Ukweli ni kwamba mataifa ya magharibi mwanzo yaliona km Russia anataka kutumia kitisho tu kwa Ukraine,lakini hawakutegeme km ataivamia mazima na ndio maana na wao wakaanza kutia mkwara kwa kufanya mazoezi ya kijeshi na Ukraine ili kumuogopesha Urusi,ila hali ilivyozidi kubadilika na intelligence zao kuona kuna ukweli anaweza kuivamia na wakanza kutafuta namna nyengine ya kumtia moyo jamaa yao Ukraine..hata hivi vikwazo walivyoviweka hawakujipanga vizuri kuona madhara gani yatawakuta kwa upande wao,
Na ndio maana kuna baadhi ya nchi za ulaya wanaona hawana sababu ya kuingizwa kwenye mgogoro wenye madhara kwao,ila kwa sababu ya shinikizo kutoka kwa wakuu na wao wanalazimika kufanya hivyo kwa matakwa ya wakuu wao kwenye muungano huo..
Kuna wachambuzi wa uchumi kutoka mataifa ya ulaya wanakili wazi kwamba hivyo vikwazo walivyoviweka vinawaumiza na wao,kuliko matarajio yao viwaumize waRusi tu.