MOSintel Inc
JF-Expert Member
- Mar 24, 2016
- 818
- 593
Habari wakuu,
Kwanza nitoe pongezi kwa wale wote waliochaguliwa kwa ajili ya usaili wa mahojiano utakaofanyika kuanzia tarehe 02 Mei hadi 14 Mei, 2025.
Na kwa wale wote walio na malalamiko tayari imetolewa nafasi ya kuwasilisha malalamiko Yao ili waweze kutendewa haki kama ilivyo kwa wale waliochaguliwa.
Naomba sasa nielekee katika kuwasilisha Hoja yangu.
Awali mchakato huu(usaili wa TRA) ulipoanza kulikuwa na utaratibu mzuri wa kufanyika kwa usaili kwani TRA iliweka vituo kikanda jambo ambalo lilirahisisha na kupunguza gharama kwa waombaji wa ajira, hasa gharama za usafiri.
Lakini jambo la kushangaza ni kwamba katika hatua inayofuata ya usaili wa mahojiano baada ya Ile ya usaili wa kuandika, TRA wamechagua vituo vya usaili kuwa sehemu moja ya Mkoa wa Dar es Salaam pekee jambo ambalo Nina uhakika litachangia kutohudhuria kwa baadhi ya wasailiwa kutokana na gharama kubwa za usafiri zilizopo kwa sasa .
Mfano, Watu wa Simiyu, Musoma na Mwanza waliofanya usaili Mwanza iliwapunguzia gharama kubwa za usafiri pamoja na muda na kutoa fursa kwa idadi kubwa ya wasailiwa kufika katika usaili. Sasa MTU aliyefaulu kuingia katika usaili wa mahojiano, atapaswa kuingia gharama zaidi ya mara 7 ili aweze kufanya usaili wa mahojiano.
Rai yangu kwa TRA ningewaomba angalau kufikiria juu ya gharama wanazoingia wasailiwa na kuandaa vituo ambavyo vitapunguza gharama za wasailiwa kufika katika usaili wa mahojiano.
Nashauri Dodoma ingekuwa ni sehemu ambayo ingewapunguzia gharama wasailiwa, ikiwa kama utaratibu wa awali kikanda utakuwa mgumu kutekelezwa na TRA; ijapokuwa utaratibu wa kikanda ulikuwa utaratibu mzuri na rafiki kwa mtanzania hasa Yule wa Hali ya chini anayeomba ajira.
Naamini kwa uungwana wa taasisi Yetu nyeti hii katika kujenga Nchi Yetu itasilikiliza ushauri huu na kuutendea KAZI.
Naomba kuwasilisha.
TRA- Pamoja tunajenga Nchi Yetu.