Urusi yatangaza usitishaji mapigano Ukraine ili raia watoke

Urusi yatangaza usitishaji mapigano Ukraine ili raia watoke

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
1646731535796.png

Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa, Vassily Nebenzia, amesema nchi yake itasitisha mapigano kuanzia saa nne asubuhi ya leo kwa majira ya Moscow na kufunguwa njia salama kuwahamisha raia kutoka miji ya Kiev, Cher-nigov, Sumy na Mariupol. Kwa mujibu wa Nebenzia, pendekezo hilo halina masharti yoyote kwa raia wanaopitia Urusi.

Rais Volodymyr Zelenskiy amesema badala ya kutangaza makubaliano ya kuwepo kwa njia salama, Urusi inaongeza vifaru, makombora na mabomu. Wote wawili wamezungumza baada ya duru ya tatu ya mazungumzo kati ya Ukraine na Urusi iliyomalizika jioni ya jana. Pande zote mbili zimetangaza kupigwa kwa hatua kwenye mazungumzo hayo.

Hata hivyo, Rais Zelensky amelikataa pendekezo la kuwapitishia raia wa nchi yake kwenye kile alichokiita "ardhi ya mvamizi." Akizungumza akiwa ofisini mwake mjini Kiev, Zelensky ameapa kuendelea kusalia ndani ya nchi kuongoza mapambano.

DW Swahili
 
Kule Zelensky anajimwambafai kaua jenerali wa urusi, kipind hiki Cha cease fire

Sasa Ngoja wafatiliaji tukae mkao wa kula tuone jinsi gani ukrane inakwenda kugeuka HISTORICAL SITE kwa magofu yanayoenda kutengenezwa.[emoji4]

Uyu Zelensky anakwenda kuifanya ukraine yake igeuke mavumbi kwa upumbavu wake mwnyw wa kutaka cheap populality Kwny media.
 
Zelensky akikubali hapa tu kesha.

Inabidi akomae na raia wasitoke ili mrusi awe na huruma asiimalize ukraine.

Wakitoka raia aisee inaenda kuwa vita zaidi ya ngumu kwa ukraine.

Putin ni mshenzi sana yaani huruma hana
 
Zelensky akikubali hapa tu kesha.

Inabidi akomae na raia wasitoke ili mrusi awe na huruma asiimalize ukraine.

Wakitoka raia aisee inaenda kuwa vita zaidi ya ngumu kwa ukraine.

Putin ni mshenzi sana yaani huruma hana
Angekuwa mjanja asingekubali raia waondoke maana hapo hakutakuwa tena na haki za binadamu.ni mwendo wa mabomu kwenda mbele
 
Angekuwa kuwa mjanja asingrkubali raia waondoke maana hapo hakutakuwa tena na haki za binadamu.ni mwendo wa mabomu kwenda mbele
Raia wenyewe sidhani kama watakuepo wenye huo moyo,raia watataka watoke kwa namna yoyote ile.

Zelensky azuie raia wasitoke ili vita iishe,ama azidi kuomba radhi na kukubali yaishe huwenda putin atarudisha moyo nyuma.

Putin ni mshenzi sana aisee,zelensky alitakiwa ajishushe tokea mwanzo lakini pia putin ni Mshenzi,so kila mtu amezingua
 
Zelensky akikubali hapa tu kesha.

Inabidi akomae na raia wasitoke ili mrusi awe na huruma asiimalize ukraine.

Wakitoka raia aisee inaenda kuwa vita zaidi ya ngumu kwa ukraine.

Putin ni mshenzi sana yaani huruma hana
Raia wanatoka miji iliyotekwa kwenda maeneo mengine salama nchini kwao. Putin amefeli tena azama ya kuwahamisha Urusi. Ukrainians kwa kweli wanao msimamo.
 
Angekuwa mjanja asingekubali raia waondoke maana hapo hakutakuwa tena na haki za binadamu.ni mwendo wa mabomu kwenda mbele
Mwanzo mlisema anatumia raia kama ngao, sasa karuhusu raia kutoka bado mnaleta maneno, Sasa huo ni ujumbe kwenu kwamba Zelenskiy na jeshi lake haogopi mtu na ndo maana Hadi Sasa anamtoa kamasi Putin na anapuuzia masharti yake uchwara.
 
Na kinachomkwamisha mrusi kumaliza vita hiyo ni hao watu kinyume na hapo tungeongea habari nyingine kabisa.
Visingizio tu, mbona JWTZ walitandika Idd Amin Kagera hadi Kampala na waganda wakiwemo, US alimaliza vita Iraq na wairaq wakiwemo nchini, nk. Shida Russia analipua makombora hovyo hovyo mitaani baada ya kuona kupigana ana kwa ana kwa bunduki na wanajeshi wa Ukraine wamezidiwa na kudhibitiwa kuiteka kyiv.
 
Sahii kabisa,
Alichokifanya khakiev, anataka akirudie na kwingine.

Itakua Ni mvua ya mabomu na hatolaumiwa maana watakaokua wamebakk ni wanajeshi TU[emoji4]
Raia watangaze kutotoka hapo ukraine.

Haiwezekani uwe na huruma na watu lakini usiwe na huruma na makazi ya watu hao.
 
Back
Top Bottom