Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Mahakama ya mji mkuu wa Moscow nchini Urusi, imeitoza Twitter faini ya fedha ruble milioni 3.2 kwa ukiukaji wa kiutawala.
Kesi iliyowasilishwa na Idara ya Teknolojia ya Habari ya Serikali ya Urusi na Mamlaka ya Usimamizi wa Mawasiliano ya Umma (Roskomnadzor) dhidi ya Twitter ilisikilizwa katika Mahakama ya Taganskiy mjini Moscow.
Mahakama iliamua kuwa kampuni ya Twitter haikutii sheria kwa sababu ya kupatikana kwa machapisho yaliyopigwa marufuku nchini Urusi kwenye jukwaa hilo la mtandao wa kijamii, na kusababishwa kutozwa faini ya fedha ruble milioni 3.2 (takriban dola elfu 42).
Pamoja na uamuzi huo, idara ya Roskomnadzor ilipunguza kasi ya Twitter kwa asilimia 50 kwenye vifaa vya rununu kwa madai kuwa maudhui ya kujitoa uhai, yenye uchafu na utangazaji wa dawa za kulevya hayakuondolewa kwenye mtandao huo wa kijamii.
TRT