USAID haiwezi kufutwa kwa Executive Orders; watetezi kwenda Mahakamani kuzuia uamuzi wa Donald Trump

Stuxnet

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2011
Posts
13,417
Reaction score
23,310
Hili ni kinyume cha sheria. Si Donald Trump wala Elon Musk anayo mamlaka ya kufuta USAID; ni Bunge (Congress) pekee linaloweza kufanya hivyo kwa kupitisha sheria.

Kesi za kisheria zinaendelea, ili kujaribu kuzuia hili.

JFK alitoa amri ya kiutendaji kuunda USAID, kisha baadaye Bunge lilipitisha sheria iliyoifanya USAID kuwa taasisi huru. Hivyo, kufuta USAID kungehitaji sheria ya Bunge (si amri ya kiutendaji).
Screenshot 2025-02-04 140755.png

Ikiwa Marekani itajiondoa katika kusaidia mataifa ya Afrika, kuna uwezekano mkubwa kwamba mataifa kama China na Urusi yataongeza ushawishi wao barani humo. Hii inaweza kubadili uwiano wa kisiasa na kiuchumi, huku mataifa ya Afrika yakigeukia nchi hizo kwa msaada wa maendeleo.

Kwa sasa, hatima ya USAID haijulikani. Wafuasi wa shirika hilo wanatoa wito kwa bunge la Marekani kuingilia kati ili kulinda programu zake, wakisisitiza kuwa misaada ya kimataifa ni muhimu si tu kwa masuala ya kibinadamu bali pia kwa maslahi ya kimkakati ya Marekani duniani
 
Russia iliwahi kumsaidia nani wakati hapa suala sio kutoa msaada wa AK 47 bali ni msaada wa kimaendeleo.

China naye hana cha msaada bali yeye ni kutoa mikopo umiza na ndio maana mataifa kama Kenya, Zambia, Sri Lanka ni vilio tu.
 
Mwaka juzi tu Urusi ametoka kusamehe deni la zaidi ya $bilion 20 kwa nchi za Afrika ,sasa sijui hizo hela zote walikopa kwa ajili ya Ak47?
Hata hivyo Urusi awasaidie kwani nyinyi hamna mikono ya kufanya kazi kujenga nchi zenu?
Yaani Urusi iwakamue kodi raia wake kwa ajili ya kuwahudumia nyinyi ,hali yakuwa nyinyi kodi zenu mnanunulia,magoli, ma v8 ya mabilion kila mwaka na kuiba kupeleka Uswizi?
Huo upumbavu Urusi hawezi ufanya maana alisha ufanya huko nyuma uka mgharimu na kusababisha soviet kuanguka.
 
Ikiwa Marekani itajiondoa katika kusaidia mataifa ya Afrika, kuna uwezekano mkubwa kwamba mataifa kama China na Urusi yataongeza ushawishi wao barani humo. Hii inaweza kubadili uwiano wa kisiasa na kiuchumi, huku mataifa ya Afrika yakigeukia nchi hizo kwa msaada wa maendeleo.

Kwa sasa, hatima ya USAID haijulikani. Wafuasi wa shirika hilo wanatoa wito kwa bunge la Marekani kuingilia kati ili kulinda programu zake, wakisisitiza kuwa misaada ya kimataifa ni muhimu si tu kwa masuala ya kibinadamu bali pia kwa maslahi ya kimkakati ya Marekani duniani
Ushawishi wa china na rusia utaongezeka barani africa kwa maana hao ndio watakaotoa hiyo misaada au vp? Fafanua kidogo
 
Hili ni kinyume cha sheria. Si Donald Trump wala Elon Musk anayo mamlaka ya kufuta USAID; ni Bunge (Congress) pekee linaloweza kufanya hivyo kwa kupitisha sheria.

Kesi za kisheria zinaendelea, ili kujaribu kuzuia hili.

JFK alitoa amri ya kiutendaji kuunda USAID, kisha baadaye Bunge lilipitisha sheria iliyoifanya USAID kuwa taasisi huru. Hivyo, kufuta USAID kungehitaji sheria ya Bunge (si amri ya kiutendaji).
Lakini Republicans wako wengi kwenye Congress na Sanete, wakienda huko pia watashinda na USAID itafutwa.
 
Mwaka juzi tu Urusi ametoka kusamehe deni la zaidi ya $bilion 20 kwa nchi za Afrika ,sasa sijui hizo hela zote walikopa kwa ajili ya Ak47?
Hata hivyo Urusi awasaidie kwani nyinyi hamna mikono ya kufanya kazi kujenga nchi zenu?
Yaani Urusi iwakamue kodi raia wake kwa ajili ya kuwahudumia nyinyi ,hali yakuwa nyinyi kodi zenu mnanunulia,magoli, ma v8 ya mabilion kila mwaka na kuiba kupeleka Uswizi?
Huo upumbavu Urusi hawezi ufanya maana alisha ufanya huko nyuma uka mgharimu na kusababisha soviet kuanguka.
Ni wakati mzuri kwa China kuongeza mizizi yake Afrika kwa kuwa hata viongozi wa Afrika wanaona impact kwenye miundombinu anayowajengea
 
Kwa yanayoendelea Sasa .. Ninaamini pasi na shaka jaribio la kumuua Trump lilipangwa kimataifa..
 
Ikiwa Marekani itajiondoa katika kusaidia mataifa ya Afrika, kuna uwezekano mkubwa kwamba mataifa kama China na Urusi yataongeza ushawishi wao barani humo. Hii inaweza kubadili uwiano wa kisiasa na kiuchumi, huku mataifa ya Afrika yakigeukia nchi hizo kwa msaada wa maendeleo.

Kwa sasa, hatima ya USAID haijulikani. Wafuasi wa shirika hilo wanatoa wito kwa bunge la Marekani kuingilia kati ili kulinda programu zake, wakisisitiza kuwa misaada ya kimataifa ni muhimu si tu kwa masuala ya kibinadamu bali pia kwa maslahi ya kimkakati ya Marekani duniani
Kiukweli hapa elon na trump wameyatimba.
Wanaenda kuacha mwanya mpana sana ambao China au Urusi wakiutumia watakua na influence kubwa sana na kucontrol resources za Africa
 
Back
Top Bottom