Usafi wakati wa kupika

Tamalisa

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2015
Posts
2,542
Reaction score
905
Habari zenu wana jamvi,napenda tukumbushane kidogo juu ya usafi katika hili suala la mapishi. usafi huu ni wa pande 3.

1.Usafi wa mpishi.

2.Usafi wa pishi/mapishi yenyewe.

3.Usafi wa mazingira ya mapishi.

Nilinukuu kauli moja toka kwa mwanaume fulani wakati wa maongezi, akisema "nikimkuta mke wangu anapika akiwa mchafu au mazingira anayopikia ni machafu, yani nashiba kabisa".

Wanawake hasa wale tulioko katika ndoa, ni muhimu tuwe wasafi wakati wa kutayarisha chakula, ukiwa umevaa vizuri na hata nywele zako zinapendeza inavutia sana, hakikisha unachokipika unakiosha vizuri hasa mboga za mjani,maboga unakuta mtu amepika spinachi au mchicha una michanga mitupu, je huyu akipika majani ya maboga.

Itakuaje, osha mchele wako kwa makini, pia hakikisha vitu kama nyanya, vitunguu au bamia nk. ulizoandaa vimefunikwa vizuri na sio kuacha wazi. Huku watoto wanakimbia hovyo eneo la jikoni eneo zima la mapishi liwe safi.

Hata kuepusha inzi kukuzunguka, unaweza hakikisha vitu uchafu wote uliopokaribu nawe unauondoa kama maganda nk hii itasaidia kufukuza inzi,yani vyakula ukiwa unakula unakutana na vipande vya mkaa, vijiti, michanga ndo hatari.

NB: Tupike tukiwa tunathamini na kujali wanaokuja kula, watoto, waume, wazazi, ndugu, na sisi wenyewe.Na wale wenye tabia ya kulamba mwiko eti unaonja, ni uchafu weka katika kiganja onja na si zaidi ya mara 2.Please usipende kuonja hadi unashibia jikoni.

Asanteni.
 
haswaa, mi lakuonjaonja linaniboa. pia sipendezewi na mtu kuongeaongea wakati anapika, nahisi kama mate yaweza ingia kwenye hicho chakula.
 
Mada nzuri hilo la usafi kuhusu nywele me nashauri ufunge kabisa na kitambaa

kweli suluhisho nywele zskae wazi wakati wa kupika. tena skuhizi vilemba na vikofiakofia vipo tele.
 
haswaa, mi lakuonjaonja linaniboa. pia sipendezewi na mtu kuongeaongea wakati anapika, nahisi kama mate yaweza ingia kwenye hicho chakula.

Hahahahha umenichekesha me wanawacha hoi ma chef wa kizungu wanaonja alafu kijiko hicho hicho wanapikia saa nyengine wanaonja kinabaki kinarudishwa lol alimadi balaa au unakuta wanamenya kitu hakioshwi chapikwa hivo hivo au sijui kwa vile vidudu vyote vinakufa vikipikwa lol
 
Mimi hata uwe msafi vipi, kama umejichubua sili chakula chako hata kwa ngumi....
naona kinyaa
 
Mada nzuri nimeipenda....kuna wadada unakuta anakucha ndefu,kapaka na rangi ila anapika!Unawezaje kupika ukiwa na mikucha mirefu? Wengine anapika huku anajikuna au unakuta kanga chafuuu na hiyo hiyo anafutia vyombo(nshawahi kuona na sikula kile chakula). Kwenda msalani si kiss lakini mtu ajikaze either ahakikishe anaenda kabla au ajibane akimaliza ila inatia kinyaa kwenda katikati ya mapishi.Kingine kupenga kamasi yani daaah ngoja niishie hapa.Asante mleta mada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…