Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Usafi na mpangilio mzuri wa vitu vya ndani huenda pamoja. Huwezi kuwa msafi lakini ushindwe kupanga vitu vyako vizuri. Wana saikologia husema mpangilio mzuri wa vitu husaidia akili kutulia.
Kuna wanaofikiria usafi huendana na uwezo wa kiuchumi. Hapana kuna watu wanaishi maisha duni lakini akikupa maji ya kunywa kwenye kikombe cha bati kina ng’aa unaweza ujione. Ingawa maziringira huchangia, si rahisi kuishi kwenye chumba kimoja unapikia kuni na moshi unatanda na kuta za nyumba ziwe safi.
Kuna watu mpangilio wa nyumba unamshinda anasingizia watoto. Watoto ukianza kuwafundisha mapema mnaweza kusafisha na kupanga nyumba pamoja. Michezo yao unawaonyesha sehemu ya kuhifadhi.
Wanaume wengine hushindwa kukaa katika mazingira yasiyo na mpangilio. Mtu ametoka kazini na stress za boss, akifika nyumbani anakuta mambo vurumai. Huyu akipata mchepuko unaojua usafi na mpangilio wa vitu andika maumivu.