Urusi yatoa masharti ya kusitisha vita Ukraine

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191


Urusi imesema kuwa inaweza kusitisha operesheni "wakati wowote" ikiwa Ukraine itatimiza masharti ya Urusi. Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema Ukraine lazima itambue Crimea kama Urusi, na Donetsk na Luhansk kama mataifa huru.

Mbali na hayo, Peskov anasema Ukraine lazima irekebishe katiba yake na kukataa madai ya kuingia katika kambi yoyote (kama vile Nato, kwa mfano).

Anaongeza kuwa Urusi itamaliza "kuondoa jeshi" kwa Ukraine, na ikiwa masharti haya yatatimizwa hatua za kijeshi za Urusi "zitakoma mara moja".
Msemaji wa Kremlin amesisitiza kuwa Urusi haitaki kutoa madai yoyote zaidi ya eneo nchini Ukraine.

BBC swahili
 
Hao ndiyo Wanaume wanaofanya dunia izunguke, siyo itawalike na beberu mmoja tu hapatakuwa salama duniani.

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
 
Kwa destruction inayoendelea Ukraine, na kwa masharti hayo, nakubali.......
 
Ya kutokuwa na jeshi ameyaondoa now

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Ngoja nicheke kwa dharau πŸ˜¬πŸ˜¬πŸ˜„πŸ˜„,hayo masharti anaweza kukubali mke wa Putin sio Ukraine..
 
Nilicheka Puti aliposema kuwa anaweza acha kupigana vita endapo tu Ukrain ataacha na kupigana sasa anataka aingie and then Ukraine aweke silaha chini kwa destruction aliyofanya baada kushindwa mbinu za vita nani amsamehe... Puti alipue tu hovyo hovyo ipo siku atachokwa ndipo atajua kuwa hajui.. uzuri ya waikraine hawana mapenzi kabisa na Putin and Russia kwa ujumla.. wao wanamsubiri tu ashambulie mji kwa mbali ila akiingia kwa miguu Russia wanaliwa live
 
Mashart ya kidada sana .i vita ya kijinga tu
Masharti ya Urusi ni ya msingi sana tena ni ya kuungwa mkono na kila mtu mwnye timamu zake. Fikiria Zelensky alivyoua watu wengi waliojaribu kumpinga, fikiria Rais huyo alivyompindua Porochenko na kutesa wafuasi wake, fikiria alivyojipendekeza kwa Marekani na Ulaya na kushiriki kuua Wa Iraq kibao, kuua Wa Libya, n.k. Urusi iendelee kumchapa hadi atoke madarakani Shetani mkubwa huyo.
 
Ngoja kwanza tuwachakaze kidogo vibaraka hawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…