USA: Uchaguzi 2020

USA: Uchaguzi 2020

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Mbio za uchaguzi wa wa marekani kumchagua rais, wabunge congress wote 435 na maseneta 35 kati ya 100 zimeanza kuwapa nguvu bainba ya Democrats na Republicans.

Kwa sasa hivi Democrat ina wabunge 232 wakati republican inao 197; kwa jumla Democrat imeposhateza mbunge mmoja aliyehama kuwa republican iliyokuwa imepoteza mbunge mmoja aliyeamua kuwa independent. Demokrat wangependa kuendelea na idadi yao hiyo hiyo au hata kama wakipoteza wasipoteze zaidi ya ya wabunge 17. Ramani ya Uchaguzi inaonyesha kuwa ngumu kidogo kwa demokrat kwa sababu viti vilivyoipa demokrat ushindi mwaka 2018, viko katika maeneo ya weupe tu, ambao ni wapiga kura wa Trum, kwa hiyo kuna uwezekanao mkubwa sana kuwa mwaka 2020 vitakwenda Rpublican, hata hivyo kuna viti kadhaa kule Virginia, North Calorina, Texas na Arizona ambavyo vilikuwa vimekaliwa na Republican vinaegemea kwenda Domkrats, kwa hiyo ukiweka kwenye mizani kama polls zinavyoonyesha mpaka sasa hivi Demokrats was 6 point advantage.

kwa upande wa Senate, Republican wana viti 52, wakati democrat wana viti 45, na independent wanachukua viti viwil ingawa hawa indendents mara nyingi huungana na Democrats. Republican wangependa wabaki na namba yao ile ile, na hata wakipteza, basi wasipteze zaidi ya viti viwili. Demorat wao wanata wapate viti angalu vitatu vya senate ili waichuke Senate ikichukuliwa kuwa viti vya indendent vitaendelea kuwa vinashikirikiana na democrats. Sasa Ramani inavyoonyesha ni kuwa Demkrat wana halingumu kwenye kiti cha Albama kwa vile Jeff Sessions anakitaka tena, na kama tujuavyo State ya Alabama ni katiya zile dixie states ambazo ni republican tupu, kwa hiyo Doug Jones anaweza asirudi kwenye Senate. hata hivyo kwa upande wa Republicans mambo yao pia siyo mazuri sana hasa kwenye states za Arizona, Colorado, na North Calorina na Maine. Polls za sasa zinaonyesha kuwa viti hivyo vinaweza kuangukia Demokrat kirahisi sana, kwani on average Democrats wana advantage ya kati ya 4 na 7 points. Kiti kimoja cha state ya georgia pia kina mashakaingawa odds ni kuwa kitabaki republica, ina siku za hivi karibuni state ya Georgia imekwa inageukia democrats zaidi ingawa nayo ni mojawapo ya Dixie states. Kiti kinachokaliwa na mkuu wa Senate sasa cha kentucky nacho kinasemekana kuwa mashakani, lakini odds pia ni ndogo sana kwa kiti hicho kuangukia demcrat

Kiti cha urais mpaka sasa bado nia pata potea kwani inategemea democrats watamsimamisha nani. Udhaifu wa Democrats ni kuwa wafuasi wake wengi ni wale wanaotaka serikali ya welfare itakayokuwa inawapa free stuff nyingi; kwa hiyo wanapomsikia Sanders anawaaihidi kila kitu free, basi wanaelekea huko huko, na kuna odds kubwa sana kuwa Sanders anaweza kuwa nominee wa Democrats. Wachambuzi wengi wanaonyesha kuwa Sanders akiwa nominee, basi wapiga kura wengi independents watampigia kura Trump hata kama hawamtaki, au hawatapiga kura kabisa na hivyo kufanye ile base ya Trump ishinde. Dhana ya free stuff inayosimamiwa na wafuasi wa Sanders kama huyu mwanadada wa New York Alexandra (AOC) aliyepinga kuwa Amazon isijenge ofisi yake New York kwa msamaha wa kodi, badala yake hizo pesa za kusamehewa kodi wapewe waalimu, ndiyo itakayoangusha chama cha Democrat. Kwa bahati mbaya matokeo ya uchaguzi wa rais ndio pia huathiri matokea ya uchaguzi wa Senate na congress.

Hali ya Uchumiilivyo sasa, ni bahati sana kwa Trump kuwa alikuta uchumi imara na hakuvuruga, hivyo sasa anachukua credit yote. Angekuwa kiongozi mzuri, nadhani demokrat wangekuwa na ugumu sana wa kupambana naye, ila sasa Odds za trump kushinda tena ziko 50-50 kutegemea na candidate atakelewa na democrat. Kuna wasiwasi kuwa iwapo Blumberg ndiye atakayeletwa na democrat, basi Trump atakuwa katika hali mbaya sana. Tatizo kubwa kwa Democrat litaletwa na Sanders asipokuwa nominated, kwani anaweza kutuma indirect ujumbe kwa wafuasi wake kutopiga kura tena kama alivyofanya mwaka 2016
 
Huyo bwana sijui anachambua kutoka wapi asione kuwa hao Democrats hawana strong candidates hadi hata shoga anashiriki kwenye hizo primaries zao.

Sioni hao Democrats wakiwa na nafasi yoyote hasa kwenye kiti cha urais, wao wajipange tu kwa 2024.

Wamezusha "Impeachment" ya uongo na kweli wakawaka sasa wanakuja hadi na mashoga kugombea. Hao Dems ni bure kabisa hawana maana.
 
Huyo bwana sijui anachambua kutoka wapi asione kuwa hao Democrats hawana strong candidates hadi hata shoga anashiriki kwenye hizo primaries zao.

Sioni hao Democrats wakiwa na nafasi yoyote hasa kwenye kiti cha urais, wao wajipange tu kwa 2024.

Wamezusha "Impeachment" ya uongo na kweli wakawaka sasa wanakuja hadi na mashoga kugombea. Hao Dems ni bure kabisa hawana maana.
sijui kama umeelewa post yangu. swala la ushoga ni watu kama wewe ndio wanahangaika nalo, lakini wenzio wamarekani hawana taimu nalo kabisa. huyo unayemwita shoga alikuwa meya mara mbili tena kwenye state ya wahafidhina Indiana kwa pence.
 
Trump will win. Republicans will control the Senate and probably the House

Sent using Jamii Forums mobile app
odd za trump zinategemea sana candidate wa democrats.wakileta Sanders, basi Trump anapita kirahisi sana, lakini wakileta mwingine, basi odds ni 50-50 kwani Trump anategemea base yake zaid; ana independent wachache sana. Wanawake wa mijini wote wameshamkimbia..Ushdini wa kutegemea base tu hauna guarantee sana, yaani anataka akutane na candidate ambaye pia hapendwi na independents, kama ilivyo kwa Sanders sasa hivi.
 
Back
Top Bottom