A
Anonymous
Guest
Tunaomba msaada wa kuboreshewa usafiri kati ya Loliondo na Arusha, magari yanayotoa huduma katika njia hii mengi ni mabovu na yanajaa kupita kiasi, mara tatu au nne ya uwezo wake, kutokana na kukosekana kwa udhibiti wa kutosha na ukosefu wa kampuni au mabasi mengine ya kutoa huduma.
Pia, wasafiri hatuna haki wala huduma zinazostahili; tunachukuliwa kana kwamba hatuna thamani, huku tukilazimika kuvumilia hali hiyo kwa kukosa usafiri mbadala.
Tunaomba mamlaka husika ziingilie kati na kudhibiti hali hii ili wananchi tusilazimike kulala njiani. Kwa mfano, jana basi lililoondoka saa 12 asubuhi lilitarajiwa kufika kati ya saa 7 na 8 alasiri, lakini lilifika saa 4 usiku baada ya kupiga simu kwa polisi wa Karatu na Arusha.