USAHIHI: Aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali amepangiwa Majukumu mengine na siyo kutumbuliwa. Anaweza kuwa na Majukumu makubwa kuliko ya Awali

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu watanzania,

Nimeona ni kama kiswahili kimekuwa kigumu kidogo kwetu watanzania japo ndio lugha yetu ya Taifa au huwa tunasoma taarifa kwa juu juu tu,kama kawaida yetu ya baadhi yetu watanzania ya uvivu wa kusoma habari au taarifa kwa umakini na utulivu.

Nimepita baadhi ya maeneo na kwenye kurasa mbalimbali za Mitandao za baadhi ya watu,nimeshangaa wakitumia maneno kuwa aliyekuwa msemaji mkuu wa serikali ametumbuliwa,jambo ambalo siyo kweli .

Ukweli na usahihi ni kuwa taarifa ya ikulu inasema kuwa AMEPANGIWA MAJUKUMU MENGINE,ambapo majukumu hayo bila shaka yatatangazwa muda wowote ule kwa umma, ili umma ujuwe mtumishi wao ni nani katika nafasi fulani.

Na unaweza kuta majukumu hayo mengine mapya yanaweza kuwa makubwa sana kuliko majukumu aliyokuwa nayo Awali. Kwa hiyo tuendelee kuwa na subira na utulivu kusubiri majukumu hayo mapya.

Japo ningependa pia kuwaambia ya kuwa siyo kila nafasi ya uteuzi huwa inatangazwa.yaani namaanisha zipo nafasi nyeti ambazo Rais anaweza mteua mtu au kumpangia mtu Majukumu na isitangazwe kwa watu,kutokana na unyeti wake. Ndio maana ukiwa kiongozi sehemu fulani unapaswa kuwa mtulivu na mwenye kudhibiti na kuchunga Ulimi wako. Siyo kuwa roporopo tu ,kwa kuwa ulimi wako unaweza kukukosesha baadhi ya nafasi kufikiriwa kupewa.hasa zinazohitaji usiri mkubwa wa taarifa na kila kitu ukionacho na kukifanya.

Kuelewa hiki nilichokizungumza basi angalia katika orodha hii ya majina hapo chini uende mpaka namba (IV )uone lugha iliyotumiwa katika taarifa ya Ikulu .
IMG-20240615-WA0007.jpg
IMG-20240615-WA0007.jpg

Kazi iendelee Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Ndugu zangu watanzania,

Nimeona ni kama kiswahili kimekuwa kigumu kidogo kwetu watanzania japo ndio lugha yetu ya Taifa au huwa tunasoma taarifa kwa juu juu tu,kama kawaida yetu ya baadhi yetu watanzania ya uvivu wa kusoma kwa uharaka habari au taarifa bila umakini na utulivu.

Nimepita baadhi ya maeneo na kwenye kurasa mbalimbali za Mitandao za baadhi ya watu,nimeshangaa wakitumia maneno kuwa aliyekuwa msemaji mkuu wa serikali ametumbuliwa,jambo ambalo siyo kweli .

Ukweli na usahihi ni kuwa taarifa ya ikulu inasema kuwa AMEPANGIWA MAJUKUMU MENGINE,ambapo majukumu hayo bila shaka yatatangazwa muda wowote ule kwa umma, ili umma ujuwe mtumishi wao ni nani katika nafasi fulani.

Na unaweza kuta majukumu hayo mengine mapya yanaweza kuwa makubwa sana kuliko majukumu aliyokuwa nayo Awali. Kwa hiyo tuendelee kuwa na subira na utulivu kusubiri majukumu hayo mapya.

Kuelewa hiki nilichokizungumza basi angalia katika orodha hii ya majina hapo chini uende mpaka namba (IV )uone lugha iliyotumiwa katika taarifa ya Ikulu .View attachment 3018479View attachment 3018479

Kazi iendelee Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
pamoja na hayo,
hii inadhihirisha kwamba chama na serikali ina hazina kubwa ya watu na viongozi makini, wenye sifa, vigezo, weledi na uadilifu katika utumishi wa umma ukilinganisha na na taasisi au vyama vya kisiasa vinavyojitutumuaga eti wana ndoto ya uongozi wa nchi hali yakua hata kwenye vyama vyao tu hawatoshi ni wachache mno...

waliopangiwa majukumu mengine ni miongoni mwa watu wa maana na muhimu,

na kwahivyo wakati mwingine hupitishwa kwanza kwenye mafunzo ya muda mfupi kuhusu kazi atakayopangiwa, kabla ya kuteuliwa na kupangiwa hayo majukumu mengine mapya....

kwa nyongeza,
ni vizuri ikafahamika hivyo pia 🐒
 
ni vizuri inafahamika hivyo pia 🐒
angalia chama kama CHADEMA kinaongozwa na mtu mmoja tu muda wote utafikiri wengine wote ni vipofu ndani ya Chama.
 
Wewe mwenyewe pia Kiswahili hapo kimekuchenga. Umeshindwa kubaini ngeli sahihi iliyotumika. Ukisema mtu "amepangiwa" ina maana hilo tukio limeshatokea tayari. Taarifa haisemi kuwa "atapangiwa majukumu mengine". Ila wewe unaaminisha watu wasubiri kuwa atapangiwa tena huenda pazuri zaidi. Hiyo 'atapangiwa' unaisema wewe ama ndio taarifa inavyosema? Kwamba ni wewe pekee ndio unayejua kusoma na wajua kiswahili zaidi? Acha hizo basi kaka.

Kwa lugha iliyotumika inamaan ameondoka hapo na amewekwa pengine ambapo sio lazima mimi na ww kujua. Kiongozi kupanga na kupangua safu yake ni haki yake na ni jambo la kawaida sana. Kwani kwa mfano hata angekuwa ametumbuliwa ajabu ingekuwa wapi? Kwani ndio angekuwa yeye wa kwanza? Tusimpangie rais, tumuache mama yetu mpendwa apige kazi yake na watu anaowaamini kwa uhuru.
 
Sie tunajua "ametumbuliwa" kwa sasa, by the way yule ni mwajiriwa wa serikali ajira yake inakoma mpaka pale atakapotimiza miaka 60. Hivyo mwajiriwa yoyote wa serikali akitumbuliwa lazima apangiwe majukumu mengine tofauti na wateule wa kisiasa kama ma-RC, DC etc wao wakitumbuliwa wanakaa benchi. Hivyo basi "mtumbuo" wa Mtumishi wa umma (mwajiriwa) sio sawa na "mtumbuo" wa Mtumishi wa umma (mwanasiasa).....mwajiriwa automatically atakuwa na majukumu mengine hata kama isipotangazwa.

Tuseme tu AMETUMBULIWA
 
Wewe mwenyewe pia Kiswahili hapo kimekuchenga. Umeshindwa kubaini ngeli sahihi iliyotumika. Ukisema mtu "amepangiwa" ina maana hilo tukio limeshatokea tayari. Taarifa haisemi kuwa "atapangiwa majukumu mengine". Ila wewe unaaminisha watu wasubiri kuwa atapangiwa tena huenda pazuri zaidi. Hiyo 'atapangiwa' unaisema wewe ama ndio taarifa inavyosema? Kwamba ni wewe pekee ndio unayejua kusoma na wajua kiswahili zaidi? Acha hizo basi kaka.

Kwa lugha iliyotumika inamaan ameondoka hapo na amewekwa pengine ambapo sio lazima mimi na ww kujua. Kiongozi kupanga na kupangua safu yake ni haki yake na ni jambo la kawaida sana. Kwani kwa mfano hata angekuwa ametumbuliwa ajabu ingekuwa wapi? Kwani ndio angekuwa yeye wa kwanza? Tusimpangie rais, tumuache mama yetu mpendwa apige kazi yake na watu anaowaamini kwa uhuru.
Kwa ufupi ni Kuwa AMEPANGIWA MAJUKUMU MENGINE. Umeelewa maana ya maneno hayo? Ni tofauti na maneno kuwa atapangiwa majukumu mengine.
 
Back
Top Bottom