EINSTEIN112
JF-Expert Member
- Oct 26, 2018
- 21,711
- 35,644
Wizara ya Ulinzi ya Urusi siku ya Jumatano imetangaza uharibifu uliofanywa na wanajeshi wa Urusi wa makombora mawili ya HIMARS MLRS ya Marekani huko Donbass.
Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Urusi Luteni-Jenerali Igor Konashenkov alisema makombora hayo yaliyotengenezwa na Marekani ya HIMARS na maghala mawili ya risasi yaliharibiwa na ‘’makombora yenye usahihi wa hali ya juu’’ ya Urusi karibu na kijiji cha Malotaranovka katika Jamhuri ya Watu wa Donetsk kama ilivyojiita.
Hata hivyo, mshauri wa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ukraine, Anton Gerashchenko, anakataa taarifa za jeshi la Urusi kuhusu madai ya uharibifu wa makombora ya HIMARS yaliyopelekwa Ukraine kutoka Marekani.
Data ya jeshi la Urusi pia imekataliwa na mbunge wa Ukraine, ambaye pia ni mwanachama wa kundi la Umoja wa Ulaya Oleksiy Goncharenko.