USAHIHI: Aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali amepangiwa Majukumu mengine na siyo kutumbuliwa. Anaweza kuwa na Majukumu makubwa kuliko ya Awali

Haiondoi ukweli kuwa Ikulu kuna jambo kubwa linaendelea na mazonge zonge yameanzia kwenye mrejesho wa ziara ya Korea
 
Haiondoi ukweli kuwa Ikulu kuna jambo kubwa linaendelea na mazonge zonge yameanzia kwenye mrejesho wa ziara ya Korea
Mheshimiwa Rais anao uhuru na mamlaka ya kufanya mabadiliko ya watendaji serikalini kwa namna anayoona itachochea zaidi ufanisi serikalini katika kuwatumikia wananchi.ndio maana leo mtu anaweza tolewa huku na kupelekwa kule na wa kule akapelekwa kwingine au kupumzishwa kidogo kabla ya kurejeshwa tena baadaye.
 
Duh! Prof. Mkenda bado ana kazi kubwa sana kwenye mfumo wetu wa elimu, elimu sahihi ni ile itakayomuwezesha msomi kufikiri na kuchanganua mambo (criticle thinking). Haya yote ni matokeo ya Taasisi zetu za elimu ya juu kuingia kwenye mfumo wa siasa kwa kukubali kuwa matawi ya vyama vya siasa badala ya kunoa bongo za wasomi. Prof. Mukandala, Prof. Kabudi na wengine damu ya Taifa hili itawalilia daima, wametumbukiza wasomi shimoni kwa kuwafanya wakubali "kuwaabudu" wanasiasa
 
Wazee wa kujikomba aka vyawa
 
Hata RC wa SIMIYU atapangiwa majukumu mengine ni suala la muda tu kwa hawa watawala wa ccm
 
Ili huko wanakopelekwa wakaharibu tena zaidi kwasababu uhalisia ni kwamba hakuna binadamu anakubali makosa yake kirahisi na anapotolewa sehemu iliyokuwa na maslahi kwake/ hadhi ukampeleka sehemu ya chini/yenye hadhi ndogo kuliko alipokuwa utendaji wake utakuwa wa hovyo maradufu. Hii ni asili ya binadamu
 
Hata RC wa SIMIYU atapangiwa majukumu mengine ni suala la muda tu kwa hawa watawala wa ccm
Ndio anaweza kupangiwa ikiwa uchunguzi utabaini kuwa tuhuma zilikuwa ni za uongo na kutengenezeana ajali za kisiasa na kuchafuana kwa maslahi ya baadhi ya watu. Si unaona CHADEMA walikuwa wanamuimba hayati Edward lowassa kuwa ni fisadi lakini 2015 walimkaribisha na wakawa wanainama barabarani kupiga deki lami ili akipita matairi ya gari lake yasichafuke?
 
Cheo ni dhamana,ukiharibu lazima uwajibishwe.
 
Wazee wa kujikomba aka vyawa
hata iweje waTanzania lazima wakombolewe kwa hali na mali, dhidi ya malaghai ya kisiasa nchini yanayofadhiliwa na mabwenyenye ya magharibi....

na ni Faraja ya kipekee sana kwamba uelewa, ufahamu, Imani na matumaini ya waTanzania ni kwenye chama na serikali sikivu ya kizalendo, chini ya kiongozi makini, shupavu na madhubuti sana comrade Dr Samia Suluhu Hassan 🐒
 
Hata Mbowe tu anayo imani kubwa sana na Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan,kuwa ndio mtu na kiongozi pekee awezaye kuliongoza Taifa letu kwa Sasa na kuliletea maendeleo endelevu na yenye kugusa maisha ya watanzania.
 
Lukuvi alipangiwa kazi gani?
 
Chai
 
Lukuvi alipangiwa kazi gani?
Kwani huwa humuoni kwenye matukio mbalimbali muhimu akiwa na Mheshimiwa Rais? Hukumuona hata juzi tu hapa alipokuja mgombea Urais wa Msumbiji Kupitia FRELIMO? Hukumuona siku ile Mheshimiwa Rais amekutana na kuonana na Kardinali kule Tabora? Unafikiri anafanya nini?

Wewe endelea kupambana na CHADEMA yako inayoendelea kupukutika na kusambaratika. Ungekuwa na akili na unayekipenda chama chako na umoja wa chama usingeweza kuleta taarifa katika namna ambayo ulileta baada ya Mboya kushindwa uchaguzi.
 
Kutegemea kupiga fix JF bila shaka utakua ama huijui JF au huna Ubongo
 
Hiyo inajulikana bila hata maelezo haya mengi. Anaweza kuwa pia katumbuliwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…