Usafiri wa Mwanza to Dar Jioni hii

Usafiri wa Mwanza to Dar Jioni hii

JF Member

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2014
Posts
7,914
Reaction score
10,793
Msaada Kama Kuna mtu yuko Mwanza anakuja Dar jioni hii kwa gari nijulishe . Kuna ndugu zangu wanatakiwa Dar kesho asubuhi.
 
Inawezekana kweli kufika dar asubuhi wakitoka mwanza jioni?
Maybe..
 
Nakushauri wasubirie Basi kesho asubuhi waanze safari, hata kama ni dharura kiasi gani, bora wasubiri tu Kesho siyo mbali.
 
Waambie wawe wavumilivu, Jua likipoa gari ni nyingi jioni.
 
Wakae kwa juu ya stand hapo panaitwa Kumalija hotel,kuna private car zinapitia watu hapo nyingi tu kuelekea Nzega,Singida mpaka Dom..waunge unge wanaweza kufika hata saa kumi za alfajiri,inawezekana waambie wakae kwa juu ya stand hapo barabara kuu
 
Wasogee mpaka Tinde ni rahisi pale'kuunganisha hata bus toka karagwe.
Kwenye mida ya saa mbili ivi ipo Taqwa toka Kampara
Tinde pale iwapitie .....Dar ni kati ya 3/4. Asubuhi hiyo
 
Past No.12 ndiyo inafaa kufanyia kazi.

Ila watafika Dar majira ya saa 4-5 asubuhi.
 
Back
Top Bottom