Baada ya Jamii Forums kuripoti kuhusu Soko la Kawe kuwa chafu kutokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni Jijini Dar es Salaam, mamlaka zimeanza kuchukua hatua ya kufanya usafi sokoni hapo.
Barabara ya kuelekea sokoni hapo imeanza kufanyiwa marekebisho ya kuwekewa vifusi, ambapo awali kulikuwa na matope mengi, mazingira yaliyokuwa na taka nyingi nayo yamefanyiwa usafi.
Soko hilo lipo katika Jimbo la Kawe ambalo Mbunge wake ni Joseph Gwajima.