Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yaani inabaki story kwa kweli.
Halafu unajua Mtwara sio kubwa kiviile enzi hizo, basi ukifanya jambo, unafahamika haraka
Vile nijuavyo ni mabasi ya somebody JOEL MABIBA from Mbeya!Kweni mabasi ya JM luxury Coach ni ya Kikwete?
kama ni Barabara tunajua kuwa zote zimejengwa na kodi ya wanainchi ile ambayo hubaki baada ya kuchakachuliwa kwa saana na hawa mafisadi wa CCM
Kumbe wengi humu mlipita Mtwara Girls..aisee, nimewapenda bureeee
Kwa kweli Madam B Mtwara unaifaham vizuri. Vipi hivi karibuni ushawahi kutembelea tena. Kuko vizuri sana kwa sasa! Ila nadhan kwa miaka inayotajwa nadhan mimi nilishamaliza kitambo kidogo sekondari miaka ile ya 97. Wakat ule Mtwara Tech nilikosoma madem hamna, munasubiri hadi.siku ya Disco munaruhusiwa kuondoa stress kwenda kucheza na Mtwara Girls. Wakati ule Manispaa ya Mtwara sekondari ni tatu tu yaani Mtwara Tech, mahasim wetu Sabasaba na Mtwara Girls. Ilikuwa bonge la raha tunafanya michezo pale TTC!
Miaka ile sisi tunasoma primary ulikuwa ukivuka Magomeni ni pori, Kanisa la Magomeni lilikuwa peke yake ni miembe tu, maembe unapiga mateke tu. Kutoka kanisa ni pori hadi pale Kijiji cha Ufukoni( Ufukweni kwa Kiswahili kilichozoeleka) kutoka pale ni pori hadi ufike Mikindani. Kutoka Mikindan ni pori hadi Mpapura yaani pale Msijute ambapo leo kuna mji na bar ile ya Mr Kweka ni.msitu mtupu. Ama kwa hakika mambo yanabadilika.
Leo hii kutoka mjini hadi Mikindani kilometa 12 ni mji mtupu na pia Mikindani hadi Msijute kilometa 7 hadi ulipo mji kinapojengwa kiwanda cha Alhaj Aliko Dangote ni almost mji tu! Ama kwa hakika Mtwara Kumekucha- KUCHELE!
Ha ha haaa,,,,,najaribu kuvuta picha wakati unatembeza ubabe na mikogo yakischana af,, wapambe wakumwaga ,,,,,daah,,,Maisha haya watu wanatoka mbali sana,,,! Kwa fulsa zilizopo Mtwara miaka michache ijayo kutakuwa km Mwanza manake Mwanza kwa sasa haina tofauti na DAR,, kumekucha kweli kweli
Wengi sana nimemsikia na madame B, kasema Alihamia.
Viwanja vimepanda bei mdau tena sana! Hiyo nyanda ya juu kusini unayoisema ni ipi tusiyoijua? Eneo ambalo ni prime ni jiji la Mbeya hasa kule forest. Kiwanja Mtwara eneo la beach kule Shangani kimeuzwa 1bn/-, pale Mnarani kiwanja kiliuzwa 400m/-. Ni mkoa gani wa Tanzania ukiondoa Dar hasa Kariakoo na kule kwa washua Mikocheni au Masaki nk kiwanja kitauzwa 1bn? Kwa anaepafaham vizuri Mtwara pale karibu na Jeshini round about ya kanisa la biblia kuna kiuzio fulani cha garage ya Mpemba mmoja hivi nadhan anaitwa Abdu Swamad, Oilcom walitaka wanunue kwa 200m/- akakataa!
Hivyo viwanja vimepanda bei. Kule Msijute ndo viwanja bei hiyo million10, lakini pale town uwe na million20-30, ambayo ni bei ya kawaida hata hapa Dar utapata kiwanja kwa bei ya 10-30m/- kule Kinyerezi, Kitunda, Kongowe, Kigamboni nk. Kusema nyanda ya juu kusini kama Njombe, Songea, Iringa na Rukwa kwamba zinaweza ku compete na Mtwara sidhani, tena vimeshuka kidogo mara baada ya zile rapsha, vinginevyo bei ilikuwa ni ghali sana.
Yaani ni full kupigana na watoto wa DSA.
Ila Mtwagiseco sitapasahau,
eti tulikuwa tunawavizia wanafunzi wanaosoma Naliendele halafu tunarushiana mawe kule mikoroshoni....uwanafunzi bhana, tunakuwa kama tumedata
Andrea Mturi ni mchoraji mzuri sana huyu jamaa,baadae aka okoka baada ya dada yao kufariki na kuwahusia waokoke,wakati huo niko Mtwara tulikua tunapiga sana nondo pale kwa mzee nani sijui jina lime nitoka kwa kina ras bano ligula pale.
we unapajua mtwara tena pale mnarani yule mzee mil400mwenyewe hakutaka ila wanawe ndo wakakomalia mpunga ukaingizwa benki
pale kanisa la biblia upande upi wa abdu swamadu?pale kwenye migahawa na kimsikiti k unaelekea mkoani?pembeni kuna gereji ya ng'itu?
au km unaelekea mnarani?
ila bado viwanja baadhi vipo vya bei ya kawaida
jamaa aliyebugi wa blantyre kuuza mil800 yaani yule ndo baas tena
Kwa Abd swamad pale mdau. Sasa si utaona pale Blantyre million800 je kwa mikoa mingi huwez kupata hizo! Mtwara Kuchele
andrew ana kaka ake mturi anakaa coco beach anakodishaga mziki mi nilikua nakaa hapa maeneo ya half lonron nyuma ya indian cotaz pale mturi namkubali sana hiyo kampuni yake ya uchoraji iko maeneo ya nangwanda
yaani mtwara rahaa bbaah
Yule dogo blazameni flani hivi anaitwa mshamu nayopa yupo?
Dah! Afadhali kuendelee maana kuna walozamia mikoa mingine na wamepasahau nyumbani kabisa wala hawatak kurud. Mosh wapo weng
simfahamu ila hilo jina la nayopa nilikua naliskiaskia au mpaka ningemuona
Hahahahah.....yaano nina uhakika kwa mtu aliyekuwa humu kama alikuwa Mtwara miaka hiyo, nikimtajia jina langu atanijua maana ile ishu ya kumteka mwenzetu tulitembezwa karibu ofisi zote za umma.
Ila watu tunatoka mbali jama
Mrembo by Nature mie wakati nasoma nilikuwa mtata sana, ....
Kisanga ambacho nakikumbuka mpaka leo ni pale nilipopewa sansipeshen, kwa kosa la kumvunja miguu head girl.
Basi tulivyomaliza kifungo wakati wa kurudi si unakuja na mzazi wako,...baba alikuwa hajui kama nilipewa adhabu maana home sikwenda wala nini, niliishia ghetto kwa rafiki zangu.
Nilichofanya, nikamtafuta konda wa bus la Wifi nae alikuwa anaitwa Omary 'toz wa liwale'...nikajifanya ndie mzazi wangu.
.....hahhahah, Mungu anaumbua sana jamani, ile siku ya kurudi shule huku niko na Omary, kumbe baba nae kaja kunitembelea.....hahahahaha, ilikuwa patashika.
Tulicharazwa mikwaju mimi na Omary wangu, sitasahau.
Ila nilisikia Omary alishakufa 2012(r.i.p).
Maisha ya shule, kama tumevutishwa bhangi
Haha haha haha haha haha eti konda wa wifi nae kochi watu mlikuwa mmepinda hadi unamvunja mtu mguu (nguu)? Watu kwa masoo shule ni sheedah. Shuleni kwetu wapo walioiba mchele wa shule km gunia zima stoo kila j2 wakawa wanajipikia wali na mbogamboga wanakula na demu zao. Siku imesanuka walipigwa Kama wameua vile.