Usajili wa laini za simu kwa alama za vidole against ujumbe uliozagaa leo

Utapeli hautaisha milele.

Unaweza ukasajili line kwa wakala akakuambia imegoma. Utambishia?

Lakini kumbe ilikubali then hiyo line akaenda kupewa mtu mwingine.

Nmezungumza sababu nmeshakiona hicho kitu mara kadhaa.
Ebwanaee

Kwa hiyo akisema chochote kinachoonyesha utata niite polis maana hakuna namna nyingine
 
That is my point 👍

Na kwa watu wa Nida watueleze possibilities za hili kutokea au watutoe hofu in their own way.
Hiyo msg haijatoka nida.
Ni wahuni wameandika
 
Hapo sasa sijui... lakini ni salama zaidi kusaji line kwenye ofisi zao kuliko kwa hawa wanaopita mitaani.
Ebwanaee

Kwa hiyo akisema chochote kinachoonyesha utata niite polis maana hakuna namna nyingine
 
Ujinga mtupu, wanaiba na kidole chako kwenda kusajilia? Bogus kabisa waliosambaza huo upuuzi.
_______________________________________
IG: @marble_na_granite
 
Anything is possible in Africa, except Development and Selfishness
 
Chochote kinawezekana kwasababu matapeli ni wabunifu na wajanja zaidi kuliko wanaosimamia hiyo mifumo kwasababu tunaona mifumo yetu mingi bado inamapungufu kadha wa kadha.Mimi nashauri wahusika wabuni mfumo ambao utamwezesha mtumiaji kuingiza Jina lake na Namba ya kitambulisho chake nakuona namba zote zilizosajiliwa kwa jina lake ili kama kuna ambazo hazitambui atoe taarifa mahala husika.Tukiweza hilo tutaondoa namba nyingi mamluki.
 
Kama kuna mwenye namba ajaribu kusajili line hata ya mmewe au mkewe tuone kama atakuwa rejected na system
 
Mimi huwa nashangaa jitihada kubwa with a huge use of resources lakini wana-fail kwenye a very minor technicality. mfano ni nini kinachosababisha kushindwa ku-integrate hizi system zote. wakati mwingine huwa nahisi ni hujuma zinazosababishwa na baadhi ya watalaam.

Database ya NIDA Module ya National ID ni very important tool kwenye integration na mifumo mingine ya inayohitaji utambulisho nadhani sasa ifike taasisi zote ziwe integrated na NIDA kwa kuzingatia kuwa sehemu ya utambulisho ni very important karibu katika kila sehemu.
 
Jumbe nyingine hazina ukweli zaidi kuleta taharuki kwa jamii,,,,,hakuna usajili wa laini kwa finger print kwa sasa unaotumia copy,,,,, ni kitambulisho tu.
OK basi ni kitu gani kitasababisha "conflict" kwenye benki ya takwimu za lain kati ya NIDA, Biometrics etc.

Mi naona mtu anaweza kwenda halotel mwingine akaenda tigo na makaratasi hayo hayo akasajili tu.

Wajuzi tusaidie hapa
 
Utapeli hautaisha milele.

Unaweza ukasajili line kwa wakala akakuambia imegoma. Utambishia?

Lakini kumbe ilikubali then hiyo line akaenda kupewa mtu mwingine.

Nmezungumza sababu nmeshakiona hicho kitu mara kadhaa.
Hii kwangu ilitokea nilisajili ikagoma..hadi natoka sikufanikiwa kusajili..hapa sijui **** walakini
 
Acha kuwazibia Freelancers riziki kwa kuwaita vishoka. Kumbuka nao wale wanajitafutia kipato,hawaibi.
Na hakuna uwezekano wowote wa kuedit taarifa zako za ki- biometry.
 
Huu ujumbe unasambazwa na malayman.
Nasema hivi kwasababu ili kusajili namba ya kitambulisho pekee haitoshi kusajili bila kuweka alama ya kidole chako.

Mchambuzi.
Kabla ya kuwaita hao ‘malayman’ hebu fafanua kidogo hapo, kwani nikishapewa copy ya namba (kama ni copy anyway) nitakuwa pia sina vidole vya kubofya..?

Vinginevyo utuambie kama system inao uwezo wa kutambua kuwa ‘namba’ hii imetumika kusajili Kidole X, mleta mada anaweza kuwa na kitu cha kutafakari... ila ujumbe aliotumia kama ushahidi umeandikwa hovyo hovyo mno binafsi siwezi kuamini mwandiko wa hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…