Usahili Utumishi zitumike lugha zote

Usahili Utumishi zitumike lugha zote

Sawa Mkuu Nakubaliana Na Wewe kuwa tatizo ni walimu wanaotufundisha, wanatufundisha kiingereza Kiswahili aka kiswanglishi.

Lakini Pia ikumbukwe hao walimu wenyewe nao walikuwa wanafunzi walifundishwa na mfumo huo huo wa kiswanglishi kwahiyo ni kama Tu muendelezo wa walichofundishwa.

Ifike Mahali tukubaliane kitu kimoja kama tumeamua Kiswahili basi iwe Kiswahili kuanzia awali mpaka chuo kikuu
Kama ni kiingereza ni kiingereza mwanzo mwisho,

Kama ni kuwaandaa watu wajiajiri wenyewe basi tutengenezewe mazingira mazuri toka uku chini awali mavyuo ya UFUNDI stadi yawe ya kutosha n.k

Kuliko sasa hivi hatueleweki mfumo tunaoutumia unawaumiza Vijana wengi Sana mtaani ndo maana tatizo la ajira limekuwà KUBWA Sanaa
Inabidi Tueleweke tusiwe kama Chura,
Chura haeleweki kama amesimama au amekaa au amechuchumaa.
Tufanyeje tusonge mbele, binafsi sishabikii wanafunzi kusoma masomo Kwa lugha ya kiswahili Ili Hali soko la ajira linataka uwe unajua kiingereza kama lugha ya mawasiliano, kwasasa wazazi wanaojua duniani inaelekea wapi wanawapeleka watoto wao wakajifunze lugha zingine kubwa duniani, tukitaka kiswahili kiwe lugha ya kufundishia Hadi vyuo vikuu tunatengeneza daraja la watawala (watakaojua Kiinglish nalughazingine za kigeni)na watawaliwa(watakaokuwa wanajua kiswahili tu)
 
Safi Sana Mkuu
Umekuja Ninapopataka.
Nini Kifanyike Ni Hiki
Tunatakiwa tukae chini na kuupitia upya mfumo Wetu wa Elimu, Kama tumelitambua kuwa lugha ya kiingereza ndo lugha KUBWA ya mawasiliano na INA soko KUBWA kwenye upande wa ajira na Mambo mengine basi tunatakiwa kukitumia kiingereza kuanzia shule za awali mpaka chuo kikuu na kukipa nafasi KUBWA lugha ya kiingereza kwenye majukwaa mbalimbali hii itawajengea wengi huwezi wa kujiamini na Kuweza kujieleza vizuri sanaa linapokuja swala la kujieleza.
Lakini kama tutaamua kukiendeleza na kukidumisha Kiswahili chetu kiwe cha kimataifa basi na chenyewe hivyo hivyo
Kuanzia awali mpaka chuo ni Kiswahili Tu
Mwanzo mwisho mbona nchi kama China, Russia, Korea wameweza kutangaza lugha zao, why Sisi tushindwe.
Lengo ni lile lile tukipitia mfumo Wetu wa Elimu kuanzia awali mpaka chuo kikuu itawasaidia Vijana wengi kukabiliana na soko la sasa la ajira na kupata matokeo chanya.
 
Umesema kweli.

Kama tunasema wasomi wanatakiwa wawe wanakimudu kiingreza vizuri basi inabidi mfumo wetu wa elimu uwe unasapiti hilo, maana kuitumia tu kama lugha kwa level za sekondari na chuo haitoshi.

Ndio maana watu wanakosa kujiamini.
Ni kweli Yan
Mfumo Wetu Sio Rafiki
Hawaandai wasomi Kuweza kujiamini na kujieleza vizuri na Kwa ufasaha kwa lugha ya kiingereza mbele ya watu au MTU mmoja mmoja.
Hata pia kwenye jamii tunayoishi ukiwa unaongea lugha ya kiingereza utachekwa Sana na wenzako hasa ukikosea au utaonekana unajifanya unajua Sana Yan mzungu n.k
Hiyo pia inachangia MTU kujenga inferiority complex akate Tamaa kabisa ya kujifunza kiingereza.
 
Safi Sana Mkuu
Umekuja Ninapopataka.
Nini Kifanyike Ni Hiki
Tunatakiwa tukae chini na kuupitia upya mfumo Wetu wa Elimu, Kama tumelitambua kuwa lugha ya kiingereza ndo lugha KUBWA ya mawasiliano na INA soko KUBWA kwenye upande wa ajira na Mambo mengine basi tunatakiwa kukitumia kiingereza kuanzia shule za awali mpaka chuo kikuu na kukipa nafasi KUBWA lugha ya kiingereza kwenye majukwaa mbalimbali hii itawajengea wengi huwezi wa kujiamini na Kuweza kujieleza vizuri sanaa linapokuja swala la kujieleza.
Lakini kama tutaamua kukiendeleza na kukidumisha Kiswahili chetu kiwe cha kimataifa basi na chenyewe hivyo hivyo
Kuanzia awali mpaka chuo ni Kiswahili Tu
Mwanzo mwisho mbona nchi kama China, Russia, Korea wameweza kutangaza lugha zao, why Sisi tushindwe.
Lengo ni lile lile tukipitia mfumo Wetu wa Elimu kuanzia awali mpaka chuo kikuu itawasaidia Vijana wengi kukabiliana na soko la sasa la ajira na kupata matokeo chanya.
Tatizo wanaosimamia sera watoto wao hawasomi shule za Serikali, na wanashawishiwa na wanaharakati kama HAKI ELIMU kukiponda Kiinglish kuwa hakifai kufundishia kwasababu wanafunzi hawaelewi ila wao watoto wao Wanasoma shule za English medium, mwisho wa majority ya watanzania wanadaliwa kuwa tabaka la watawaliwa
 
Aliyesema shule za serikali zifundishe kwa Kiswahli darasa la kwanza hadi la saba ndio kayaleta haya...

Iltakiwa watu wasome kwa kingereza toka shule ya msingi afu kiswahili kiwe somo tu mana kinaongelewa mtaani tungejua tu..

Sema ndio hvo tena mtoa mada ni kukaza tu mana ukishavuka usahili unaeza kaa humo ofisini had unastaafu usiongee tena kingereza
 
Back
Top Bottom