Strong ladg
Senior Member
- Jul 15, 2021
- 170
- 445
Urusi imechukua udhibiti wa mgodi wa Lithium wa Shevchenko baada ya kutwaa eneo unapopatikana mgodi huo. Hii ni mwendelezo wa Urusi kutwaa maeneo yaliyoko mashariki mwa Ukraine tangu kuanza kwa vita kati ya Urusi na Ukraine.
Mgodi huu ni miongoni mwa migodi migodi mikubwa zaidi ya Lithium barani Ulaya hivyo kitendo cha Urusi kuchukua udhibiti wake si habari njema kwa maadui wa Urusi.
Taarifa iliyotolewa na chombo cha habari cha Urusi (RT) kupitia mtandao wa Telegram mnamo tarehe 11 Januari 2025,ilitumia lugha ya kejeli kuwa " walafi " wamekosa udhibiti wa mgodi mkubwa zaidi wa Lithium barani Ulaya.
Madini ya Lithium ni muhimu hasa kwa sasa kutokana na matumizi yake katika kutengeneza betri zinazotumiwa na magari ya umeme.
Pia itakumbukwa katika mojawapo ya Interviews zilizofanywa na Lindsay Graham ambaye ni seneta wa Marekani anaetokea South Carolina, alisema " Ukraine inakalia raslimali zenye thamani ya matrilioni hivyo hatuwezi kuacha Urusi azichukue Ili akatumie pamoja na China".
SOURCE : RT