Chinga One
JF-Expert Member
- May 7, 2013
- 11,469
- 12,391
Vigaeni sasa pamebomolewa kweupee ule upande ws rahaleo sekondari ndio nasikia wanajenga Bot
RIP mzee fimbo!!--James ni mwanangu pia, unamfahamu Sunday Matembo? Mzee fimbo alianguka kanisani jumapili ndo kifo chake kilipoanzia...hahaa Azizi Mwanga aka Kagunga...nimekutana nae 1 month back...full kiteta!!
kitata=kigugumizi
daah hilo neno kwente red ume nikumbusha mbali sana tulikua tunasema mtu mwenye kitata mfunikie ungo chini kudadeki haongei kabisa.
km sikosei ni mji mwema huko
Sizinga huyo jamaa matembo ulisoma nae mtwara tech nakumbuka aluikuaga mlokole baada ya kuona ulokole na shule haviendani akaanza kuwa msela wa kufa mtu.
Aaah ok, nako kumbe kuna Mji Mwema? Mtwara ina mitaa na vitongoji vingi vyenye majina yanayofanana na Dar. Kwa mfano Tandika, Kisutu, Magomeni, Mbez, Mji Mwema!
Sasa siku walipokuwa wanabomoa zile nyumba aisee, matunguri tu ya kufa mtu...yaani uchawi uchawi kwa kwenda mbele.looh vile vijumba vya vigaeni vilikua vidogo kama kiberiti ila vinameza watu kibao halafu watu walio kua wanakaa kwenye zile nyumba wanajua kuzaana hao balaa vidukulu kibaoo!
Alimaliza 2001....Sorry, huyo Matembo ni miaka gani? Maana ikitajwa Mtwara Tech, nami nimo! Miaka ya 1997/98!
Alimaliza 2001....
Hahaha ulikuwa unakaa kota za vigae?
sio za vigae zile zngine za bod ya korosho, mitaa ya kwa luca, nandonde
Ilishakufa...we ulisoma na akina dovick eeh?elezian, anord...hahaaaKwa waliosoma Mtwara Tech, kuna sehem moja inaitwa Maibras, ilikuwa tunatoroka kwenda kuangalia Movie enzi hizo. Sijui bado ipo au ilishakufa.
Aisee mekuu.........tufanye na sisi tukatembelee Ntwara.......nilidhani ni sisi tu tunajua lakshari.........mbutananga........uwiiiii........
oooooooh!.. Chinga One vp tena,mbona wamvutia chobingo huyo mtoto?!!
Mrembo by Nature kama vp twenzetu tukawachungulie!
Kwa waliosoma Mtwara Tech, kuna sehem moja inaitwa Maibras, ilikuwa tunatoroka kwenda kuangalia Movie enzi hizo. Sijui bado ipo au ilishakufa.
Ni kwa mara kwanza kusafiri na basi ambalo ni luxury kutokea Dar kwenda mkoa ule ambao miaka ya nyuma inasemekana ni mkoa uliosahaulika na ni sehemu ya adhabu kwa wafanyakazi wa serikali hii ya bongo.
Kilichonikosha roho ni kuona basi hili likitoa huduma ambayo tulizoea kuziona kwenye njia za mikoa ile ya ukanda wa kaskazini, mwanzo kabisa wa safari wahudumu hujitambulisha kwa abiria wao, then kuwahabarisha utaratibu wa safari abiria wote kuhusu kufunga mkanda kwa usalama wetu, kutoa mifuko ya kuweka uchafu,utaratibu wa kuongea na muhudumu bila kubugudhi abiria mwezako, utaratibu wa kushuka kwenye gari,vinywaji baridi vya Azam. mwisho kumtanguliza Mungu kwenye safari.
Sasa kutokana hali hiyo nikakumbuka safari yangu ya 1995 kutoka huko Kusini kuja Dar ambao tulisafiri na lory kwa siku sita, usafiri mwingine ilikuwa meli siku mbili majini, duh Kusini tumetoka mbali.
nauli walikutoza shilingi ngapi mkuu wiki ijayo nataka kwenda huko