Usajili: Clatous Chama arejea Simba SC

Atalazimika kupigania namba yake!! Lazima m
amshawishi kocha kwenye mazoezi. na siku akianzishwa aoneshe kuwa anastahili kuanza!! Kama amerudi akifikiri nafasi ilikuwa inamsubiri anaweza kuchanganyikiwa !!

Na ubaya zaidi jezi yake aliyoivaa anatisha kama upepo…. P.O Sakho, sijui atakibidhiwa uzi namba ngapi ila nahisi atakula 10
 
Babu alieshindwa soka morocco chama clatous amerudi simba na atapewa jezi namba 17 hii ni aibu kwa soka la tanzania kurudisha wachezaji walioisha kiwango kama chama daaah simba ina vitu vya kuiga kwa yangaaaView attachment 2080712
Endelea kupoteza Mb zako kupiga makofi upepo! Mkude alitimuliwa Stars kwa majungu yenu kama hayo, mkafikiri ataporomoka kiwango lakini mziki wake mpaka leo unawahenyesha!
Tunajua hatua ya Chama kurudi Simba imewavuruga sana hapo Jangwani lakini hakuna namna itabidi tu mpambane na hali yenu, taratibu mtazoea tu!
 
Babu alieshindwa soka morocco chama clatous amerudi simba na atapewa jezi namba 17 hii ni aibu kwa soka la tanzania kurudisha wachezaji walioisha kiwango kama chama daaah simba ina vitu vya kuiga kwa yangaaaView attachment 2080712
mchezaji aliyeisha hawezi kuwa man of the match huko alikotoka.

Mchezaji kushindwa mahali fulani yapo mambo mengi zaidi ya hilo la kiwango. Ila hayo kishabiki hakuna anayeweza kuongelea.

Pili wanaomhitaji ni Simba na wanajua Ni nini wanachokitaka kwake.

Mchezaji akishindwa Yanga anaweza akawa bora Simba au pengine. Ndiyo mpira ulivyo.
 
Kitakachomhukumu chama ni performance baada ya kurudi Simba na si maneno yetu humu au ya wachambuzi.

Yote humu na ya wachambuzi Ni km ramli chonganishi tu.
 
Nategemea Simba itarudi kwenye ubora wake, pengo la chama halikuwahi kuzibwa, mwenye nafasi yake kaja

Hongera wanamsimbazi kumrudisha Kijana home kwao
Lakini pia simba inahitaji striker,
Chama pekee hatoshi kuipa ubora simba
 
Nategemea Simba itarudi kwenye ubora wake, pengo la chama halikuwahi kuzibwa, mwenye nafasi yake kaja

Hongera wanamsimbazi kumrudisha Kijana home kwao
Benchi limemkimbiza huko Morroco, tuna safari ndefu sana, mchezaji aliyekosa namba Morroco huku Tanzania ndio tegemeo. Maajabu kwakweli.
 
Naonaa semaji la mchongoo limeshakurupuka uko nao kesho wanatambulisha mchezaji wakimataifaa haijawah kutokaaa,,,,msuva nani asiyemjuaa
 
Babu alieshindwa soka morocco chama clatous amerudi simba na atapewa jezi namba 17 hii ni aibu kwa soka la tanzania kurudisha wachezaji walioisha kiwango kama chama daaah simba ina vitu vya kuiga kwa yangaaaView attachment 2080712
Kama Ni aibu kumrudisha mchezaji Basi hili Walitangulia watani Zetu Yanga kwa kumrudisha Makambo ,sijui una kubaliana na Mimi mpaka hapo.
 
Hivi uliona wapi mtu Kesha pasi mtihani na kwenda chuo,halafu anaomba kurudi sekondari afanye tena mtihani.Mkolo peke yake.
 
Chama karudi Simba kwa mapenzi yake ila utopolo kinawauma hatari,wapo watu humu presha zipo juu kisa chama karudi sasa angalia wanavyotema shomba wakati kunatapishi la makambo limerudi tena garasa hamna kitu
 
Kama Ni aibu kumrudisha mchezaji Basi hili Walitangulia watani Zetu Yanga kwa kumrudisha Makambo ,sijui una kubaliana na Mimi mpaka hapo.
Tena akiwa kachoka kweli kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…