USA, mataifa mengi Ulaya na India ni miongoni mwa ambao ndege zao bado haziruhusiwi kuingia Kenya, natumai hawatalialia kama Watanzania

USA, mataifa mengi Ulaya na India ni miongoni mwa ambao ndege zao bado haziruhusiwi kuingia Kenya, natumai hawatalialia kama Watanzania

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Ilipotolewa orodha ya ndege zinazoruhusiwa kuingia Kenya, na humo Watanzania wakaona zao hazimo, jamaa wamelialia sana ikiwemo hata wale ambao hawajawahi kukaribia uwanja wa ndege na wala hata siku moja hawategemei kuiona ndege wachilia mbali hata kuabiri. Taifa lote kuanzia walalahoi mitaa ya mabandani Tandale, kwenda mikoani vijijini na kote waliifanya kama ndio habari kubwa ya nchi, kila mmoja akawa kama aliyefiwa. Hehehe bandugu zetu huwa mnachekesha sana.

Sasa kwa taarifa zenu, mikakati ya kuzuia baadhi ya mataifa haikufanywa kwa kuzingatia chuki kama mlivyo, tumezuia hata mabeberu USA na washirika wake, maana kwao taarifa za corona hazijakaa sawa, kirusi kinawatesa sana, japo wanatoa taarifa, wanapima na kutoa taarifa, hawajajichokea kama Tanzania ambao wametelekeza zoezi lote na kuachia kila mtu ajiaminishe hakuna corona, aidha ajifie au apone mwenyewe huko atajijua.

Yaani ni kama demu anataka mfanye naye tendo ila hataki mpime UKIMWI, ameng'ang'ania kwamba yeye anajijua yuko sawa na kwamba UKIMWI ni gonjwa la mabeberu na halimhusu na hatoruhusu hata utumie kinga, mfanye naye hivyo hivyo kavu. Watanzania walianza kung'ang'ania mpakani kwamba waingie bila kupimwa, tukakomaa mpaka wakaachia, leo hii wanapimwa na wataalam wetu.

Hii ya ndege pia wameng'ang'ania, sema wataruhusiwa ila lazima tuwapime, ukija Kenya kaa ukijua lazima uwe tayari kupanua mdomo kifaa cha kupima corona kitumbukizwe humo. Hatutaki kuvuna mabua kisa tumecheka nanyi.

========

Kenya has excluded the US and the major European nations from a list of countries whose nationals will be allowed in when international flights resume from tomorrow.

A protocol guiding the resumption of international flights only has Canada, Switzerland, Japan, China and South Korea outside of Africa in the list of 11 countries whose citizens will initially be allowed into Kenya.

This means China is the only country among the top 10 nations that accounted for most of the tourists to Kenya last time that is on the list.

Also on the list are Zimbabwe, Ethiopia, Uganda and, Rwanda, Morocco and Namibia.

The list excludes countries like US, Tanzania, Britain and India, which brought in 743,310 tourists to Kenya or 37.1 percent of the two million travellers.

Source: Business Daily
 
Hatujaribiwi....

IMG-20200801-WA0014.jpg
 
Nasisi hatukulia bali tuliamua tusiwaambukize korona ndio tukaona na nyie msitue kwetu ili msipate corona sasa kwanini manaanza kubadilisha maamuzi nakutoa maelezo yasiyokuwa na tija , kila mmoja angebaki kwake mbona manalilia kuja tz si mngepotezea tu.
 
Nasisi hatukulia bali tuliamua tusiwaambukize korona ndio tukaona na nyie msitue kwetu ili msipate corona sasa kwanini manaanza kubadilisha maamuzi nakutoa maelezo yasiyokuwa na tija , kila mmoja angebaki kwake mbona manalilia kuja tz si mngepotezea tu

Hamtakiwi popote duniani, mumejiponza kwa hilo la kujichokea, ona hii ramani mlivyotiwa nyekundu, nyie pekee yenu ukanda wote huu wa EAC na kati... Kwamba lazima mpimwe mara mbili, mumewekwa kwenye orodha ya mataifa hatari.
Sasa mnalialia kwa Kenya, na hawa mtawalilia kivipi, watawaskliza?

2473175_20200801_164531.jpg
 
Haha! Naona unahangaika sana na Tanzania sijui huna kazi za kufanya? Angalia usije kufa tu kwa jakamoyo...
 
Haha! Naona unahangaika sana na Tanzania sijui huna kazi za kufanya? Angalia usije kufa tu kwa jakamoyo.

Hehehe!!! Wala sihangaiki, najaribu kutafuta mantiki ya kwanini mlilia sana kuliko mataifa yote ambayo hatukuweka kwenye baadhi ya wanaoruhusiwa kuja watakavyo, nyie sasa hivi mumepigwa stop dunia yote, kila ramani inaonyesha rangi nyekundu kwa Tanzania lakini ilipofanywa na Kenya pia aisei mkalipuka ni kama mliokutwa na msiba taifa lote.

Mpaka siku mtakubali kutumia njia za kisayansi kukabiliana na hili janga la kisayansi, mtaendelea kutengwa kote.
Leo hii paspoti ya Tanzania kutua nayo popote lazima ukubali kupitishwa kwenye ukaguzi wa hali ya juu.
 
Mimi ni mtanzania, nilisikitika sana kuona watanzania wenzangu kulichukulia suala la Kenya kuzuia safari za anga kutoka Tanzania kama jambo lililoilenga Tanzania pekee huku tukisahau kuwa Kenya ilizuia karibu nchi zote duniani kutua Kenya na nchi 11 pekee ndio wanaweza kutua Kenya.

Watanzania tunalazimisha sana Kenya watujumuishe kwenye hizo nchi wakati hatukidhi vigezo vyao.

Sababu tunayotumia watanzania ni hafifu sana, eti tunasema kwa kuwa sisi Tanzania tuliwaruhusu watue basi na sisi waturuhusu tutue!

Ni sababu ya kijinga kabisa. Tanzania tumesahau kuwa sisi tulifungua anga letu kwa kila nchi kuja Tanzania (kwa sababu hatuogopi Corona!) sasa tunalazimisha na sisi twende kwao hata kama vigezo vyao vinatukataa.
 
Hamtakiwi popote duniani, mumejiponza kwa hilo la kujichokea, ona hii ramani mlivyotiwa nyekundu, nyie pekee yenu ukanda wote huu wa EAC na kati... Kwamba lazima mpimwe mara mbili, mumewekwa kwenye orodha ya mataifa hatari.
Sasa mnalialia kwa Kenya, na hawa mtawalilia kivipi, watawaskliza?

2473175_20200801_164531.jpg
Wewe unajua maana ya 'kulia' au unarukia maneno bila kujua maana.

Tanzania haijaongea chochote zaidi ya kujibu mapigo kwa maamuzi yenu ya kifala na kukaa kimya.

Kwa kupanua uwezo wako finyu wa kiswahili; Kulialia maana yake ni kulalamikia jambo ili upate huruma ya mwenye maamuzi.

Sasa, kati ya Tz 'the great' na pashikuna Kenya nani analialia🤔
 
Hehehe!!! Wala sihangaiki, najaribu kutafuta mantiki ya kwanini mlilia sana kuliko mataifa yote ambayo hatukuweka kwenye baadhi ya wanaoruhusiwa kuja watakavyo, nyie sasa hivi mumepigwa stop dunia yote, kila ramani inaonyesha rangi nyekundu kwa Tanzania lakini ilipofanywa na Kenya pia aisei mkalipuka ni kama mliokutwa na msiba taifa lote.
Mpaka siku mtakubali kutumia njia za kisayansi kukabiliana na hili janga la kisayansi, mtaendelea kutengwa kote.
Leo hii paspoti ya Tanzania kutua nayo popote lazima ukubali kupitishwa kwenye ukaguzi wa hali ya juu......
Huo ushabiki wa Tz vs Ke utakuua bro, mambo haya waachie vijana labda kama huna kazi za kufanya. Na hiyo mantiki unayoitafuta kwa Tanzania itakusaidia nini kama haiwezi hata kukuletea ugali kwa meza. Nadhani kila nchi iko huru na iachwe ipigane kivyake sioni kwa nini Kenya (only Kenyans) mnalazimisha kutupangia nini tufanye, na kama Tanzania inaficha takwimu kwa nini mnahangaika kutaka kuleta ndege zenu, si mpeleke nchi zingine?

However, Kenyans are not our enemies. Kenyans are our brothers and sisters. They have been our friends since Nyerere's time. How come that it's only this period of time that people speak of our differences! What differences do we have? If the two governments have any issues, they have to sit on table and discuss. We citizens want peace with our neighbours and not otherwise...
 
Hamtakiwi popote duniani, mumejiponza kwa hilo la kujichokea, ona hii ramani mlivyotiwa nyekundu, nyie pekee yenu ukanda wote huu wa EAC na kati... Kwamba lazima mpimwe mara mbili, mumewekwa kwenye orodha ya mataifa hatari.
Sasa mnalialia kwa Kenya, na hawa mtawalilia kivipi, watawaskliza?

2473175_20200801_164531.jpg
Sisi na nyie mnaotutangaza nani kachoka mk?

Tulizeni mishono... kwanza muulize Macharia anamaanisha nini maana amekuwa kama popcorn ndani ya mashine.

Mara haturuhusiwi mara tunaruhusiwa.... au alikuwa anasikilizia upepo?
 
Kenya is currently in a state of disarray...
 
Back
Top Bottom