USA tells Russia : If you are wise America is a phenomena to avoid in war, if you want war with USA prepare someone to raise your Children

USA tells Russia : If you are wise America is a phenomena to avoid in war, if you want war with USA prepare someone to raise your Children

[emoji3][emoji3][emoji3] JF ni therapy tosha
Screenshot_20220430-111732.png

Nchi yako unayoishobokea ina madeni wamewakopa wajapan na wachina matrillion ya dola...
 
Alisikika akisema Mkuu wa majeshi ya Marekani

Anasema Marekani ni Taifa kuliko watu wanavyodhani anasema huu ujumbe nadhani Urusi, Iran, IS na North Korea wanaangalia , Kama una akili timamu Amerika ni Nchi ya kuikimbia kwenye vita maana imeona vita, imecheza vita na unajua vita na haipendi vita.

Lakin ukipenda vita na Marekani andaa wa kulea watoto wako maana hutabaki salama! Vita siyo sehemu ya maonesho ya Bunduki kwa amerika bali ni vitendo.

View attachment 2200587
Cheo chake ni gani? Anataka vita vya nuclear anafikiria vita vya nuclear vitakuwa one sided? Russia pia wanasema wako na hypersonic weapons ambazo marekani haiwezi kugundua angani.
 
Hahaha mikwara tena..

Mi nilidhani washapeleka jeshi Ukraine kumbe maneno ya kwenye khanga..
Mkuu umemfahamu lakini generali? kama ni vita wao hawapendi vita kama maonyesho anavyofanya yule kiduku na aila zake lakini ukilazimisha basi utafute mtu wakuja kukulelea wajukuu zako., huu ujumbe unafaa kutafakariwa sana kwa pro putin na aila zake
 
Alichonifurahisha alipambana Afghanistan kwa miaka 20 kuwaondoa Taliban ili kuwaweka Taliban

Sent from my SM-G5500 using JamiiForums mobile app
Mkuu taliban alifatwa Osama bin laden basi kazi iliishia hapo, otherwise marekani wameona kuendelea kubaki taliban ni kupoteza hela tu malengo yalishatimia wakaona wawaachie nchi yao na mapochopocho ya silaha kibao za kitaalamu wameachiwa
 
Kapigwa rafiki yake mchana kweupe na hajapeleka ngumi.
US hamwezi Urusi
Mkuu nakutoa taka za masikio ukisikia US ni marekani na aila zake, nchi za Ulaya wote wako na Marekani usijaribu kudhania kwamba ni mmoja kwa mmoja tu, Marekani ukijarib tu dunia itafumuka kote kukulenga wewe ndio ujanja huwa wenzetu walioutumia marekani miaka na kaka
 
Duh hiyo huitwa psychological war fare unapigwa kwa maneno ushundwe moyoni kabla ya uwanjani vitani.
Kwa marekani ndivyo ilivyo huu ujumbe hawa jamaa wanamaanisha, marekani hawana maonyesho ya silaha ni moja ya mbinu kubwa kumshinda vita adui, tuombe salama tu yasitokee hayo
 
Mkuu taliban alifatwa Osama bin laden basi kazi iliishia hapo, otherwise marekani wameona kuendelea kubaki taliban ni kupoteza hela tu malengo yalishatimia wakaona wawaachie nchi yao na mapochopocho ya silaha kibao za kitaalamu wameachiwa
Usisahau wamekaa miaka 20 bila kuwamaliza Taliban(Twaliban). Mwisho wakaamua kukimbia.
Ama silaha hawakuwa na uwezo wa kuzichukua. Haraka ya kukimbia iliwaponza

Sent from my SM-G5500 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu nakutoa taka za masikio ukisikia US ni marekani na aila zake, nchi za Ulaya wote wako na Marekani usijaribu kudhania kwamba ni mmoja kwa mmoja tu, Marekani ukijarib tu dunia itafumuka kote kukulenga wewe ndio ujanja huwa wenzetu walioutumia marekani miaka na kaka
Hiyo inafanya kazi kwa Iraq,Libya n.k.
Kwa mrusi hata Marekani anajua kuna mataifa yaliyochoshwa na ubabe wake,hapo watakuwa wamepata nafasi adimu. Watamgeuka. Na usishangae hata wenzake wa NATO. Nchi aliyo na uhakika nayo ni Uingereza tuu. Kwani yule nyumbu ni kama mwanamke mtiifu kwa mume wake.
Rejea juzi tu German mpaka wamemuitishia kikao kumbana ndipo kaahidi kupeleka silaha Ukraine.

Hakuna kiongozi mwenye akili atakubali nchi yake kurudishwa zama za mawe kisa tu kumfurahisha America.

Sent from my SM-G5500 using JamiiForums mobile app
 
Kwa marekani ndivyo ilivyo huu ujumbe hawa jamaa wanamaanisha, marekani hawana maonyesho ya silaha ni moja ya mbinu kubwa kumshinda vita adui, tuombe salama tu yasitokee hayo
Ana maonesho. Tena maonesho yake ni ya kishetani. Anatafuta taifa dhaifu halafu anaenda kuonesha silaha zake.
Ref. Tambo zake aliposhusha bomu lake kule Afghanistan. Bomu aliloliita "mama wa mabomu yote"

Sent from my SM-G5500 using JamiiForums mobile app
 
Hapana..
Mwanzoni alikuwa Afghanistan, mashambulizi yalipoanza akajichimbia kwenye mapango ya milima ya Tora Bora. Mabomu yaliporindima vikali huko milimani ndo akaponyoka akavuka kwenda Pakistan
Kwenye ishu hiyo,Marekani aliionea serekali ya Mullah Omar. Kwasababu;
1. Usamah aliingia kule kuwasaidia kupambana na Russia. Tena kwa msaada wa Marekani na washirika wake. Wakawamiminia silaha za kila aina,mafunzo na mbinu za kumkabili Russia.(kosa hili Marekani analirudia Ukraine. Huenda anawaandaa akina Usamah wengine) Hivyo Usama aliiva kwenye ujasusi,mbinu,silaha na jeshi imara likitumia mbinu ya imani ya kidini.

2. Taliban kwakulijua hilo,walimuomba Usamah ajisalimishe ili kuondoa mzozo. Osamah alikataa.

Kwanguvu alizokuwa nazo Taliban hawakuwa na uwezo wa kupambana na Alqaida. Na kumkabidhi kwa Marekani kama lilivyokuwa takwa la Marekani.

3.Usamah alifanikiwa kujijenga kama mpigania dini(ukweli ni kinyume chake na ndio sababu ya kuvuliwa uraia Saudia).
Hivyo lau Taliban wangepambana naye wangeanzisha upinzani wa ndani.

4. Marekani akiyajua yote hayo bado aliilazimisha Taliban imkabili Usamah. Jambo ambalo Taliban hakuwa na uwezo nalo. Badala ya kuwataka wawape nafasi wamarekani wenye nguvu hiyo,wao waliitaka Taliban wafanye hivyo. Ama sivyo watawashambulia wao. Ni rahisi kupambana na serekali si vikundi vya kuvizia hasa vinavyopambania imani. Na hili America walilijua ndio sababu ya kuilazimisha Taliban.

5. Kwakuwa Taliban hakuwa na uwezo wakumkamata Usamah,walikaa kusubiri mashambulizi ili wajitetee. Na wakaamua kushirikiana na Usamah kujitetea.
America wakafanikiwa kuiangusha serekali. Lakini sio kuwamaliza Taliban. Kwa miaka 20 wamekuwa wakipambana kwa kuviziana. Pamoja na miguvu yake aliyonayo bado hakufanikiwa kuwaangamiza. Kinyume chake Taliban ndio walikuwa wakiimarika zaidi.

Kuthibitisha hilo raisi aliyekua madarakani alikimbia kwakuwahofia Taliban na kuwaachia nchi.

Kile Marekani alichokuwa anakikwepa,alipambana nacho kwa miaka 20. Badala ya kumaliza tatizo,alijikuta akiwakomaza zaidi Taliban kivita.
Hakua na namna ila kukimbia kwa gia ya mkataba.

Sent from my SM-G5500 using JamiiForums mobile app
 
US hawezi kupigana peke yake hata siku moja lazima afanye ushirikiano na majeshi ya nchi zingine, huwezi kuifananisha Urusi kijeshi na nchi inayojigamba kwa kupigana huku ikitegemea kushirikiana na majeshi ya nchi zingine
Na siku akilogwa apambane peke yake ndio utakuwa mwisho wake. Yule akiwa peke yake JWT wanawamudu kabisa[emoji28]

Sent from my SM-G5500 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom