Usaili wa Kazi | Hadithi Fupi

Usaili wa Kazi | Hadithi Fupi

Abtali mwerevu

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2013
Posts
665
Reaction score
515
Usaili wa Kazi

Konradi Kitumbo alitembea barabarani akitangaza tangazo lake, “La mgambo likilia kuna habari…”

“Kuna jambo… Acha kuharibu maneno wewe!” Mpita njia alikosoa, Kitumbo akarudia, “Haya, la mgambo likilia kuna jambo…” akakohoa kidogo kisha akaendelea, “mwezi ujao kuna usaili wa kula mema ya kijiji. Kiingilio elimu yako, na umri usiozidi miaka 45, hatutaki wazee ebo! Anzeni kujiandaa, watakaopita watamshinda adui njaa!”

Vijana walichangamkia fursa, wakaanza maandalizi ili waweze kuyala hayo mema ya kijiji waliyoahidiwa. Tafiti zilipofanyika zikagundua kuwa, vijana laki mbili unusu walijindaa kwa nafasi za kula mema ya kijiji ambapo nafasi hizo zilikuwa alfu kumi unusu. Mchuano ulikua mkali kwelikweli.

Katika baa moja, mziki mororo ulipigwa, mwanaume mmoja akacheza kwa madoido huku akipuliza filimbi. “Acha ulofa, unatuumiza masikio bwege wee!” alilalamika mlevi aliyekerwa na tukio lile.

“Unanijua mi ni nani? Mimi ni Konradi Kitumbo, meneja mradi wa kula mema ya kijiji… tazama hapa,” anasema akitoa kitu mfukoni, “Tazama, huu ni mtihani wa usaili, unayaona maswali haya?”

Asalalaleee, Kitumbo alitembea na mtihani wa usaili mfukoni kwake, ukishangaa ya filauni utayaona ya Musa!

Basi katika kijiji kila kijana alionekana kujiandaa na mtihani. Wengine walisoma historia ya kijiji, wengine wakasoma sayansi ya kijiji, wengine wakasoma lugha ya kijiji na wengine wakajikita katika saikolojia ya kijiji, wapo pia waliojikita katika kusoma uchumi wa kijiji, basi kila mtu alijiandaa vyema ili ayale hayo mema ya kijiji.

Kitumbo alionekana katika chumba kimoja akiwa na kijana mmoja wa kiume na kijana mmoja wa kike, “Kipanga…” aliita Konradi akimtazama kijana wa kiume usoni kisha akaendelea, “Huyu ni shemeji yako, nimekuita hapa, ili tushirikiane kutafuta majibu ya mtihani huu mtakaoenda kufanya, nataka shemeji yako afaulu, changamoto yake ni moja, ana kichwa chepesi kama bata. Nataka wewe uelewe majibu na siku ya mtihani ujibu kama yalivyo halafu yeye atakaa pembeni yako, kazi yake ‘kukopi na kupesti’. sawasawa Bwana mdogo.”

“Sawa.”

“Akipita shemeji yako, na wewe si umepita? Haya jadilianeni na ujaze vyema majibu, huku mbele ni maswali na huku nyuma utaandika majibu utakayopata na hayo ndiyo yatatumika katika kusahihisha mtihani… jiandaeni vyema.”

Wakati Kitumbo anatoka alimuita Kipanga nje, “Dogo… fanya kazi niliyokupa tu, ukileta biashara zingine nakupoteza, nimewekeza hapo. Kwa heri.”

Tofauti ya Kitumbo na huyu mpenzi wake ilikuwa miaka hamsini na saba. Wakati Konradi ni mzee wa miaka 77, binti alikuwa na miaka ishirini na robo.

Hatimaye siku ya mtihani wa kuandika ilifika. Zaidi ya vijana laki mbili walijitokeza kuchuana kwa ajili ya nafasi alfu kumi unusu. Vijana waliambiwa kwamba, atakayepita katika mtihani wa kuandika, ataenda katika mtihani mwingine wa kujieleza kwa mdomo.

Kipanga alikaa na Zoazoa kipenzi cha Konradi. Naye Konradi akasimama mbele kuhutubia kabla mtihani haujaanza. “Jamani tunakwenda kuanza mtihani wetu, ficha kazi yako kwa sababu mtu anaweza akaangalizia kwako na akakupita wewe ukabaki. Watakaopata alama nzuri, wataenda katika mtihani wa pili wa kujieleza, watakaofaulu huko, wataingia katika kundi la wanakijiji wanaokula mema ya kijiji.

Mtihani ulipoanza Zoazoa alijaza kila kilichojazwa na Dogo. Kitumbo alikuwa mbele yao kuhakikisha alichoelekeza kinafanyika na alifurahishwa na namna vijana wake walivyofuata maelekezo.

Vijana wote walitoka katika mtihani wakisema ulikuwa mtihani mzuri unaoeleweka, kila kijana akawa na matumaini ya kuweza kufaulu mtihani ule.

Matokeo yalitoka, katika vijana laki mbili waliofanya, walichujwa na kubaki vijana elfu thelathini, elfu thelathini hawa walitakiwa kwenda katika mchujo mwingine ili wabaki alfu kumi unusu waliotakiwa.

Kipanga na binti Zoazoa waliinamisha vichwa vyao, wote hawakupita katika mchujo. Ati ilishangaza iliwezekanaje Kipanga asipite katika mtihani ambao majibu aliyaandaa yeye mwenyewe. Kingine kilichoshangaza, Zoazoa alijaza majibu kama yalivyokuwa kwa kipanga, lakini alama zao zilikuja tofauti. Kipanga alipata alama kumi na mbili. Zoazoa aliyeiga kwa Kipanga alipata ishirini na nne!

Wakati wakiendelea kutazamana kwa huzuni, mbele alitokea Konradi Kitumbo. Kavaa kaptura pana imeandikwa HAKI, imegoma kabisa kukaa vyema kiunoni kwa hivyo anafanya kuivutavuta. tumbo lake kubwa na shati alilovaa vikamfanya aonekane kama katuni ya Lodilofa, miguu myembaba ingeweza kudhaniwa ni kuni ziliingizwa humo ndani ya kaptura.

“Wewe kaa hapohapo, Zoazoa ongozana nami!” alisema Konradi akimshika mkono Zoazoa na kulekea naye alikokujua yeye. Kipanga akabaki peke yake.

“Wajinga wakubwa…” Alifoka Konradi Kitumbo mara tu alipoingia katika jengo lililoandikwa SEKRETARIATI YA ULAJI WA MEMA YA KIJIJI. Hakupoteza muda, akamkwida kijana mmoja aliyekuwa na kitambi kipya, “Haya niambie, mwanahizaya mkubwa, karatasi mlisahihisha hamkusahihisha… sema nisije nikakutoa roho.”

“Sijui…” alijibu kijana akihema kwa tabu, “habari hizi anazifahamu Makaku.”

Konradi akaongoza mbele katika chumba cha mikutano akiwa kamshika mkono binti Zoazoa, alipofika, aliwaona watu wengi wakiendelea na shughuli za kuandaa usaili wa mahojiano.

“Makaku…” aliita Konradi akimtazama Makaku, mwanaume mweusi tii aliyekuwa na kipara, wengi husema kichwa cha makaku hakikuwahi kuota nywele!

“Naam mkuu,” aliitika.

“Unajua kareti,” alipiga mkwara Konradi, akarusha teke juu, makende yakaonekana!

“Sistima, Krav Maga, Kungfu, Tai chi, Tae kwondo… za kichinachina huuu haaaa!” akimaliza mkwara wake, akamwelekea Makaku na kumkwinda shingo. “Sasa utanieleza karatasi mlisahihisha au kuna jambo mlifanya… bladi!”

“Kusema kweli…” alijitetea Makaku, “karatasi zilisahihishwa lakini si zote. Tulitumia kanuni moja, kwamba kama tunataka kupata watu alfu thelathini katika kuhudhuria mchujo, basi haina haja ya kusahihisha makaratasi laki mbili unusu, tulisahihisha karatasi alfu thelathini na saba tu, alfu thelathini wanaotakiwa tukawapata, waliobaki, tukawakadilia ili kuokoa muda na rasilimali za kijiji.”

“Wendawazimu!” alifoka Konradi Kitumbo, “mkamkadiria mpenzi wa maisha yangu, binti Zoazoa, wajinga wakubwa nyiee!” akatembea kwa mikogo mpaka katika sehemu ambapo hukaa mwenyekiti, akawasha kipaza sauti na kuanza kuhutubia.

“Sasa sikilizeni… kwa huruma tu, kila mmoja aandike majina sabini ya watu anaowataka wawe katika Ulaji wa kijiji. Nataka niwafundishe namna muda unavyookolewa.”

Haukupita muda, majina yakaletwa, kila mmoja kaandika majina ya watu sabini anaowataka, hata hivyo wapo wengine wengi walioleta zaidi ya idadi hiyo.

“Chapeni majina haya, hawa ndiyo wamepita na wanastahili kula mema ya kijiji, mchapaji hakikisha jina la Zoazoa linatokea katika kila ukurasa, usiliandike mara moja, narudia, hakikisha jina lake linatokea katika kila ukurasa.”

“Bwana mahesabu wa kijiji.” Aliita Konradi.

“Naam!”

“Idadi ya majina iliyoletwa zimebaki nafasi ngapi?”

“Zimebaki nafasi mbili mkuu.”

“Sawa, kesho yatangazeni majina ya watu hawa waliopata ulaji, halafu hizo nafasi mbili zilizobaki mtaendelea nazo kwa vijana waliopita. Hakikisheni mnatenda haki kwa kupitisha vijana waliobora tu, hiki kijiji chetu wote.”

“Sawa mkuu.”

“Sikiliza…” akimtazama mchapaji, “narudia, jina Zoazoa, lionekane katika kila ukurasa.

“Sawa mkuu.”

Ilikuwa asubuhi tulivu, binti Zoazoa amesimama mbele ya Konradi Kitumbo pembezoni mwa bustani ya maua. Zoazoa alishika kijiko na sahani, jina lake lilitangazwa kuwa miongoni mwa waliochaguliwa kula mema ya kijiji. Kwa mahaba akimkata jicho chokozi Konradi akasema,

“Asante mpenzi Konradi kwa kuniheshimisha na kunifanya nami niwe sehemu ya walaji mema ya kijiji. Kuanzia sasa mimi ni wako wa maisha. Nitakupa katika namna utakayo, ukitaka nichane msamba sawa, nibinuke sawa, niruke sarakasi sawa, hata ukitaka uingie wewe na viungo vyako, ingia mpenzi endapo utatosha.”

Konradi akatabasamu, akajihisi kijana, mapigo ya moyo yakamwenda mbio, mdomo ukashindwa kuficha siri, mate ya uchu yakamtoka!

MWISHO
#MwalimuMakoba
 
Kaka hongera sana kwa uandishi mzuri. Safi.
Umeakisi uhalisia kwa taswira ya kipekee. Nimefurahi kusoma.
 
Back
Top Bottom