Usafiri kutokea Dar es Salaam kwenda kisiwa cha Comoro

CrescentTz

Member
Joined
Aug 2, 2019
Posts
5
Reaction score
0
Naomba kuelekezwa jinsi ya kufika kisiwa cha Comoro ukiachana na usafiri wa angani(Ndege)
 
Mkuu kama ni kuhusu Comoro si vibaya uka share na wadau wengine wajue, ila kama ni mambo binafsi basi kheri
Kuna jamaa anafanya biashara ya kusafirisha vitu huko comoro, hutumia meli badala ya ndege sababu husafirisha mizigo mingi.

Nilichofanya ni kumpatia mleta mada number ya huyo jamaa. Ampigie tu hata amuulize usafiri wa meli ukoje, tiketi wanakatia wapi, nauli kiasi gani, wanakaa majini siku ngapi, etc.

Isingekua sahihi kuiweka number ya mtu hadharani. Maana hiyo number inaweza kutumika ndivyo sivyo mimi nikawa ndio sababu.
 
Naomba kuelekezwa jinsi ya kufika kisiwa cha comoro ukiachana na usafir wa angan(Ndege)
Usafiri wa kwenda Comoro kama ni tofauti na ndege mkuu inabidi uende mpaka Mtwara, kule ukifika nenda mpaka maeneo ya Pwani utakuta kuna mashua ambazo huwa zinabeba bidhaa mbali mbali kwenda Comoro. Ila jiandae kisaikolojia maana utatumia siku tatu hadi nne kupita deep-sea mpaka ufike. Kwa taarifa fupi tu ukiweza kufika fursa ni nyingi sana mkuu. Nakutakia kila la heri.
 
 
 
Mkuu umesomeka vilivyo. Natumai mleta mada akiwasiliana na jamaa ataleta mrejesho
 
Mkuu ni vyema ungemjuza hapa ili na wengine tufaidike na jibu lako.
Nimempa tu Number ya jamaa anaefanya hizo biashara za Kule, wala sio kwamba mie nafahamu Mkuu. Sasa haikuwa poa kuweka number hapa hadharani.
 
Ungejibu tu kua huelewi isipokua una mtu mwenye kujua namna ya kufika huko na mhitaji kama atataka namba ya huyo mtu basi aje inbox, kusema tu mara moja kwamba njoo huku inaleta harufu ya utapeli ambayo watu wote tutaona hivyo.
 
Ungejibu tu kua huelewi isipokua una mtu mwenye kujua namna ya kufika huko na mhitaji kama atataka namba ya huyo mtu basi aje inbox,kusema tu mala moja kwamba njoo huku inaleta harufu ya utapeli ambayo watu wote tutaona hivyo
Sio issue Sana,
Hata kuwaita watu inbox waje uwape number binafsi ya mtu nayo inaweza kua sio muafaka Sana, watu wanaweza tu kuja ukawapa namba za hawako serious au matapeli vilevile. .

Nimeshampatia number,
Labda akirudi hewani ataleta mrejesho yeye mwenyewe kama alifanikiwa kuongea nae ama alitapeliwa ama lah.
 
Hahaha duh mashua si mchezo aisee, miaka ya nyuma kidogo nilienda Zanzibar kwa boti ya flying horse nilihisi kufa kufa. Mashua piga ua siendi afu siku tatu no way aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…