Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Urusi imeto lawama kali kwa Marekani, ikisema kuwa inahusika na mambo yanyoendelea kwa sasa huko Middle East.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, Maria Zakharova, aliita sera yawa Rais Joe Biden huko Middle East kuwa imeshindwa kabisa.
Zakharova alitoa kauli hiyo kupitia ujumbe wa Telegram, akizungumzia mashambulizi ya Iran kufuatia mauaji ya kiongozi wa Hezbollah, Hassan Nasrallah, yaliyofanywa na Israel.
Soma pia: Iran yasema Israel ikijibu, itaitwanga mara 1,000 zaidi
Aliikosoa Ikulu ya Marekani kwa kutokuwa na ufanisi katika kushughulikia hali hiyo ya mivutano.
"Kushindwa kabisa kwa utawala wa Biden katika Mashariki ya Kati. Janga la umwagaji damu linaendelea kuongezeka, na kauli za Ikulu ya Marekani zinaonesha kushindwa kabisa kutatua mizozo. Juhudi za (Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony) Blinken zimepelekea maelfu ya vifo na hali ya kukwama,"
Zakharova aliandika.
Hapo awali, Iran ilifyatua makombora mengi kuelekea Israel, ikidai kuwa mashambulizi hayo yalilenga miundombinu ya kijeshi ya Israel.
Kutokana na mashambulizi hayo, msafara rasmi wa Urusi uliokuwa ukiongozwa na Makamu wa Waziri Mkuu Dmitry Chernyshenko, ulilazimika kusitisha safari yao kwenda Qatar.