Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu watanzania,
Nimeona ni kama kiswahili kimekuwa kigumu kidogo kwetu watanzania japo ndio lugha yetu ya Taifa au huwa tunasoma taarifa kwa juu juu tu,kama kawaida yetu ya baadhi yetu watanzania ya uvivu wa kusoma habari au taarifa kwa umakini na utulivu.
Nimepita baadhi ya maeneo na kwenye kurasa mbalimbali za Mitandao za baadhi ya watu,nimeshangaa wakitumia maneno kuwa aliyekuwa msemaji mkuu wa serikali ametumbuliwa,jambo ambalo siyo kweli .
Ukweli na usahihi ni kuwa taarifa ya ikulu inasema kuwa AMEPANGIWA MAJUKUMU MENGINE,ambapo majukumu hayo bila shaka yatatangazwa muda wowote ule kwa umma, ili umma ujuwe mtumishi wao ni nani katika nafasi fulani.
Na unaweza kuta majukumu hayo mengine mapya yanaweza kuwa makubwa sana kuliko majukumu aliyokuwa nayo Awali. Kwa hiyo tuendelee kuwa na subira na utulivu kusubiri majukumu hayo mapya.
Japo ningependa pia kuwaambia ya kuwa siyo kila nafasi ya uteuzi huwa inatangazwa.yaani namaanisha zipo nafasi nyeti ambazo Rais anaweza mteua mtu au kumpangia mtu Majukumu na isitangazwe kwa watu,kutokana na unyeti wake. Ndio maana ukiwa kiongozi sehemu fulani unapaswa kuwa mtulivu na mwenye kudhibiti na kuchunga Ulimi wako. Siyo kuwa roporopo tu ,kwa kuwa ulimi wako unaweza kukukosesha baadhi ya nafasi kufikiriwa kupewa.hasa zinazohitaji usiri mkubwa wa taarifa na kila kitu ukionacho na kukifanya.
Kuelewa hiki nilichokizungumza basi angalia katika orodha hii ya majina hapo chini uende mpaka namba (IV )uone lugha iliyotumiwa katika taarifa ya Ikulu .
Kazi iendelee Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.