Hapana..
Mwanzoni alikuwa Afghanistan, mashambulizi yalipoanza akajichimbia kwenye mapango ya milima ya Tora Bora. Mabomu yaliporindima vikali huko milimani ndo akaponyoka akavuka kwenda Pakistan
Kwenye ishu hiyo,Marekani aliionea serekali ya Mullah Omar. Kwasababu;
1. Usamah aliingia kule kuwasaidia kupambana na Russia. Tena kwa msaada wa Marekani na washirika wake. Wakawamiminia silaha za kila aina,mafunzo na mbinu za kumkabili Russia.(kosa hili Marekani analirudia Ukraine. Huenda anawaandaa akina Usamah wengine) Hivyo Usama aliiva kwenye ujasusi,mbinu,silaha na jeshi imara likitumia mbinu ya imani ya kidini.
2. Taliban kwakulijua hilo,walimuomba Usamah ajisalimishe ili kuondoa mzozo. Osamah alikataa.
Kwanguvu alizokuwa nazo Taliban hawakuwa na uwezo wa kupambana na Alqaida. Na kumkabidhi kwa Marekani kama lilivyokuwa takwa la Marekani.
3.Usamah alifanikiwa kujijenga kama mpigania dini(ukweli ni kinyume chake na ndio sababu ya kuvuliwa uraia Saudia).
Hivyo lau Taliban wangepambana naye wangeanzisha upinzani wa ndani.
4. Marekani akiyajua yote hayo bado aliilazimisha Taliban imkabili Usamah. Jambo ambalo Taliban hakuwa na uwezo nalo. Badala ya kuwataka wawape nafasi wamarekani wenye nguvu hiyo,wao waliitaka Taliban wafanye hivyo. Ama sivyo watawashambulia wao. Ni rahisi kupambana na serekali si vikundi vya kuvizia hasa vinavyopambania imani. Na hili America walilijua ndio sababu ya kuilazimisha Taliban.
5. Kwakuwa Taliban hakuwa na uwezo wakumkamata Usamah,walikaa kusubiri mashambulizi ili wajitetee. Na wakaamua kushirikiana na Usamah kujitetea.
America wakafanikiwa kuiangusha serekali. Lakini sio kuwamaliza Taliban. Kwa miaka 20 wamekuwa wakipambana kwa kuviziana. Pamoja na miguvu yake aliyonayo bado hakufanikiwa kuwaangamiza. Kinyume chake Taliban ndio walikuwa wakiimarika zaidi.
Kuthibitisha hilo raisi aliyekua madarakani alikimbia kwakuwahofia Taliban na kuwaachia nchi.
Kile Marekani alichokuwa anakikwepa,alipambana nacho kwa miaka 20. Badala ya kumaliza tatizo,alijikuta akiwakomaza zaidi Taliban kivita.
Hakua na namna ila kukimbia kwa gia ya mkataba.
Sent from my SM-G5500 using
JamiiForums mobile app