Urusi yatangaza usitishaji mapigano wakati sikukuu ya Pasaka nchini Ukraine

MBYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2020
Posts
443
Reaction score
594
Raisi Vladimir Putin ws Rasia ametangaza usitishaji mapigano Ukraine kwa siku mbili nchi Ukraine kwa siku mbili kupisha pasaka

Amri hii inakuja masaa machache baada ya Marekani kutishia kujiondoa kama mpatanishi ikiwa Ukraine na urusi hazito onyesha muelekeo wa kuacha uhasama

Chanzo BBC
 
Sasa huu ndiyo unafiki wenyewe.

Kwa hiyo kwa fimra za Putin, Mungu anaruhusu mauaji siku nyingine isipokuwa pasaka tu?

Kama anataka toba, alistahili kusema anasitisha moja kwa moja.
Putin hajielewi na ukristo wake
 
Sasa huu ndiyo unafiki wenyewe.

Kwa hiyo kwa fimra za Putin, Mungu anaruhusu mauaji siku nyingine isipokuwa pasaka tu?

Kama anataka toba, alistahili kusema anasitisha moja kwa moja.
Je kwa wale dhambi za kuachwa siku 30 na baadae mambo yanasonga kama kawaida inakuaje..........hii Dunia kila mtu na formula zake
 
Putin hana nia ya kumaliza hii vita kwa mazungumzo, bado anaamini ushindi wa kijeshi utapatikana.

Trump anajazwa ujinga tu na Kremlin.
 
Putin hana nia ya kumaliza hii vita kwa mazungumzo, bado anaamini ushindi wa kijeshi utapatikana.

Trump anajazwa ujinga tu na Kremlin.
Ni kweli kabisa lkn hata akishinda ataikalia kwa taabu sana Ukraine,hataishi kwa amani kama alivofanya kwa nchi ya Jojia
 
Putin hana nia ya kumaliza hii vita kwa mazungumzo, bado anaamini ushindi wa kijeshi utapatikana.

Trump anajazwa ujinga tu na Kremlin.
Trump anataka apeleke focus yake Israel hii Ukraine anaona haimhusu hii ni vita ya Biden sio yake ndo maana amesema kama jamaa hawatakubaliana kuachana na vita ataendelea na mipango yake mengine huko watajuana wenyewe anaona wanampotezea muda tu wakati yeye ana plan nyingine
 
Labda waendelee kufanya matukio ya kigaidi ila kwa wananchi kote alipochukua na kua chini yake wananchi wanamkubali Mrusi
Ukrain magharibi haimkubali mrusi tofauti na wale mashariki
 
Hata mi naona hivo
 
Ukrain magharibi haimkubali mrusi tofauti na wale mashariki
Na sehemu kubwa aliyochukua mrusi ni mashariki ambapo ndo wapo raia wengi wanaoongea lugha ya urusi na pia ndo maeneo yenye ardhi kubwa ya kilimo na madini ......na kuna dalili zote mrusi anaondoka na hayo maeneo yaliyojitenga
 
Anatamani kuirudisha SSR hivyo hataishia hapo tu akiimaliza Ukraine Pana uwezekano akahamia nchi nyingine iliyokuwa sehemu ya usivieti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…