Nimewahi kusafiri Mara nyingi mno ktk route hiyo miaka ya nyuma, kutokana na uzoefu wangu naweza nikasema haya yafuatayo:
1. Route ya Dsm-Tunduma-Lusaka-Harare-Johannesburg: Route hii ni bora zaidi.
Siku za safari ni NNE(4), siku 1 ni ya kusafiri usiku na mchana hakuna kulala
Nauli(Viwango na Mapendekezo)
Dsm- Lusaka-Harare(moja KWA moja): Tshs 150,000/= hadi 160,000/=
Dsm-Lusaka:Tshs: 130,000/= hadi 140,000/=
Kampuni ya mabasi ni Taqwa ya Tz.
Tunduma/Nakonde boarder to Lusaka: Kwacha 300
NB: Nauli ya Dsm- Tunduma: not included here.
Makampuni ya Mabasi ni Power Tool, ya Zambia
2.Lusaka-Harare-Johannesburg route
NB: Nauli KWA route hii Unaweza ikawa KWA fedha za Zambia(Kwacha) au za Afrika Kusini(Rand): zingatia sana jambo hili.
Ushauri wa bure: Kutokana na exchange rates ni vyema ukatumia Rand za South Africa, ukitumia Kwacha utalipa zaidi.
Nauli: Lsk-Harare-Joburg: Rand(ZAR) 900 hadi ZAR 1000
Kampuni zipo nyingi za Mabasi, lakini ilivyo bora Zaidi ni
ACK Logistics Company Ltd, kampuni ya Zambia
(the best customer care inside, and the highest quality buses in Zambia) with toilets inside.
NB: tembelea website yao KWA ratiba za safari
Harare- Johannesburg route
Nauli ni kwa Rands (ZAR)
Bei zinatofautiana kulingana na ubora wa Mabasi na huduma
Luxury buses
Nauli ni ZAR 350 hadi ZAR 500
Makampuni ya buses: CitiLiner, Eagle Liner, Sky Liner, Trans Lux, etc
NB: No toilets inside
Super Luxury Buses:
Makampuni ya Mabasi ni:
Greyhound na Intercape, yote ya Afrika Kusini.
The highest and the best customer care inside, the safety is guaranteed, toilet inside,
Nauli ni kuanzia Rands (ZAR) 600 na kuendelea, nauli inaongezeka kadiri ya muda wa safari unavyokaribia, ukikata ticket mapema utalipa kidogo kama ilivyo ktk usafiri wa ndege.
NB: Safari zote kutoka Harare to Jo'burg zinaanza SAA 1:00 jioni
They are very strictly about time like an airplane flights
Tahadhari: Usipitie nchi ya Msumbiji, Maaskari Polisi na Maafisa Uhamiaji wa Msumbiji ni Wasumbufu sana tena wana roho mbaya sana, wanapenda sana rushwa, unless kama una Passport ya Kidiplomasia au Una Kitambulisho cha Kazi cha Mashirika ya Kimataifa eg UN.Vile vile, hawako friendly na barabara zao ni mbaya sana.Japokuwa Mimi sijawahi kuwa muhanga wa masaibu hayo ktk safari zangu zote, lakini nimekuwa nikiwashuhudia Watanzania mwenzangu wakipata misukosuko ktk safari zao.
Pia, hawajui kuongea Kiingereza, wala Kiswahili isipokuwa Kireno tu.
Ukiwa na hoja nyingine yoyote, au ukitaka maelezo zaidi hata ukitaka maelezo kuhusiana na usafiri wa ndege kwa route hiyo, usisite kuwasilisha hoja zako kwangu.
Maelezo yangu nafikiri yatakusaidia KWA kiasi Fulani ktk mipango yako, nakutakia safari njema