Usafi wa Mwili vS Usafi wa Roho; Funguo no 3

Usafi wa Mwili vS Usafi wa Roho; Funguo no 3

Katika maombi yako umechanganya na ushirikina sana hivyo hayatakuwa na nguvu yeyote.

Ngoja nikufundishe jambo litakalokusaidia mwandishi pamoja na wengine wanaokufatilia .

Ni hivi kabla hujaomba dua/maombi yeyote kwanza tambua kuwa hakuna kiumbe chochote duaniani ama mbinguni chenye uwezo wa kumnufaisha mtu ama kumdhuru pasi na idhini ya MUNGU (Mmoja) ambaye hana msaidizi,mtoto wala mshirika katika mamlaka na maamuzi yake.

Ukishatambua hili utajua kuwa hakuna chochote kistahilicho kuabudiwa wala kuombwa isipokuwa MUNGU (Muumbaji) peke yake.Hivyo kama mwanadamu hupaswi kukiomba kiumbe kingine chochote kikutatulie matatizo yako zaidi ya MUNGU.

Hivyo hupaswi kuliomba Jua,mwezi,nyota,mti,maji,moto,mwanadamu,jini,malaika etc. Ukiomba muombe MUNGU pekee.

Nachelea kusema kuwa maombi yako yamejikita zaidi katika kuvitukuza viumbe (maji na moto) vikunufaishe ama vidhuru!!

NINI ULITAKIWA USEME?
Katika maombi yako ulitakiwa useme hivi ewe Mola mlezi uliyeumba mbingu,ardhi,nyota,mwezi,jua,maji,moto,upepo,bahari,mito na vyote ninavyovijua na vile nisivyovijua nakuomba kupitia maji haya uyajaalie yawe ni Tiba au ponyo (pozo) dhidi ya maradhi haya (utayataja) au shida hizi na zile (nuksi,mikosi,uchawi,vijicho n.k) .Then hapo maji (mafuta/uji,chakula n.k) hayo utakuwa umeyaombea kwa Mungu yawe na nguvu ya uponyaji ,ikiwa umetupiwa uchawi basi unaweza kuyaoga na mengine kunywa ili kwenda kutibua uchawi au viumbe (mashetani) ambao wamejificha ndani ya mwili wako. Au unaweza kumwagia maji hayo kuzunguka nyumba yako au sehemu yako ya biashara n.k

KUMBUKA:

Maji hayana uwezo wa kutibu /kukunufaisha wala kudhuru pasi na uwezo (idhini) ya aliyeyaumba (MUNGU).Hivyo maombi yako unapoomba jikite kumuomba MUNGU (Muumba) ambaye hana mshirika na hapendi kushirikishwa katika ibada.

Ni vyema maombi haya ukayafanya katika theluthi ya mwisho wa usiku pindi watu wengi wamelala yaani kuanzia saa 8 usiku mpka saa 10 usiku...amka oga na kisha piga goti uombe toba na kisha uombe lile unalolitaka kutoka kwa MOLA WAKO MLEZI.

MUNGU anapenda kuombwa yeye peke yake hivyo ana wivu sana na anakasirika sana pindi anapomuona mwanadamu anaomba wengine pamoja/ badala yake YEYE
 
Back
Top Bottom