Usaili wa TFF...Lol!

Usaili wa TFF...Lol!

Balantanda

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2008
Posts
12,480
Reaction score
4,775
I had a nice laugh at this guy,

Jamaa wawili walienda kuomba kazi Tanzania Football Federation, ikabidi mmoja mmoja aingie ili apewe interview. Jamaa wa kwanza mambo yakawa hivi;

Katibu TFF; mashindano ya kombe la dunia kwa mara ya mwisho yalifanyika mwaka gani?
Jamaa; 2002.

Katibu TFF; yalifanyikia wapi?
Jamaa; Korea kusini na Japani.

Katibu TFF; mchezaji alievuma sana ni nani?
Jamaa; Ronaldo.

Katibu ikabidi aulize swali la kijanja ; je unaamini kama yesu ni mtoto wa mungu?
Jamaa; wapo wanaokubali na wasiokubali ila mimi nakubali.
judith francis: Jamaa akatoka kwenda kumwambia mwenzake nae aingie lakini jamaa alietoka ndani akamfundisha mwenzake majibu ya yote. Jamaa wa pili nae akaingia na mambo yakawa hivi;

Katibu; ulizaliwa mwaka gani?
Jamaa; 2002

Katibu; ulizaliwa wapi?
Jamaa; Korea kusini na japani.

Katibu; Baba yako anaitwa nani?
Jamaa; Ronaldo.

Katibu; We chizi nini?
Jamaa;wapo wanaokubali na wasiokubali ila mimi ninakubali.

Katibu: Heeeeeeeeeheeeeeeee
 
Back
Top Bottom