Usafiri wa level seat lazima uratibiwe

Usafiri wa level seat lazima uratibiwe

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Usafiri wa level siti ni mzuri sana katika kupambana na magonjwa Kama COVID-19, TB, surua, mafua, upele, fungus yanayoenea kwa njia ya hewa na kugusana, lakini yafuatayo lazima yafanyike kwenye Usafiri huu ili usilete usumbufu:

1. Nauli ya kituo hadi kituo iwe 1000. Sh. 400, 500 au 600 hazitoshi kiuhalisia hasa kwa level siti.
2. Mabasi yapangiwe ratiba za kupita vituoni.
3. Mabasi yasisubiri siti zote zijae kwenye kituo kimoja Cha mwisho maana abiria wengi wako vituo vya njiani.
4. Traffic waache kukamata mabasi kipindi Cha Asubuhi sana hadi saa 4 asubuhi kupunguza usumbufu kwa abiria
5. Mabasi ya Usafiri wa umma yapewe kipaumbele barabarani, vituo vya mafuta, mataa ya barabarani.
6. Mabasi ya Usafiri wa umma yapunguziwe tozo za Kodi mbalimbali.
 
Nauli iwe 1000! Acha tamaa ya hela Corona itaisha na hesabu yenu itakaa sawa.

Hiyo 1000 unadhani ni nyongo kila mtu anayo.
 
Kwahiyo ww unaona ni sawa kwa basi la watu 36 kubeba abiria kutoka Mbagala hadi Kawe kwa sh. 600 level siti. Mara nyingi abiria wanaopandia kituo Cha kwanza huwa wanakwenda mwisho au kituo kimoja kabla ya kituo Cha mwisho wa basi. Hii inasababisha abiria wengi wa njiani waachwe maana gari imejaa abiria wa Mbagala-Kawe/Makumbusho kwa sh. 600 @. Hii haiwezi kulipa hesabu ya tajiri, mafuta, hela ya dereva, posho ya kondacta, spea, services, bima na Kodi mbalimbali
 
Usinikaripie kama mimi ndiye nimeleta Corona. Kama gari yako haipati hesabu paki ndani uache kuongea kwa kutumia ashiki za mapenzi.
 
Kama haiwalipi si wakapack tu gari zao
Hakuna anaewalazimisha kua barabarani
Ss hv bajaji mpaka posta bodaboda zinajiachia bei cheeee
 
Mkuu Bajaj na Pikipiki Ni Bei Chee?

Sent using Jamii Forums mobile app
Yes cheeee tusiwe wanafki mfano steshen ilikua wanaringa nauli buku3 kuanzia katikati hapo mivinje au bandari kukiwa na foleni ila ss hv ni elfu2 uwe aziz ali, tandika au mtongani bajaji buku huoni unafuu

Sent from my SM-G988 using Tapatalk
 
Tshs 1000? Hivi unajua kwamba kuna mtu mpaka kufika kazini anapanda magari mawili? So kwenda na kurudi Tshs 4000? Hajanywa chain wala hajala mchana? Kwa uchumi huu huu na kipato hiki hiki? Bila shaka utakuwa mmiliki wa daladala!

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ungekuwa unamiliki hizo daladala ungekubali nauli ilipwe 400??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una ata ABC za uchumi kweli..?? huwezi kumfikiria abiria anayeshuka kituo kimoja na seat ikauzwa mara 2,3 mpaka 4.
Usafiri wa level siti ni mzuri sana katika kupambana na magonjwa Kama COVID-19, TB, surua, mafua, upele, fungus yanayoenea kwa njia ya hewa na kugusana, lakini yafuatayo lazima yafanyike kwenye Usafiri huu ili usilete usumbufu:

1. Nauli ya kituo hadi kituo iwe 1000. Sh. 400, 500 au 600 hazitoshi kiuhalisia hasa kwa level siti.
2. Mabasi yapangiwe ratiba za kupita vituoni.
3. Mabasi yasisubiri siti zote zijae kwenye kituo kimoja Cha mwisho maana abiria wengi wako vituo vya njiani.
4. Traffic waache kukamata mabasi kipindi Cha Asubuhi sana hadi saa 4 asubuhi kupunguza usumbufu kwa abiria
5. Mabasi ya Usafiri wa umma yapewe kipaumbele barabarani, vituo vya mafuta, mataa ya barabarani.
6. Mabasi ya Usafiri wa umma yapunguziwe tozo za Kodi mbalimbali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una ata ABC za uchumi kweli..?? huwezi kumfikiria abiria anayeshuka kituo kimoja na seat ikauzwa mara 2,3 mpaka 4.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nenda kafanye utafiti kwenye daladala za Makumbusho-Posta au Makumbusho-Gongo la mboto level seat ili uone ni percent ngapi ya siti za ngari zinazouzwa mara 1, 2, 3 na 4 hadi linafika posta kituo Cha mwisho halafu ndiyo uje uchangie huu uzi
 
Back
Top Bottom