Tamalisa
JF-Expert Member
- Feb 3, 2015
- 2,542
- 905
Habari zenu wana jamvi,napenda tukumbushane kidogo juu ya usafi katika hili suala la mapishi. usafi huu ni wa pande 3.
1.Usafi wa mpishi.
2.Usafi wa pishi/mapishi yenyewe.
3.Usafi wa mazingira ya mapishi.
Nilinukuu kauli moja toka kwa mwanaume fulani wakati wa maongezi, akisema "nikimkuta mke wangu anapika akiwa mchafu au mazingira anayopikia ni machafu, yani nashiba kabisa".
Wanawake hasa wale tulioko katika ndoa, ni muhimu tuwe wasafi wakati wa kutayarisha chakula, ukiwa umevaa vizuri na hata nywele zako zinapendeza inavutia sana, hakikisha unachokipika unakiosha vizuri hasa mboga za mjani,maboga unakuta mtu amepika spinachi au mchicha una michanga mitupu, je huyu akipika majani ya maboga.
Itakuaje, osha mchele wako kwa makini, pia hakikisha vitu kama nyanya, vitunguu au bamia nk. ulizoandaa vimefunikwa vizuri na sio kuacha wazi. Huku watoto wanakimbia hovyo eneo la jikoni eneo zima la mapishi liwe safi.
Hata kuepusha inzi kukuzunguka, unaweza hakikisha vitu uchafu wote uliopokaribu nawe unauondoa kama maganda nk hii itasaidia kufukuza inzi,yani vyakula ukiwa unakula unakutana na vipande vya mkaa, vijiti, michanga ndo hatari.
NB: Tupike tukiwa tunathamini na kujali wanaokuja kula, watoto, waume, wazazi, ndugu, na sisi wenyewe.Na wale wenye tabia ya kulamba mwiko eti unaonja, ni uchafu weka katika kiganja onja na si zaidi ya mara 2.Please usipende kuonja hadi unashibia jikoni.
Asanteni.