Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
USAFI WA MWILI NA ROHO, FUNGUO NO 2.
Kwa Mkono wa, Robert Heriel
Andiko hili ni moja ya maandiko ya msingi, ambayo sharti uyazingatie. Usijesema mimi Baba yako, sikukwambia.
Jumbe hii isomwe wana na binti zangu, na rafiki zao, na familia zao, na jamaa, pia ikiwapendeza na wote waishio duniani. Isomwe kwa hekima kwa hao wenye hekima, pia isomwe kipumbavu kwa hao waliowapumbavu.
Wote walizaliwa wakiwa safi, miili ms roho zao zilikuwa safi zikiwa zimetakaswa. Lakini Dunia imewaharibu, nao wakaupenda uharibifu huo. Nao wamekuwa wachafu wa mwili na roho, hata kila wakishikacho kinachafuka, kila wakanyagapo huacha uchafu, na kila wasemapo hutoa uvundo midomoni mwao. Hayo nayo niliyasema.
Niite Taikon wa Fasihi, mwana wa Tibeli, nyota yenye mbawa mbili irukayo toka anga moja hata anga za mbali.
Basi niongee kama mwalimu, nawe unisikilize kama mwanafunzi mwenye akili ya udadisi, nisitumie lugha ngumu, bali lugha laini ili asiwepo atakayeshindwa kunielewa.
USAFI.
Upo usafi wa Mwili(physical cleanliness) na Usafi wa Roho(The Purity of the Spirit)
Usafi maarufu ambao kila mtu anaujua, ni ule usafi wa mwili(Physical Cleanliness- PC) ambao unahusisha kusafisha viungo vya mwili. Kama vile kuoga, kusafisha kinywa kwa mswaki, kuchamba/kutawaza baada ya haja kubwa na ndogo, kufua nguo tunazozivaa kila siku.
Pia Usafi wa mwili unahusisha vitu tunavyokula na kunywa, mathalani, usafi wa chakula na matunda, usafi wa maji tunayokunywa, na vyombo tunavyotumia kulia na kunywia vimiminika.
FAIDA ZA USAFI WA KIMWILI
1. Ni nyenzo ya Afya ya mwanadamu. Usafi wa kimwili huleta Afya imara
2. Kuboresha mahusiano kati ya mtu na watu wengine.
Mtu akiwa msafi wa kimwili huvutia watu wengine. Usafi huboresha mahusiano baina ya watu.
Usafi huboresha mahusiano ya wanandoa, wachumba, watu wengi hupenda wenza wao wawe wasafi, watanashati na warembo.
3. Usafi huleta furaha, na utulivu. Nk.
Watu wengi wakiamka asubuhi huzingatia usafi wa mwili, kwa kusafisha vinywa na kukoga kisha ndio waende makazini kutafuta riziki zao.
Wakati wa jioni wakirudi pia husafisha miili yao ndipo walale.
Kosa kubwa watu wanalolifanya ni kuwa wanajikita zaidi kusafisha miili yao ilhali roho zao wakiziacha hivi hivi zikiwa chafu zinazonuka uozo. Hali hii huwaathiri katika shughuli zao wawapo katika utafutaji wa riziki,
Usafi hufanywa kwa kutumia mambo yafuatayo;
1. Maji
2. Moto
3. Damu
Usafi wa mwili hutumia zaidi maji na Sabuni ili kuufanya mwili utakasike.
Usafi wa Roho hutumia zaidi Moto na Damu kuifanya Roho itakate.
Moto huzalishwa kupitia mambo yafuatayo;
1. Maombi, Sala na Dua kwa waumini wa Mungu Mmoja.
2. Matambiko, Manuizo, uganguzi, ulozi kwa waumini wa ushirikina, mizimu, majini, uchawi, uganga na shetani.
Damu hutumika yoyote kutegemeana na aina ya uchafu unaotakiwa kusafishwa. Inaweza kuwa damu ya kondoo, mbuzi, njiwa, ng'ombe au hata damu ya mtu.
Kama vile unavyojiweka safi kimwili unapoenda kazini kwako, iwe Shuleni, Hospitalini, Mahakamani, Gereji, Studio, kwenye Magari, Dukani au sokoni au kazini popote kwa kadiri ya kazi yako. Ndivyo unapaswa uwe Msafi kiroho ili ujenge mahusiano mazuri na wanaokuzunguka.
Unapokuwa mchafu kimwili na kimavazi watu hukuona kero na wengine hukuona kama kichaa. Hivyo hawana time na wewe na ikiwezekana wanakufukuza. Hivyo hivyo roho yako inapokuwa chafu inakuwa kero kwa roho za wengine na roho za wengine zinakuona kama kichaa.
Roho hazionekani kwa macho, lakini roho yako inaonana na roho za watu wengine. Ikiwa roho yako ni chafu au imechafuliwa na huna mpango wa kuisafisha basi unahatari ya kujiona mtanashati kimwili kumbe kiroho wewe ni mwendawazimu unayeokota makopo.
Tatizo kubwa la Roho kuwa chafu linajitokeza pale watu wanapokuchukia bila sababu, kuandamwa na mikosi, pesa umeifanyia kazi haiji kwa wakati, kudhulumiwa kila mara,
Kwa vijana unakuta unapendeza vizuri, unahela lakini wanawake hawakupendi,
Au mwanamke mrembo, msafi, unauzuri usiosemeka, umbo kama lote lakini bado wanaume hawakufuati, na wakikufuata wanakaa muda mrefu. Basi jua kuwa kuna kila dalili roho yako ni chafu.
Uchafu unatabia ya kujilimbikiza mpaka kutoa ukurutu au nongwa. Hivyo kama Roho yako inaukurutu basi yakupasa uisafishe haswa ili itakate.
Unapaswa kila unapoamka asubuhi, kama vile unavyopiga mswakili na kuoga asubuhi na mapema, vivyo hivyo unapaswa kuitakasa roho yako kwa kuomba toba ya kweli ili utakaswe.
Andiko hili sio la kidini, bali ni andiko linalohusu mwili na roho ambavyo kila mtu anavyo.
Hata wanaoenda kwa waganga wa kienyeji, wanajua mambo haya, huwezi fanyiwa uganga wowote ukafanikiwa pasipo kusafishwa kiroho iwe kwa kuchinja mnyama, kuua mtu au kuogeshwa na mitishamba ili roho yako iwe safi. Kiuganga huitwa KUSAFISHA NYOTA YAKO.
NAMNA YA KUSAFISHA ROHO YAKO
1. Kila uamkapo Omba Dua kwa kufuata kanuni na uelekeo wa Jua linapochomoza ikiwa unaomba mambo ya kheri, na ikiwa unakemea mambo mabaya, mikosi, au unazika takataka basi utageukia magharibi. Ikiwa upo sehemu usiyojua jua linapochomozea na kuzamia, basi toka nje uangalie uelekeo wa upepo. Kule upepo unapotokea omba baraka, kule unapoelekea zika laana, mikosi na kemea mabaya.
2. Kabla hujaomba, chukua moja ya viumbe vyenye sifa za kuponya na kuua lakini vyenyewe ni viumbe hai mfu. Kama MAJI na Moto.
Chagua maji au moto.
Ukichagua maji basi weka kwenye kikombe. Ukichagua moto basi unaweza washamoto wa kuni lakini usiozimika mpaka utakapomaliza ibada yako. Ikiwa utaona inakusumbua, basi chukua mishumaa.
Kisha waweza fanya ibada ya kusafisha roho yako.
Nikupe mfano, kama umeamua kuchagua MAJI utafanya kwa mfano huu
Utachukua hiyo Glass yenye maji yenye ujazo kwa kadiri na mahitaji yako.
Utasujudu mpaka ardhini. Kisha utashika hiyo Glass, mkono wa kushoto utakuwa chini kwenye kitako cha Glass, mkono wa kulia utafunika kwa juu mdomo wa Glass.
Kisha utafumba macho yako na kuanza kuomba, zingatia uelekeo wa mawio na maachweo ya jua, na kama huyajui basi nalikuambia uelekeo wa upepo.
Kisha utaomba dua yako kulingana na mahitaji yako. Ukishamaliza, utasema maneno mfano wa maneno haya;
" Wewe Maji, uliyeumbwa na Mungu, ule uwezo uliopewa na Mungu mkuu wa kuweza kuotesha Mbegu zilizoardhini, ule uwezo uliopewa na Mungu Mkuu wa kukata kiu ya viumbe, Ule uwezo uliopewa na Mungu Mkuu wa kusafisha na kustawisha mimea. ule uwezo uliopewa wa kuisafisha dunia na kuiosha kwa mvua, Basi uwezo huo huo utumie kuotesha na kustawisha biashara(kazi yoyote unataja) yangu, Safisha roho yangu na uitakase, safisha kazi na biashara yangu, au ndoa(unataja kile unachotaka kisafishwe), Ikate kiu ya mafanikio yangu.
Ewe maji ule uwezo uliopewa na Mungu Mkuu wa kuzima moto, Ule uwezo uliopewa na Mungu Mkuu wa kuua na kugharikisha, Ule uwezo uliopewa na Mungu Mkuu wa Kulegeza na kutepeza, basi uwezo huo leo hii nautumia kuua adui, majini uchawi wote uliokuwa katika njia yangu(biashara, ndoa, kazi nk), nagharikisha leo na kuwafurikisha adui zangu waangamie hivi leo, nawazima kama vile maji uzimavyo moto ndivyo ninavyowazima hvi leo adui zangu"
Ukishamaliza kunene hivyo, Utamalizia na maneno haya;
" Maji Takasika, utasema mara saba
Maji Safishika utasema mara saba
Maji otesha na stawisha. utasema mara saba
Maji Gharikisha na ua. Utasema mara saba"
Hii itakuwa Dua ukiwa umefumba macho.
Ukishamaliza, utafumbua macho yako, kisha utasimama toka ardhini. Kisha utaanza kumwagia maji hayo pande zote za Ofisi yako, biashara yako, au shamba lako. Nyumba yako.
Hii utafanya ukigeukia upande huu utamwagia mara tatu, kisha utageukia upande wa pili utamwagia mara tatu, hivyo hivyo kwa pande nne. Hivyo utamwagia maji mara kumi na mbili,
Hivyo utafanya kila siku unapoamka ukienda kazini. Utafanya hivyo nyumbani ikiwa ofisini kuna watu wengi wasijekukuita mchawi.
Lakini kama umejiajiri mwenyewe fanya hivi kila siku kabla hujafungua ofisi yako.
Kisha utakuja kunishukuru.
Zingatia Maji hayana nguvu bali wewe ndio unayapa nguvu ya Mungu kwa kuyaruhusu yafanye kile ukitakacho.
Mambo haya ni amini na kweli. Ingawaje yanatumika kwa masuala mepesi, kwa ishu complicated hatua zaidi zitahitajika.
Utakaso wa Moto, mishumaa ikiwa kama ishara na kielelezo sitaeleza kwa leo kwani makala imekuwa ndefu
Ulikuwa nami, Mwana kutoka Nyota ya Tibeli.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Morogoro