US election 2020: Joe Biden, kinara katika kura za maoni. Trump, hali ni tete!

US election 2020: Joe Biden, kinara katika kura za maoni. Trump, hali ni tete!

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Posts
5,500
Reaction score
8,060
Habari!

Hali si hali kwa rais Donald Trump, wapenzi na wafuasi wa Chama cha Republican kwa ujumla wakati ambapo tukielekea katika Uchaguzi wa Rais panapo mwezi Novemba mwaka huu.

Hii ni kulingana na matokeo ya hivi karibuni ya kura mpya za maoni za kitaifa za jarida la New York Times pamoja na Taasisi ya Utafiti ya Chuo cha Siena ambapo mgombea mteule wa Chama cha Democratic Joe Biden anaongoza kwa alama 14 dhidi ya mpinzani wake Donald Trump.

Trump amejipatia asilimia 36 ya kura huku Biden akiongoza kwa asilimia 50 ya kura za washiriki wote.

Biden amejipatia faida ya uungwaji mkono kutoka katika makundi ya wanawake na jamii za watu wasio weupe huku kukiwa na uwiano sawa wa kura kutoka kwa wapiga kura wa kiume, Wamarekani weupe pamoja na wapiga kura wenye umri wa kati na kuendelea.

Huu ni mwanzo tu kuelekea Uchaguzi wa Novemba na pengine ni kidogo tu ya kile kilichopo mbele. Muda utaweka bayana kile kilichobaki!

-promo-1592949468987-videoSixteenByNineJumbo1600.jpg
 
Uchaguzi wa US hauamuliwi kwa kura zamaoni DT anaweza akaburuzwa hapa at the end akaibuka mshindi

Sina upande ila natamani DT ashinde tena kwakishindo kabisa


Sexer pitia hapa kaka MKUBWA.
His chances of winning are very good, unless,kama Democrats hawatarudia uzembe wa 2016.
I honestly wouldn't be too surprised.
 
Uchaguzi wa US hauamuliwi kwa kura zamaoni DT anaweza akaburuzwa hapa at the end akaibuka mshindi

Sina upande ila natamani DT ashinde tena kwakishindo kabisa


Sexer pitia hapa kaka MKUBWA.
Huna upande wowote na wakati huo huo unatamani Trump ashinde.
 
Back
Top Bottom