Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Usafiri wa ungo upo wa aina nyingi, upo usafiri wa ungo unaotumia wanyama, upo usafiri wa kutumia fagio, upo usafiri wa kutumia fimbo, upo usafiri wa kutumia ungo. Wachawi wote wana roho ya uchawi, roho ya uchawi ni roho inayokufanya uweze kupita eneo ngumu na kutokeza upande wa pili, kwa mfano
wachawi wanapowanga usiku roho hizi huwafanya kuingia katika nyumba yoyote na kuwafanyia uchawi usiku watu waliolala ndani ya nyumba hizo bila ya kuonekana. Isipokuwa nyumba za walokole haziingiliki kabisa. Roho za uchawi zinawawezesha wachawi kujibadilisha maumbo yao, kutoka maumbo ya kibinadamu na kugeuka kuwa paka, panya, kunguru n.k.
1. Usafiri wa UNGO
Picha ya wachawi walio dondoka huko mkoani Mwanza. Ungo uliokuwa ukitumiwa na wachawi hawa, ulizidiwa nguvu baada ya wachawi kupita katika anga ambalo chini yake kulikuwa kanisa la kiroho. Wachawi hawa walitumwa kutoka mkoani Kigoma, kwenda mkoani Mwanza kuchukua roho za watu wawili. Wachawi hawa walikuwa wamepewa maagizo na mkuu wa wachawi katika madhabau yao ya kichawi.
Askari polisi na watu mbalimbali wakiwashangaa wachawi hawa walio anguka na ungo wao wa kichawi katika eneo la Butimba jijini Mwanza. Wanapotaka kusafiri anakuwa na vifaa vyake vya kichawi, kisha huomba dua akinuizia majini yampeleke sehemu fulani, roho yake ya uchawi na majini humuinua juu angani kwa kasi hadi eneo alilokusudia. Usafiri wa aina hii ni hatari kwani unaweza kutunguliwa kirahizi ukiwa angani.
2. USAFIRI WA KUTUMIA WANYAMA KAMA FISI.
Usafiri wa kutumia wanyama kama fisi, hutumika kwa nchi kavu tu, hawawezi kuvuka bahari kwenda visiwani au nchi za mbali. Fisi ni mnyama anayetumiwa sana na wachawi wa nchi katika usafiri. Usafiri huu hutumika katika maeneo ya nchi kavu tu, hauvuki bahari.
Uchawi wa kusafiri na fisi, unatumiwa sana na wachawi waliopo katika mikoa ya kanda ya ziwa , Mwanza, Shinyanga na Tabora, pamoja na mikoa ya Kigoma, Dodoma, na Singida. Katika makala inayo fuata nitawafahamisha kwanini wachawi wa maeneo tajwa hapo juu hupenda kutumia usafiri wa fisi.
3. USAFIRI WA KUTUMIA FIMBO
Usafiri wa kasi sana ni wa kutumia fimbo, kabla ya kuanza safari, unaomba dua ya manuizo na kukanyanga incha moja ya fimbo, roho ya uchawi na majini hukuinua juu angani, kama unataka kwenda Nigeria kutoka Dar, utaonyeshwa njia yote ilivyo, kama kuna hatari yoyote huonekana, na inabidi uhairishe safari,
kama njia ni nyeupe, unatakiwa ukanyage incha ya pili ya fimbo, na safari huanza kwa kasi ya sauti. Kwa sababu safari ni ya kasi sana na upepo ni mkali sana, kiasi kuwa huwezi kufika ukiwa hai, majini huchomoa roho yako ndani ya mwili wako na roho kukutangulia mbele, mwili wako huikimbiza roho yako ukiwa katika hali ya
umauti, unaweza kutumia sekunde 10 kufika Nigeria, lakini ni usafiri wa hatari kuliko zingine, usafiri huu hujulikana kama usafiri wa kujichinja. Mfano wa picha ya mchawi wa kizungu akisafiri kwa kutumia fimbo.
3. UCHAWI WA KUSAFIRI KWA UFAGIO.
Uchawi huu hutumiwa sana na wachawi waliopo katika nchi ya Romania na Ulaya na Marekani yote kwa ujumla. Barani Afrika, uchawi huu hutumiwa zaidi na wachawi waliopo katika nchi ya Swaziland. Picha ya mfano wa mchawi wa kizungu akisafiri kichawi kwa kutumia ufagio. Usafiri huu ni maarufu sana miongoni mwa wachawi waliopo Ulaya na Marekani na katika nchi ya Swaziland.
Uchawi huu ulianza kutumika katika nchi ya Romania iliyopo Ulaya Mashariki miongo mingi iliyopita. Katika makala yajayo nitaeleza kuhusu usafiri wa fisi. Bunge La Mtandao Usafiri wa ungo upo wa aina nyingi, upo usafiri wa ungo unaotumia wanyama, upo usafiri wa kutumia fagio, upo usafiri wa kutumia fimbo, upo usafiri wa kutumia ungo.
Wachawi wote wana roho ya uchawi, roho ya uchawi ni roho inayokufanya uweze kupita eneo ngumu na kutokeza upande wa pili, kwa mfano wachawi wanapowanga usiku roho hizi huwafanya kuingia katika nyumba yoyote na kuwafanyia uchawi usiku watu waliolala ndani ya nyumba hizo bila ya kuonekana. Isipokuwa
nyumba za walokole haziingiliki kabisa. Roho za uchawi zinawawezesha wachawi kujibadilisha maumbo yao, kutoka maumbo ya kibinadamu na kugeuka kuwa paka, panya, kunguru n.k.
Chanzo: MziziMkavu