Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
US na UK zilikuwa zimeizuia Ukraine kutotumia makombora ya ATACMS ya USA na Storm Shadow ya UK kupiga ndani ya Russia. Juzi kati wakairuhusu na Ukraine ikayatumia kupiga ndani ya Russia. Putin amechafukwa sana baada ya kitendo hicho. Kwanza kasema kuwa hatasita kupiga target za kijeshi za nchi ambazo zinaruhusu makombora yao kupiga ndani ya Russia. Pia amelegeza sheria za matumizi ya silaha za nyuklia akisema kuwa shambulio kutoka nchi isiyo na nyuklia lakini inayosaidiwa na nchi ya nyuklia litahesabiwa kuwa ni shambulio la hao wawili pamoja na Russia itakuwa na haki ya kujilinda kwa silaha za nyuklia.
Pia kaishambulia Ukraine kwa kutumia makombora ya masafa ya kati yenye uwezo wa kubeba silaha za nyuklia na ni ambayo si rahisi kuyaintercept. Kamaliza kwa kusema kuwa wenye mashaka na maamuzi yake wayaondoe, yaani anamaanisha anachosema.
Swali, US na UK wataendelea kuiruhusu Ukraine iendelee kuipiga Russia kwa makombora yao au watafyata baada ya huu mkwara? tutegemee nini iwapo hawatafyata?