kutumwa moja kwa moja nchini Ukraine.

Aliuawa siku chache baadaye.

Alikuwa na umri wa miaka 24.

Nina Chubarina anasema alijaribu kumzuia mwanawe kwenda kupigana nchini Ukraine

Nina anakubali kukutana nami katika bustani karibu na Moscow, ambako amepata kazi ya muda katika kiwanda cha mkate.

Anasema kazi chungu nzima anakofanya kazi zinamfanya asahau kumpoteza mwanawe.

Anakumbuka akimsihi mwanawe asiende Ukraine.

‘’Nilijaribu kuzungumza naye asiende. Nililia. Nikasema, Kuna vita, utauawa! Akaniambia, Mama, kila kitu kitakuwa sawa.’’

Nina anakosoa jinsi mamlaka inavyoajiri watu wa kujitolea kupigana nchini Ukraine.

‘’Wanawatuma tu kama kuku wadogo wasio na lakufanya! Hawangeweza hata kushikilia bunduki hapo awali. Majenerali wanafikiri, Tuna mtu wa kujitolea: vizuri, wewe nenda!’’

Sio kila mtu anafaa! ikiwa nia ni kujiandikisha kama mpiganaji kama ilivyokuwa kwa Yevgeny.

Yevgeny Chubarin aliuawa ndani ya siku chache baada ya kujiunga na jeshi la Urusi kwenda kupigana huko Ukraine.

Idadi ya magari kwenye barabara za Urusi yanaonyesha alama ya ‘’Z’’ inayounga mkono vita bado ni machache.

Wataalamu wanasema kwamba idadi ya watu wanaojitolea kujiunga ni jeshi kwa ajili ya kwenda kupigana Ukraine ni ndogo.

Mchambuzi wa masuala ya kijeshi Pavel Luzin anasema watu hapa hawako tayari kujitolea kwa ajili ya rais wao.

‘’Tatizo la Kremlin ni kwamba watu wengi wa Urusi hawatakufa kwa ajili ya Putin au kwa ajili ya kurejesha Dola kubwa.

Kusajili wanaojitolea haiwezekani katika hali ya sasa kwa sababu hakuna makubaliano ya kiraia nchini Urusi katika vita ‘’ikilinganishwa na Ukraine.Raia wa Ukraine wako tayari kupigana.

Chanzo: BBC
 
Natamani sana ungebold hapo mwandishi aliposema huwez kutegemea kushinda hii vita kwa kuajiri askari wa kujitolea.

Huwa tunasema kila siku humu ndani, hakuna uelekeo kwa Russia kushinda hii vita.
 
Urusi atangaze vita kamili ili wanajeshi wasikatae pelekwa vitani
 
Bado hatuwaamini watu wa magharibi pale wanaposema Russia amepoteza si chini ya askari 80,000?
Huamini nini sasa?wanajeshi
Hawa wa Urusi 45,550 ndio waliouwawa ukichanganya majeruhi hiyo idadi ya 80K inatimia🤔
FB_IMG_1661326905713.jpg
 
Natamani sana ungebold hapo mwandishi aliposema huwez kutegemea kushinda hii vita kwa kuajiri askari wa kujitolea.

Huwa tunasema kila siku humu ndani, hakuna uelekeo kwa Russia kushinda hii vita.
Ni kweli kabisa hawawezi kushinda lakini anayelalaika kila siku ni Urusi au Ukraine,na kama hao Urusi hawawezi kushinda mbona nyie hamushindi??
 
kwa cortation hii umeshafeli . 80,000 ndiyo waitishe jeshi la akiba

Hiyo aitoshi Sasa Putin amesema kila mwana kaya ANATAKIWA aazae watoto si chini ya kumi na watalipwa na kusomeshewa watoto zao Bure Ndio kauli mbiu Ivi sasa
Kashachanganyikiwa bwana Putin. Mtu mpaka afikishe watoto 10 ni uwekezaji wa miaka 20/25
 
Urusi haitoi idadi, lakini maafisa wa Magharibi wanasema kati ya wanajeshi 70,000 na 80,000 wa Urusi wameuawa au kujeruhiwa tangu ilipoanzisha uvamizi wake nchini Ukraine miezi sita iliyopita.

kwa cortation hii umeshafeli . 80,000 ndiyo waitishe jeshi la akiba
Lakini ndiyo hali halisi labda kuna wanajeshi wengine wametunzwa kusubir vita halisi itangazwe....
 
Natamani sana ungebold hapo mwandishi aliposema huwez kutegemea kushinda hii vita kwa kuajiri askari wa kujitolea.

Huwa tunasema kila siku humu ndani, hakuna uelekeo kwa Russia kushinda hii vita.
Ukraine wanajeshi anatoa wapi?
 
Back
Top Bottom