US debt is now $37trn – should we be worried? (Deni la Marekani sasa ni $37trn - Je tunapaswa kuwa na wasiwasi)?

US debt is now $37trn – should we be worried? (Deni la Marekani sasa ni $37trn - Je tunapaswa kuwa na wasiwasi)?

Ah! Yaani 'Elfumea' analinganiaha deni lake na "Milionea"? Utani tu 😀
 
Wakope tuu,mbona na sisi Tanzania tunakopa?

Huwa nawashangaa sana wale mbumbumbu wa bongo kulaumu kukopa.
Kweli aisee tukope tu ili ccm na machawa wake akina mwamposa na kuhani musa wakagawane.
 
Marekani ni nchi tofauti na nchi nyingine, inaweza kukopa kadri inavyohitaji na sio lazima ilipe hilo deni ilimradi duniani watu wanayo imani kwa serikali yake tu, tatizo sasa hivi watu wanapoteza imani kwa kasi sana kwa serikali ya Marekani kutokana na kuwa na viongozi wendawazimu kama Trump.
 
Hivi hata umeelewa ninachokiongelea ? Tatizo watu nikisema kuhusu mikopo kwamba USA anadaiwa unadhani nasema na sisi tukope wakati mimi nipo against kabisa na hii mikopo ambayo haina tija



Pili Marekani hadaiwi na Matajiri wa Marekani USA anadaiwa na Dunia ambayo anawalipa kwa kuprint madollar mengine kuwalipa Riba and so on and so forth

Watanzania wengi wamezoea ''kuchukuwa pande'' kwenye mijadala bila kujua undani wa kinachojadiliwa. Hapa wengi watadhani kuwa umefungua thread ili kumtetea Samia na deni la Tanzania (uchawa) japo lengo lako ni tofauti. Hapa ndiyo wanasiasa wetu walipotufikisha. Na si ajabu thread yako ikadakwa juu kwa juu na Ikulu na kuwa kama utetezi wa deni letu kuwa kubwa (badala ya ule utetezi kuwa ni kubwa kwa sababu linatajwa kwa shilingi). Pengine kichwa cha thread kinawafanya watu wapate picha tofauti na lengo lako?
 
Tatizo kubwa kwenye deni la taifa ni jinsi mikopo inavyopatikana na matumizi ya hiyo mikopo. Ukiwa na serikali stable(inayoaminika kwa miaka mingi ijayo),
na uchumi unaokua unakopesheka kirahisi mikopo ya muda mrefu isiyohusisha assets na uhuru wa nchi yako na riba ni ndogo hapo hakuna tatizo. Tatizo la madeni ni inapokuwa kinyume na hivi.
 
Nope printing pesa sio Ghali na ni ghali kiasi gani ingekuwa Ghali watu wasingefoji pesa (Pesa ni just Paper) lakini ni perceived value (kwamba hilo karatasi tuseme ni tshs 10,000/= na mtu akinipa hilo karatasi mimi niweze kumpa maembe ili kesho nikanunue mahindi na maharage)

Mbili dunia ya leo kuprint pesa sio necessarily naweza tu kusema ku-add figures fulani katika mzunguko i.e. electronically (computer) kwa kutoa mikopo kwa Bank A to Bank B au kununua Bonds za Serikali ambayo inaziuza / inakopa....; ukizingatia Banks wanaruhusiwa kukopesha pesa ambazo hawana na ndio mfumo wa Sasa unaoitwa FIAT Currency unavyofanya kazi;
  1. Wewe unakwenda kukopa benki milioni kumi bank hawana hio 10m lakini wanakupa tuseme wanakuwekea kwenye account yako (labda hata kutoka kwenye pesa ya mzunguko ya watu wengine au inakopa Central Bank na Central Bank inazifyatua hizo 10m) wanakwambia kwamba utatupa riba 100,000/=
  2. Wewe unakwenda kuzungusha hio 10m ila benki unawarudishia 10m yao na faida ya laki Moja
  3. Huenda Benki inachukua elfu tisini na elfu kumi nyingine inawapa central bank pamoja na 10m.
Kitendo kilichofanyika hapo ni kutengeneza wealth (kwa wewe kufanya uliyofanya na kuwapa watu mishahara na miradi yako uliyowekeza ambayo imeongeza ajira, hence mzunguko wa pesa wa watu kutumia na wengine kuweza kuweka deposits bank) as well as kuongeza laki moja ambayo ilikuwa haipo kwenye mzunguko au kama Central bank waliprint pesa na sio kwamba zilikuwepo sehemu watakuwa wameongeza 10m kwenye mzunguko...

Sasa anachofanya USA ni kwamba anakopesha watu kwa dollar (bonds) na mikopo hii ni zaidi maradufu ya uzalishaji na makusanyo yake...... (Kinachofanyika Pesa inaprintiwa inapewa Serikali na Serikali inatoa Bonds kwa kuwapa Wanao-print (Treasury) na wanao-print (Treasury) wanauzia Bonds hizo mabenki / watu na mataifa mbalimbali kwa promise ya kupewa riba kila Mwaka...

Watu wakija kudai riba anaprint pesa nyingine nyingi ili kuweza kuwalipa riba na kuwaongezea wanazokopa (Hakuna directly wealthy creation) na watu wanalipwa sio kwa uzalishaji bali kwa kuongeza deni (kuongeza pesa kwenye mzunguko) Nadhani miaka ya hivi karibuni USA itakuwa inalipa 10 trilioni USD kila mwaka kwa ajili ya mikopo na Interest za kuwalipa watu....; Tatizo la hii scenario utaendelea kuwalipa watu riba kwa kuprint zaidi mpaka lini ? Sababu wakianza kushituka na kudai pesa zao kitakachotokea nadhani kitafanya Financial System ya dunia nzima kupata mshituko mkubwa sana (kwahio watu wenye busara wanaona faida ya kupunguza utegemezi mkubwa wa Dollar)
Acha uongo na upotoshaji, ulichoandika hapa ni total rubbish, Marekani haiprinti pesa kiholela kama unavyoaminisha watu hapa, Federal Reserves ni taasisi huru kabisa kutoka serikali kuu ya Marekani, kama uchumi wa Marekani haukui watu wake wasingekuwa na kipato cha kuwafanya soko kuu la bidhaa za ubora wa juu za China na wasingeukuwa exporters namba mbili baada ya China, wasingekuwa na viwango vidogo sana cha unemployment na inflation. Halafu kama US wataanza kulipa 10 trilioni USD kwa mwaka ina maana ndani ya miaka minne tu watakuwa wameweza kumaliza deni lote, hizi ni contradictions tupu.
 
Acha uongo na upotoshaji, ulichoandika hapa ni total rubbish, Marekani haiprinti pesa kiholela kama unavyoaminisha watu hapa,
Aisee kumbe uelewa pia ni kipaji ngoja nikupe simplification ya kijachoendelea :-
  1. USA analeta bajeti yake ambayo ni always maradufu kuliko mapato / makusanyo na anachofanya ni ku issue bonds ambazo treasury anaprint hizo bonds sawa sawa na bajeti ambayo ni maradufu kuliko makusanyo
  2. Bonds hizo zinauzwa kwenye soko (ambapo ni pamoja na dunia nzima kununua kutokana na backing ya USA) kutokana na Imani ya nchi nyingine kwamba USA italipa (na kwa sasa inalipa riba kutokana na ku issue kila mwaka bonds nyingine / plus madeni)
Kama hio sio uholela ni nini (by definition this is not sustainable na itaingiza dunia katika matatizo) refinancing debt by more debt; and we have been here before kwa USA kutapeli ulimwengu wakati wa Gold Standard kwa ku print pesa zaidi ya deposits walizokuwa wakidanganya ulimwengu hadi Nixon akaamua kuiondoa dollar kwenye gold standard (sababu kilichopo kilikuwa kidogo na walichosema)

Pili tunajua kwamba USA wanaweza kwenda extreme, kama walivyonyanganya Gold za watu wote kwa kuzinunua kwa bei waliyotaka ( kufanya confistication ya gold za watu mwaka 1933) na mpaka leo hii inasemekana tu USA ndio ana Gold Deposit kubwa but no body knows for a fact (na kwa mwendo wa uwongo uwongo huu it might all be a ruse / deception)
Federal Reserves ni taasisi huru kabisa kutoka serikali kuu ya Marekani,
Huru au sio Huru hio ni debatable mimi nimekupa facts kinachoendelea uhusiano wa Serikali na Federal Reserve ni kama wewe na printer yako ni kubonyeza tu button unataka kiasi gani; na issue inakuja pale kwamba kila mwaka order inakuja ya kuongeza kiasi fulani kwenye mzunguko ili kukidhi madeni na matumizi ya Serikali
kama uchumi wa Marekani haukui watu wake wasingekuwa na kipato cha kuwafanya soko kuu la bidhaa za ubora wa juu za China na wasingeukuwa exporters namba mbili baada ya China, wasingekuwa na viwango vidogo sana cha unemployment na inflation.
How has this got to do with anything ? Ni kama unaniambia kwamba Desi wangekuwa wezi watu wasingelipwa au ndogo Ponzi asingelipa watu au Bernie Madoff asingelipa watu (FIAT Currency inahitaji Imani ya watu kwamba Pesa hio ni Valuable) tofauti na hapo ni kama Voltaire alivyosema (will return to its intrinsic value which is Zero)
Halafu kama US wataanza kulipa 10 trilioni USD kwa mwaka ina maana ndani ya miaka minne tu watakuwa wameweza kumaliza deni lote, hizi ni contradictions tupu.
Kama wataanza kulipa !!!! Hivi unajua ni mara ya mwisho lini USA wamekuwa na Surplus (2001) kuanza kulipa deni hizo 10 trilioni inabidi kupunguza matumizi na ni marais wangapi (kwenye hii demokrasia ambayo watu wanataka instant results) wana guts za kupunguza matumizi ? Ndio maana Musk alikuja na Dogde yake ya kupunguza Government spending ingawa Trump kama kawaida yake mapunguzo ya UMMA amehamishia kwa washikaji wake katika kupunguza Kodi (hence matokeo yake ni kuongeza deni) na mbaya zaidi ni kwamba Mikopo inakopwa mingine ni kwa ajili ya kulipa madeni

NB: Hio 10 Trilioni kwa mwaka sio kwamba ndio walipe mambo yawe Kosher bali ni Interests na loan Repayments
Kama nilivyoshatoa tahadhari kwa wanaopenda Mikopo....

 
Tatizo kubwa kwenye deni la taifa ni jinsi mikopo inavyopatikana
Na ndio hapo kila siku nasema tusijilinganishe na USA sababu USA anachezesha Desi hivyo mikopo yake ni tofauti sababu ni sisi ndio tunamsaidia kubeba zigo la miiba na hapo nilishasema yafuatayo


na matumizi ya hiyo mikopo.
Naam hata hivyo USA anafanyia nini hio Mikopo ? (Ni kama watu mna Mkoba ya Kikundi na mwenyekiti wenu anafuja hio balance yenu kwa kudhania kwamba mambo yatakuwa sawa na atalipa ila kwa kufuja kwake ni kuweka dunia nzima katika hatari ya crisis any moment; Na je anchofanyia ni nini ngoja nikupe example kidogo:-
  • Reagan aliyesifika kama baba wa Ubepari ila ndio mmoja kati ya marais waliongeza deni kwa kiasi kikubwa; na moja ya program yake ilikuwa ni Strategic Defense Initiative (SDI), proposed U.S. strategic defensive system against potential nuclear attacks—as originally conceived, from the Soviet Union. The SDI was first proposed by President Ronald Reagan in a nationwide television address on March 23, 1983. Because parts of the defensive system that Reagan advocated would be based in space, the proposed system was dubbed “Star Wars,” after the space weaponry of a popular motion picture of the same name. (A White Elephant)
  • Trump na yeye naona anakuja na ya kwake Golden Dome; ila mwisho wa siku ni watu kula tender na pesa za walipa kodi (which would have been none of our business) kama Dollar isingekuwa Global Currency

Ukiwa na serikali stable(inayoaminika kwa miaka mingi ijayo),
na uchumi unaokua unakopesheka kirahisi mikopo ya muda mrefu isiyohusisha assets na uhuru wa nchi yako na riba ni ndogo hapo hakuna tatizo. Tatizo la madeni ni inapokuwa kinyume na hivi.
Kwahio wanaaminika ? Kila mtu anajua hili ni tatizo kubwa sana ni kwamba tu watu wanatafuta mbadala, wanasema fool me one shame on you, fool me twice shame on me..., Nixon ali pull the carpet under peoples feet.., na sasa hivi mambo ni kama yanajirudia. Na kwa USA kufahamu hilo ndio maana kuna wakati wanatumia mabavu mfano kuwalazimisha waarabu kutumia Petrol Dollar a commitment by Saudi Arabia to use dollar revenues from oil sales to the United States to buy US Treasuries
 
Back
Top Bottom